Imam Abbas | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Imam Abbas

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Viper, Oct 11, 2012.

 1. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Je mnamkumbuka huyu mkongwe wa hiphop ya bongo ...?! moja ya nyimbo yake maarufu ni BILA SANAA . Leo nimepata shauku sana ya kujua huyu kijana yupo wapi na anafanya nini..?! ilibidi ni google na nikapata story mbili za imam Abass lakini hazijanipa mwanga yupo wapi sasa.. nakumbuka hii thread https://www.jamiiforums.com/entertainment/8100-hawa-wako-wapi-sasa-6.html#post114063kipindi cha miaka 2008-2007 wachangiaji wa hii thread kama bado wangali active kutakuwa na wachache wana majibu


  story ya kwanza muandishi anaelezea mashairi ya imam abbas "bila sanaa"

  BILA SANAA... sikiliza hapa


  Hivyo ndivyo mashairi ya msanii mkongwe wa Bongo Hip Hop, Imam Abbas yanavyoanza kwenye nyimbo yake ya ‘Bila Sanaa'. Nadhani lile swali la nini nafasi ya Bongo Hip Hop katika jamii yetu litaanza kupata maana kupitia nyimbo hii. Pamoja na bado wapo wajinga wachache katika vyombo vya habari, wanaoita Bongo Hip Hop, muziki wa kufokafoka, bila kujua hii ni aina ya fasihi simulizi. Taswira ya fasihi katika nyimbo hii ni ya kipekee, ambayo inaibua maswali muhimu na kuonesha mustakabali wa vijana wa leo.  [​IMG]  ‘Bila sanaa' inakupa mtazamo wa vijana walio wengi katika Tanzania ya leo, kwani maisha yao ni kama kuwa na "panga shingoni". Panga hilo, laweza kuwa la kibaka akimwibia raia, au panga hilo laweza kuwa mafisadi wanaodhoofisha maendeleo; hivyo rushwa zao na ubinafsi wao ukizidi kuacha taifa lenye vijana wengi matatani.


  [​IMG]

  Ugumu wa maisha, hasa kwa vijana unatokana na sababu mbalimbali. Wale walio bahatika, wakasoma na wenye vipaji, wanahemea kupitia elimu yao au sanaa yao, kama hii ya Hip Hop. Lakini wengi wa vijana wapo kwenye fungu la wanaoishi kwenye mazingira magumu na hatari. Hao sasa, ndio wale ambao kila siku wanatamani wangebaki "utotoni", kwani "Bongo motoni;"kwani wakiwa wezi kweli watachomwa moto

  Lakini kwanini tuishi kama tupo motoni? Mtu unabaki ukijiuliza, hivi ukimya wetu vijana ndio unatufanya tuonekane mafala, au tumekubali yaishe kuwa sisi ni watu dhaifu. Labda moja kati ya sababu kubwa zinazotufanya tusiamke, ni hofu kuwa, kelele zetu "zitapotea kama moshi wa udi," bila kusikiwa na hata kuleta mabadiliko yo yote.  Vijana waliosoma ni wachache, ajira zenyewe ni chache, na kwa wale ambao "maisha piga mashuti," wanajikuta wanashindana na Wachina kwenye umachinga. Msanii II Proud enzi hizo aliuliza "ni wapi tunakwenda, tu.. tunakwenda" kipindi hicho ambapo tabia ya kuzamia meli kwa vijana ndiyo ilikuwa imeshamiri. Leo hii uzamiaji meli sio ishu tena, kwani tumekubali kubaki nyumbani na kuwa watumwa.  Sasa je, utumwa huu utakuja kufika kikomo? Hawa viongozi je, viongozi wanaodharau vijana, wanaodharau mchango wa Bongo Hip Hop kwa vijana na jamii kwa ujumla, hivi hawajui hatari ya dharau zao? Leo hii, tunaweza kuulizana maswali tu, ya "tafakari je, ningevunja mlango wako, juu yake kibano, kisha vitu msanyo," kupitia nyimbo hii. Lakini, kesho ufisadi ukazidi, maisha ya vijana yakazidi kuwa matatani, unadhani vijana tutabaki tu kuwa kwenye "kona ya mtaa," huku"moshi wa msuba unapaa, umeishia ukizubaa," au hata wao mafisadi watajikuta wakiwa wamewekewa mapanga shingoni. Labda hilo ndilo tunalohitaji lifanyike, badala ya kugeuziana visu sisi wenyewe kwa wenyewe.


