Hali ya ushirikina inaonyesha ishara kuwa kwenye jamii kuna matatizo mengi zaidi! Shinikizo mbalimbali katika jamii zinaleta hali ya watu kutafuta suluhisho au jawabu la matatizo yao kwa njia mbalimbali, nyingi ambazo si nzuri. Ni muhimu wana jamii kutafuta chanzo cha matatizo hayo na kuyatafiti kwa undani.
Mkuu Kitila,
Nimuhi kwa sisi kama wana jamii kuchungua kwenye hili,na tujue ukweli wa maswala haya.
Nadhani sio vibaya niki-share my experience hapa,
"Miaka mimi nyuma wakati niko mdogo huko kijijini kwetu,nyumbani kwetu aliletwa Mganga wa kienyeji,jamaa akatuchanja mwili mzima na kiwewe chake.
Mimi nilikua wamwisho na kwa kua nilikua mdogo sikuweza kuvumilia maumivu ya kiwembe kile nakumbuka kugoma sana mpaka wakanishika ili nichanjwe.Kwa sababu ya maumivu na kuona kama nimeonewa hayakunitoka kichwani mambo yale,siku mmoja nikiwa na Mzee peke yetu nilimuuliza HIVI NI KWANINI YULE JAMAA (Mganga) alituchanan chana na viwembe?
Jibu la MZEE lilikua lefu na maelezo mengi ila kwa kifupi aliniambia "ile ni dawa ya kujikinga na wachawi ambao walikuwapo pale kijiji" .
Mimi niliendeleza maswali mfululizo kwa mzeenikimuuliza mambo mengi kuhusu jibu lake mfano nakumbuka kuuliza,"Yeye anadhani nani au jilani yetu gani pale ni mchawi,na kwanini hwaonekani na maswali mengi ya kitoto?"
Aliishia kunia mbia
"subiri ukikua utayaona na kujua"
Nina miaka Mingi sasa sijawahi kuona mchawi live ila nimesikia mengi na kusoma mengi juu ya Ulozi lakini sina proof yeyote mpaka sasa.Ila critical thinking na experience ya maisha kwenye nyanja nyingine tells kwamba "kunapo Fuka moshi,ujue kunawaka",
Jamii inazidi kuelemea na kulizungumza sana jambo hili kila siku na hivyo kupelekea kwamba huenda kuna ukweli fulani katika hili.Na nikazi yetu sisi kuja na mawazo furani ili kuweka swala hili bayana na sio KUKUBARI TU au KUKATAA kwamba hizi ni imani TU za kishilikina tu kwa sababu shule tumefunzwa hamana vitu hivyo.
Nimazo yangu sehemu fulani ya hili swala lazima kutakuwepo na ukweli wa mambo haya na kama michango ya wachangiaji wengine kwamba hata vitabu vya dini vime bainisha uwepo wa m,ambo haya sasa tukiendelea kukataa au kubari bila ya kua na misingi ya HOJA za kukataa ama kukubari hatujitendee haki sis na wale tuwaelezao haya.