David ngayanimo
Member
- Nov 8, 2018
- 18
- 19
FANANI AFUNGUKA WAZI, JINSI HARD BLASTERS CREW (H.B.C) ILIVYOMJENGA PROFESSOR JAY, "1990s"..
"HARD BLASTERS ndio kundi lililombeba na kumsaidia Prof. Jay, siyo Prof. Jay kuisaidia Hard Blasters..."
“Hard Blasters, ndio kundi lililombeba na kunsaidia Prof. Jay siyo Prof. Jay kuisaidia Hard Blasters, kwasababu Proj. Jay amekuja na tukafanya naye wimbo wa kwanza mwaka 1995 kwenye albamu ya Blasters aliingia kama featuring na alikuwa ana aanandika sana Kiingereza na kwenye uandishi wa Kiswahili mimi ndiye nilikaa naye, albamu ya ‘Mwanzo’ na tulimpa nafasi aonekane na bado tukampa platform atoke na albamu yake”
Fanani, member wa kundi la zamani la Hard Blasters Crew (HBC) alilotokea Legend, Profesa Jay, Fanani alikuwa kwenye mahojiano Mjini FM.
Hayo ni maneno ya Fanani wa Hard Blasters Crew (H.B.C) aliyoyasema kwenye mahojiano yake na Mjini FM, na kwa hakika yameibua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau wa Hip Hop ya Tanzania.
Kwa mujibu wa Fanani, mwaka 1995 Professor Jay alishirikishwa kwenye kazi za H.B.C akiwa kama msanii wa "featuring". Anasema kipindi hicho Prof. Jay alikuwa anaandika zaidi kwa Kiingereza, na katika upande wa mashairi ya Kiswahili walifanya kazi pamoja hadi kufikia hatua ya kumpa nafasi kwenye albamu na baadaye kupata jukwaa la kutoka kama msanii binafsi.
Kauli hii inatukumbusha jambo moja muhimu; nyuma ya kila msanii mkubwa mara nyingi kuna kundi, mazingira au watu waliompa nafasi ya kwanza kuonekana.
Lakini pia kuna upande mwingine wa mjadala.
Wapo wanaoamini kuwa ingawa H.B.C ilichangia safari ya mwanzo ya Professor Jay, ni mafanikio ya Prof. Jay ndiyo yaliyoendelea kulifanya jina la Hard Blasters Crew lisahaulike katika historia ya Bongo Hip Hop.
Mfano kama ule wa The Wailers na Bob Marley. The Wailers walikuwa sehemu muhimu ya safari ya Bob Marley, lakini mafanikio ya Bob Marley nayo yalilifanya kundi hilo likumbukwe duniani kote. Mmoja hawezi kutenganishwa kabisa na mwenzake.
Hivyo basi, katika historia ya Bongo Hip Hop, pengine si suala la nani alimjenga nani zaidi, bali ni jinsi walivyochangiana katika safari ya mafanikio.
🔥 SWALI LA UKWAJU WA KITAMBO:
Je, bila H.B.C Professor Jay angekuwa Professor Jay tunayemfahamu leo?
Au je, bila Professor Jay, Hard Blasters Crew ingekumbukwa kwa kiwango hiki mpaka leo?
Tupe maoni yako 👇
#UkwajuWaKitambo
#Tunakurudisha
#BongoHipHop
#ProfessorJay
#HardBlastersCrew
#HipHopYaTanzania
Ukwaju wa kitambo
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202