  [​IMG]
  Bila ubishi, sisi vijana na hao mafisadi tuishukuru sanaa, kwani ‘Bila Sanaa', Imam Abbas anajadili maisha yangekuwa vipi; labda angekuwa mkabaji, mteja, mwizi, muuaji, lakini kama Lupe Fiasco msanii wa Marekani, Hip Hop Saved His Life.
  Mwisho, Imam Abbas anaonya kuwa, "taifa la leo, majambazi wa kesho," kama viongozi hawatachukulia kilio cha vijana kwa umakini. Kwani siku moja itatutabidi tujenge ukuta, wakati nyimbo kama ‘Bila Sanaa', zinatuwekea wazi nyufa ambazo zinatakiwa kuzibwa. Mwisho wa siku, ukweli ni huu, matatizo ya vijana hayatatuliwa yote leo, kwani hata Roma haikujengwa kwa siku moja. Lakini sasa, juhudi lazima zianze leo, kwani kama nchi hii itateketea, basi sote tutateketea nayo, na tusisahau wala kudharau uwezekano huo.  sorce ya hii story http://www.vijana.fm/2010/08/19/bila-sanaa-imam-abbas/


   
 2. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Wimbo unaitwa Mitaa ya kati na sio bila sanaa kama unavyosema. Alishirikiana na Juma Nature, mara ya Mwisho nilimuona ktk Channel O Hiphop free style battle 2007 ambapo alipambana na akapata kuwa mshindi wa pili.
   
 3. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2012
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  story ya pili

  sanaa imeniokoa

  hapa mwandishi analinganisha track mbili moja ya mtoni nyingine ya bongo! hapa anamzungumzia imam abbas na msanii Lupe ..

  Imam Abass Bila sanaa - sikiliza hapa

  Lupe Fiasco feat. Nikki Jean - Hip-Hop Saved My Life


  Imam Abbas anatupa hali halisi ya maisha ya kitaa yalivyo, kama sanaa isingemtoa kutoka huko. Mhusika katika nyimbo ya Lupe Fiasco anatupa hadithi ya maisha yake na yale ambayo yanamzunguka. Pamoja, vijana hawa wawili wapo mitaa tofauti, mmoja kwenye ghetto iliyopo Marekani, na mwingine kwenye mitaa ya Uswazi Tanzania. Lakini, je, ni nini kinawaunganisha ukiacha kuokolewa na sanaa ya Hip Hop?

  Mhusika (kwenye ‘Hip Hop Saved My Life’) na Imam wote hawapendi maisha ya mtaa, na mhusika anaweka wazi kuwa “I don’t like where I be”. Imam anatudokezea kwanini kitaa siyo sehemu ya kuishi, kwani “tunaishi kijeshi”. Na ukifuatilia maisha na kigangsta ya Marekani, ni kama kuwa mjeshi vitani. Video ya wimbo wa Lupe inapoanza, tunaoneshwa vijana wakiwa kama kwenye “kona ya mtaa”, labda wakisubiria madili. Imam anaendelea kwa kutuelezea ni nini vijana wanakuwa wakifanya kitaani wakiwa kijiweni. “Moshi wa msuba unapaa”, huku vijana wakiwa wamezubaa. Taratibu hoja ya uhaba wa kazi kwa vijana inajidhihirisha katika hizi jamii mbili.
  [​IMG]


  Mhusika ni kijana ambaye ni Mmarekani mwenye asili ya Kiafrika, na Imam ni kijana wa Kitanzania. Ufahamu wa sehemu wanazotoka unaweza kuanza kujibu maswali kadhaa, kama hili la tatizo la ajira. Mwanzoni kabisa Imam anakwambia, “kila kitu siasa”. Siasa anazozizungumzia zinaweza kuwa ni hizi za vijana kutokupewa nafasi na kusahauliwa na jamii. Siasa hizo zinaweza kuzilinganishwa na siasa za kigabuzi wa rangi zilizopo Marekani, ambazo zinabagua watu weusi katika shughuli za kiuchumi, au kwa maneno mengine ‘institutionalized racism‘


  Tatizo hili linaweza kuwa moja ya sababu ya mhusika wetu kuwa kwenye hali aliyopo — labda. Kwa upande wetu, institutionalization inaweza kuwa ni mila na desturi zetu ambazo zinawapa watu wazima — hasa wanaume/wazee — nguvu kwenye jamii; pamoja na nafasi mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na hata kijamii.  Mhusika anatupa undani wa maisha yake kidogo, baba yake anatumikia kifungo cha maisha, na kaka yake amehukumiwa kunyongwa. Mwenyewe anasema, “daddy servin life and a brother on a row”. Pamoja hatujui makosa yao, lakini tunaweza kukisia labda kaka yake aliua mtu, kutokana na hukumu aliyopewa. Hapa tunapata picha ya maisha ya kitaa, ambapo inawezekana kaka mtu alikuwa kwenye gang.Na hivyo kujikuta akiua mtu au watu wa gang pinzani.


