Imani ya Ushirikina na Maisha ya Mwananchi

Ukitaka kujua kama yapo ama hayapo si umuingie tu huyo jamaa. Lakini usisahau kuja hapa kutupa taarifa baada ya utafiti wako.
 
Ukitaka kujua kama yapo ama hayapo si umuingie tu huyo jamaa. Lakini usisahau kuja hapa kutupa taarifa baada ya utafiti wako.

Itakuwa proof ya kisayansi kabisa; kazi kwako mleta mada- kwa nini uandikie mate wakati wino umejaa!
 
Kukosa elimu ya kutosha, hupelekea watu kukosa confidence in whatever they do......so kimbilio lao ni huo uchawi!

Wote wanaoogopa wachawi......na wao wanaabudu uchawi.......! Kama mtu huamini na huogopi uchawi hata utishwe vipi hakuna kitakachotokea kwako!

Uchawi to me ni more sychological than reality!....so wachawi hupenda sana kucheza na sychology za watu...hasa waoga, wasiokuwa na confidence!

Kwenye blue si kweli, watu wanaoongoza misafara ya ma-VX kwenda mlingotini wengi wao ni wasomi na wengine wana hata PhD.

Kwenye red it is a contradiction. Unasema uchawi is more sychological than reality, then unasema wachawi hupenda........ Yaani ukakataa kuwa uchawi upo then unakiri wachawi wapo.
 
Last edited:
Mzizi ama kweli wewe imani yako ndogo!Sifa moja kubwa ya mtu kama huyo ni kukuteka kiakili.
Akifanikiwa hapo kuwa unamuogopa ndo ushindi wake mkubwa.Kama imani yako nzuri tu na una uwezo wa kujiamini, ukaweza kumdharau hapo umemshinda na hataweza kufanya lolote chini ya mbingu , pengine akunyweshe sumu!

Watu wengi wanawaogopa watu kama hawa lakini kimsingi hawana madhara yoyote isipokuwa kuwatisha tu watu wengine, akifanikiwa katika hilo basi uliyetishwa ndio mwenye matatizo.
 
wengine hawakusudii kuwa wachawi unakuta kaanza kurogwa kweny position yake..na yeye anaangukia kurogana..au anatupiwa jini etc.. dunia hii ni chafu sana. uchawi exists people!
 
95% ya watanzania,wameshawahi kwenda kwa mganga, au kuchanjwa. wengi wa vigogo ni wachawi kw kutumia waganga sio wao wenyewe..wengine ndio wanaomba washushiwe na mikoba,wajigange wenyewe
 
95% ya watanzania,wameshawahi kwenda kwa mganga, au kuchanjwa. wengi wa vigogo ni wachawi kw kutumia waganga sio wao wenyewe..wengine ndio wanaomba washushiwe na mikoba,wajigange wenyewe

Lete source ya takwimu zako..kama huna itabidi uombe radhi waTZ kwa post yako, ukishindwa kufanya hivyo itabidi tuombe MODS wakupe haki yako..server ban.
 
Lete source ya takwimu zako..kama huna itabidi uombe radhi waTZ kwa post yako, ukishindwa kufanya hivyo itabidi tuombe MODS wakupe haki yako..server ban.
wewe acha kuwa in denial,wake up from that little bublble you call 'LIFE' or your driving me to think that 'truth hurts' did i hit home!?
 
wewe acha kuwa in denial,wake up from that little bublble you call 'LIFE' or your driving me to think that 'truth hurts' did i hit home!?

Unadhani JF ni kijiwe cha gahawa? Narudia tena lete source ya takwimu zako..au ukiri kuwa umezibuni mwenyewe ili tukupuuze kuanzia sasa..
 
huyo anayesema source ya takwimu mwenyewe tungekuwa tunamfahamu tukamkagua,tunaweza kuona tunguri kiunoni. asilimia zaidi ya tisini ya vigogo wote tz ni wachawi, ukianzia na mdau wa bagamoyo, yaani J opssss. sory. sijui nilitaka kusema nani?

ninao ushahidi wa vigigo wengi tu family friends, ambao wamekuwa wakiwaalika waganga kuja nyumbani kwao, anaweza akamlipia mganga toka sumbawanga au ukerewe anakuja analala home kwake hata wiki mbili anampika yeye tu. anaondoka na mimilion huyo mganga. nitajee? tena wengi wao ni ccm.ni jamaa zangu ninao uhakika na ninachoongea.
 
Mmh!! mjomba Uchawi upo sana tu !!! hata makanisani wanaupiga vita kwasabau unayumbisha imani za waaumini.
Kuuepuka jitahidi kuwa mcha mungu na ishike sana imani yako ya dini ili mungu akuepushie.......
Mjomba ...kuuzunguka mbuyu si kazi mjomba kazi ni kuukumbati.
 
Uchawi na ulozi upo na ishara zake ni nyingi na naweza kabisa ama kukubaliana na takwimu akisi zilizotolewa kuhusu jambo hili katika jamii yetu ya Tanzania. Nitataja baadhi; Vita vya Majimaji ni ishara kuwa uchawi ulitumika na implication zake walikufa kama headless chicken....je kuna atakayepinga? Je hili linahitaji uthibitisho? Kwa mantiki hiyo basi wanaojaribu kutafuta takwimu za mbaaali inaonyesha historia ya nchi hawaijui and yet they are Tanganyikans. Uchawi upo na ni product ya ujinga. Kwa mwenye ufahamu na aelewe hivyo. PERIOD!!!
 
...Hivi jamani ni kweli haya mambo ya ndumba kazini yanasaida kweeli? ...

...inaonekana tayari ushaamini mambo ya 'ndumba-nangae!' huko ulikotoka, ...hilo la ndumba kazini ni hitimisho tu.

Ni sawa na kukuta kibao getini HATARI MBWA MKALI nawe ukageuza njia kurudi ulikotoka!
 
Hivyo halloween nao ni uchawi wa nchi za Magharibi? Kuna sikukuu kila octoba huko Nchi za magharibi wanasherekea huo uchawi, hivyo chimbuko la uchawi huko africa lililetwa tu.
 
Lete source ya takwimu zako..kama huna itabidi uombe radhi waTZ kwa post yako, ukishindwa kufanya hivyo itabidi tuombe MODS wakupe haki yako..server ban.

Mtindi , this guy only needs to be educated, nafikiri yeye anatoka kwenye jamii inayoendekeza jadi hiyo iliyopitwa na wakati.Server ban haitasaidia sana , elimu can do the trick.
 
Mtindi , this guy only needs to be educated, nafikiri yeye anatoka kwenye jamii inayoendekeza jadi hiyo iliyopitwa na wakati.Server ban haitasaidia sana , elimu can do the trick.

Mkuu kuna mhadhiri mmoja pale UDSM anaitwa Dr.Simion Mesaki yeye alifanya utafiti katika haya mambo ya uchawi nadhani yeye atakuwa na jibu rahisi la uwepo wa uchawi ndani ya maeneo ya kazi na katika mazingira yetu.
Na tasnifu yake ya shahada ya Falsafa ameandika mambo mengi yanayoendana na uchawi.

Sasa kama hii dhana ya uchawi hisingekuwepo sidhani kama huyu bingwa angefanya tafiti hizi.
 
Back
Top Bottom