Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 85,879
- 145,863
Samahani. Haina haja ya kupaniki. Hatushindani. Tunajadili tu. Sio kuwa nimeshindwa kutoa majibu ila hata nikisema hivi au vile, majibu yangu yata-base kwenye Biblia inayosema Mungu ni Roho nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Pia, si mimi nisemaye mtu asiyeamini uwepo wa Mungu ni mpumbavu, again ni Biblia hiyo hiyo ninayoiamini mimi 100% inasema asemaye hakuna Mungu ni mpumbavu.
Sasa kwa vile wewe huamini uwepo wa Mungu (upumbavu kwa mujibu wa Biblia ninayoiamini), basi si rahisi tukaelewana. Hutayaamini majibu yangu maana huamini Uwepo wa Mungu, hivyo sijashindwa kujibu maswali yako.
Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aachie watu wafe kwa ugonjwa kama Ebola?
Nikikwambia watu walioandika biblia walitaka kuwashikia akili wapumbavu wanaoogopa kuitwa wapumbavu kwa kuandika "mpumbavu amesema hakuna mungu" na kwa sababu wewe ni.mpumbavu unayeogopa sana kuitwa mpumbavu kuliko kuwa mpumbavu utajibu vipi?