  Imam anatuonesha fikra au dhana ya kitaa, “watoto wadogo, visu nje nje”; kwani uhalifu umegeuka ajira kwa vijana! Pamoja vibaka wa Tanzania ni “visu nje nje”, wenzano wa Marekani ni bastola nje nje. Lakini vijana hawa wote wana hiyo dhana ya “niguse kidogo, nikuumize makusudi”, kutokana na misongo ya maisha. Nasema hivyo, kwani mauaji mengi ya vijana Marekani, hasa kwenye gang violence, ni kutokana na vitu vidogo, kama jinsi tunavyouwa vibaka ambao wameiba vitu vidogo sana, kama vile kuku.  Bahati nzuri mhusika wetu hataki kuishia jela kama baba na kaka yake. Imam pia anasihi vijana kubadili “mifumo ya maskani”. Mhusika anatambua akiendelea kuishi maisha ya mtaa anaweza kuishi jela, au kuuwawa kwa bastola, kwani ana mifano hai kutoka kwenye familia yake. Wakati kwa Imam, akiendelea kukaa kwenye kona, akisubiri kukaba na kuiba, anaweza kuchomwa moto na wananchi wenye ‘hasira kali’. Hii ni mojawapo ya sababu ambazo zinafanya vijana watake kuachana na maisha ya mtaa, na kuishi maisha ya kistaarabu.  Imam anazama kwenye suala la uhalifu, na sisi tunaweza kuchukulia hilo ndilo jambo kuu linalomfanya akazanie sanaa ya Hip Hop ili ‘atoke’. Mhusika wa Lupe anazidi kutuelezea undani wa maisha yake, ambayo unatupa sababu yake kuu ya kukazania sanaa. “Cryin from the next room, a baby in need, of some pampers and some food and a place to sleep”. Mhusika tayari ana majukumu, sio kama yale ya Jay Mo, lakini tayari ana mtoto huku akiwa na umri wake mdogo. Hili sio geni katika jamii yetu pia. Huku wasichana wengi wakiachwa wenyewe kulea.


  Mhusika anataka kuwa tofauti, na kuwa mfano wa kuigwa. Baba yake yuko jela, hivyo inawezekana alilelewa na mama yake tu. Hili linaakisi mambo yanayotokea kwenye jamii yetu sisi pia; wakina baba hawapo, au kama wapo, hawajiwajibishi ipasavyo kulea watoto wao.  Hivyo, mhusika anataka kulea mtoto wake pamoja na mchumba wake. Hataki mtoto wake akue bila baba, kwasababu baba alifungwa jela au aliuwawa mtaani katika vita ya magenge. Kukubali kubeba majukumu inawezekana pia ilimfanya mchumba wake asitoe hiyo mimba, kitu ambacho wasichana wengi kwenye jamii yetu hufanya. Mhusika, anavunja cycle ya familia zenye mzazi mmoja au single parent homes. Hii inaleta taswira mpya na ngeni, kwani katika jamii za Wamarekani wenye asili ya Kiafrika vijana wengi, kama wa hapa nyumbani, hukimbia. Badala yake, mhusika anaonesha kuwa vijana wanaweza kuwa makini, huku akijitoa kwenye kundi la wale ambao hukimbia majukumu pindi yanapojitokeza.
  [​IMG]  Majukumu ya kulea yanamfanya mhusika ajitahidi ili afanikiwe katika sanaa, na aweze kulea mtoto wake. Ameamua kushika “kipaza” na “kupiga kelele”, lakini Imam anasihi vijana kukazania elimu. “Shika darasa” na “kupiga kengele”, kwani “sio lazima kughani”. Imam analeta hoja ya elimu kitu ambacho Lupe hajagusia. Kwanini? Jamii ya Kimarekani ina stereotype kwa vijana weusi, kuwa ili wao wafanikiwe basi wajiingize kwenye fani ya Hip Hop au wafanye michezo. Hili suala hatuna kwenye jamii yetu, ingawa kasi na idadi ya vijana wanaoingia kwenye Hip Hop inaongezeka kila siku; inaonesha ni “dini iliyokubalika”, kama Afabde Sele alivyosema. Sanaa imekuwa kimbilio la vijana wengi wa kitaa, kitu ambacho kinaweza kutufanya tujiulize, kwani shule zimefungwa na elimu imeenda likizo?

  Mhusika na Imam wote wanazungumzia jinsi Hip Hop ilivyookoa maisha yao, na huku elimu ikigusiwa juu juu tu, wakati huo ndio ufunguo wa maisha. Umasikini wa vijana hawa wawili unaweza kuwa ni chanzo cha kukimbilia Hip Hop badala ya elimu. Kivipi?  Shule za inner cities za Marekani, ambako ni sawa na Uswazi, sio nzuri. Documentary ya ‘Waiting for Superman‘ inaliezea hili tatizo vizuri. Wakati filamu ya ‘Freedom Writers‘ inatuonesha jinsi mfumo wa elimu unavyobagua matajiri na masikini, huku wengi wa masikini hao wakiwa vijana weusi. Hivyo, labda ndio maana kukimbilia Hip Hop ilileta maana zaidi kwa muhusika, badala ya kwenda shule. Hapa nyumbani, inawezekana, wengi hawawezi kulipia ada za shule nzuri, ambazo kawaida ni shule za binafsi, na hata hiyo mikopo ya vyuo vikuu ina mjadala. Shule za kata kwa upande mwingine zina matatizo yake mengi. Labda ndio maana Hip Hop imekuwa kimbilio la wengi, katika kujikwamua kutoka kwenye umasikini. Lakini, kama mtu hana kipaji cha kuandika mashairi na kughani, na shule imemshinda, ategemee nini?  Halafu tunaona jinsi mhusika anavyopatwa na vikwazo vingi (kama wasanii chipukizi wa hapa nyumbani), akijaribu kufikia malengo yake katika fani. Bahati nzuri familia yake inajitolea na kumsaidia. Mchumba wake akiwa “his biggest fan”, kitu ambacho kinafanya nijiulize, jamii yetu inakubali sanaa kwa kiasi gani, hasa hii ya Hip Hop?

  Kama kijana akiamua kuwa msanii, unadhani familia itajitolea kumsaidia, kama mama yake mhusika na mchumba wake walivyofanya? Ni kweli kuwa soko la sanaa ya muziki Tanzania sio kubwa kama ya Marekani, lakini, je, litakuwa kubwa lini na kuweza kuanza kutoa ajira za uhakika kwa vijana wengi, kama sisi wenyewe hatuijali hii sanaa inavyotakikana?

  [​IMG]  Imam na mhusika wa Lupe wote wanatuonesha jinsi Hip Hop ilivyokuwa ni sauti ya wanyonge, kwani wote ni vijana masikini wa kitaa, ambao wametumia sanaa kujitetea, badala ya kujihusisha na mambo mabaya. Wametafuta njia mbadala, hivyo kuwa mabalozi wazuri wa vijana walio kwenye mazingira magumu. Wametumia Hip Hop kama nyenzo ya ujasiriamali ili kuweza kujikimu. Mhusika anataka kuwa na maisha kama yale anayoyaona kwenye TV, lakini kama vijana wa nyumbani, wengi tunasahau kuwa maisha tunayoyaona kwenye “MTV” ni maisha ya vijana wachache sana, na hiyo American Dream ni ndoto ambayo kwa wengi; na itaishia kuwa ni ndoto tu.


  Pia, uhalisi wa hadithi zao, zinaonesha jukumu la Hip Hop katika jamii, na hilo ni kuongelea Hali Halisi, au kama mhusika anavyosema “I write what I see”. Vijana wote wawili wapo kwenye mazingira magumu lakini hawakukata tamaa. Wote wametumia sanaa ya Hip Hop kujikwamua kimaisha.


  Wakati wasanii wengine wanatumia sanaa kujipatia umaarufu, wapo wengine wanatumia sanaa kwa mambo ya msingi kama anayoyataja muhusika mwishoni, huku Imam akitumia kipaza kuokoa vijana wa mitaa ya kati kwa kupitia ujumbe wa wimbo wake. Je, wewe unatumia sanaa ya Hip Hop kwa nia gani na malengo yako ni yapi?  sorce ya hii story http://tzhiphop.com/2011/06/utandarhymes-sanaa-imeniokoa/
   
 4. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Huyu,
  Na jamaa mwingine anaitwa Salu T
  Bila kumsahau dolla soul
  Sio vijana wa siku hizi sijui
  Stamina, sijui sheta
   
 5. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2012
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  alafu juzi kati nacheki mtandaoni nakuta DIMOND kabongo`a anaonesha nguo ya ndani ... inasikitisha vijana wa leo wanapopeleka mziki huu! ambao umehasisiwa na kuwekewa misingi na kina SUGU, SAIGONI , KWANZA UNIT, ETC!

  DIMOND KAMA ANASOMA HII THREAD "SHAME ON YOU ....
   
 6. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
   
 7. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,094
  Likes Received: 1,269
  Trophy Points: 280
  ..kwenye bold yuko USA..
   
 8. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2012
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Haha!! Kwa nini man
   
 9. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Si ndo kwanza ameanza English course
   
 10. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2012
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  ah! lakini ni msanii anayezunguka dunia muhimu ajifunze lugha za watu
   
 11. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #11
  Oct 16, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145

  nlitamani kumtia k.idole ila nilikuwa mbali nae
   
 12. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #12
  Oct 16, 2012
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Haha! Mkuu huo utakuwa umende sasa
   
 13. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2015
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Sikuhizi kuna wakina ally kiba
   
Loading...