Image of virgin Mary grows on tree

Image of virgin Mary grows on tree

Umenena vizuri. Lakini hajajibu swali la msingi, naomba unijibu:

Bikira Maria yuko hai kama alivyo Musa na Eliya huko mbiguni?

Kama ndiyo, unaweza ku-justify kwa angalia mstari mmoja wa Biblia?

Kama hayuko hai, point iko wapi kuwasiliana na mfu?

Pia naomba jibu, kuna shida gani mkiomba kwa Yesu moja kwa moja?

kuna maswali mengi ningekuuliza but ngoja nianze na haya,
Eliya pekee ndiye aliyepalizwa mbinguni bila kufa kwa mujibu wa hao watatu uliowarefer hapa, lakini musa alikufa na sehemu ulopata kwa bible inayomuongelea musa ni pale alipokuja yeye na eliya wakazungumza juu ya kifo cha yesu mlimani...wakat yesu akiwa na wanafunzi wake wale watatu...
sasa swali je waamini katika ufufuo?if yes why useme utaombaje kwa wafu? kwani yesu alipomwambia yule mwizi pale msalabani amini amini nakuambia leo hii utakuwa pamoja nami paradisoni in maana wafu wanawasiliana na kuonana?au unadhani yesu alipokufa kwa zile siku 3 alikuwa mfu completely?
 
Kama hujui jibu la swali unakubali kitu usichokielewa.

Unaamini Virgin Mary na utakatifu wake, lakini huwezi kuelezea kwa.nini mama huyu na utakatifu wake wote na uwezo wake wa kuwapa Waafrika masikini dawa wasife kama nzi kwa Ebola hajitokezi Monrovia Liberia awape dawa masikini hawa anaenda kutokea sehemu nyingine.

Swali lako la shetani na binadamu nani katangulia lina assume kwamba mimi naamoni katika kuwepo kwa shetani na mungu.

Mimi sikubali kwamba shetani yupo, sikubali kwamba mungu yupo.

Kwa hiyo swali lako kwangu hali apply.

Ukifimiri kwa kutumia akili na kuacha mambo ya mapenzi ya dini pembeni utaona huyu mungu wa waislamu na wakristo ni kamba tu.

Hawezekaniki.

Ndugu, uko serious?
 
Sawa twende taratibu.
Mimi nina mahusiano ya Ki DNA na mama yangu, mimi siku exist before ya mama yangu, mimi sikumuumba mama yangu, mimi si Mungu wa mama yangu.....
U-mama wa Maria kwa Yesu si sawa na U-mama wa mama yangu kwangu

twende taratibu.

asante kwa hiyo wataka kuniambia maria alikuwa kama kasha tu la kupitishia/kubebea mzigo?
tuanze na maswali rahisi, kwa nini ilikuwa yeye na si mwingine?
na huko kutokuwa na mahusiano ya ki-DNA na maria nani alikuambia ni kweli? nifahamuvyo mie kwa sayansi yangu duni (mind you nimegraduate kwa degree ya Engineering Biotechnology) ili mtoto awepo/afanyike kunahitajika sperm and egg, sasa yesu hakukuwa na sperm from a man, je leo pia wataka kutupa ufunuo mpya kuwa hakukuwa na egg from a mother?
je ndugu yangu wataka kuchanganya concept ya roho na mwili?
maana wengi pia hawaelewi concept hii ya roho na mwili katika biblia. unakaribishwa kwa ufafanuzi zaidi wa chochote.
 
Ndugu, uko serious?

Why should you think I am not?

Have I slaughtered some sacred cow or something?

To the contrary, you might be the one who is not serious. Upholding something without understanding it.
 
Sio lazima awe na nafasi. Pale Ikulu uliwahi kusikia chochote kuhusu mama wa prof?

hujasikia kwa kua hujajifunza zaidi kuhusu professor. ila kama wataka kumjua zidi professor amini amini nakuambia ni lazima pia utamjua na mama yake.
 
Wanduguueee Je, tuwasaidieni hapo ? !!!! basi mkihitaji Msaada Sie jirani zenu tupo Standby anytime / 24/7.
 
kuna maswali mengi ningekuuliza but ngoja nianze na haya,
Eliya pekee ndiye aliyepalizwa mbinguni bila kufa kwa mujibu wa hao watatu uliowarefer hapa, lakini musa alikufa na sehemu ulopata kwa bible inayomuongelea musa ni pale alipokuja yeye na eliya wakazungumza juu ya kifo cha yesu mlimani...wakat yesu akiwa na wanafunzi wake wale watatu...
sasa swali je waamini katika ufufuo?if yes why useme utaombaje kwa wafu? kwani yesu alipomwambia yule mwizi pale msalabani amini amini nakuambia leo hii utakuwa pamoja nami paradisoni in maana wafu wanawasiliana na kuonana?au unadhani yesu alipokufa kwa zile siku 3 alikuwa mfu completely?

Nashukuru kunijulisha kuwa ni Eliya pekee aliyepalizwa. Ila ni kweli pia kuwa Musa na Enok wako hai mbinguni.

Naamini katika ufufuo. Lakini Biblia imeweka wazi kuwa ufufuo una majira yake yatakuja. Sio mtu afe leo then immediately afufuliwe aendelee kuishi peponi. Wafu hawako hai (wamekufa) mpaka hapo Yesu atakapowafufua siku ya mwisho.

Mfano wa Yesu na yule mwizi msalabani, maana yake ni kuwa alimsamehe na amempa pas ya kuurithi ufalme wake (siku ya mwisho na watakatifu wengine waliolala katika Yesu Kristo) sio kuwa yeye ametangulia!! Ndio sababu walikufa wote lakini aliyefufuka ni Yesu peke yake, yule mwizi alibaki mfu mpaka leo anasubiri ufufuo ila yeye ana advantage kuwa ataingia mbinguni maana Mungu alishamwambia pale msalabani.
 
hujasikia kwa kua hujajifunza zaidi kuhusu professor. ila kama wataka kumjua zidi professor amini amini nakuambia ni lazima pia utamjua na mama yake.

Kwa nini bikira Maria hatokei Monrovia Liberia awape watu dawa ya Ebola wasife kwa mafungu kama nzi?

Uwezo anao, upendo anao, kwa nini hatokei huko anaenda kutokea Iowa?
 
Naamini maisha baada ya kufa. Lakini sio immediately baada ya kufa ni mpaka siku ya ufufuo ndugu yangu. Kwa sasa maria hayuko hai. Ni mfu. Hata hao watakatifu wengine akina Petro, Yakobo, Yohaba, hata baba wa imani Ibrahim wote ni watu wanasubiri ufufuo. Hivyo maria ni mfu.

kama hivi ndivo unavyoamini, je tuseme yesu asingebadilika sura pale mlimani na kwa sababu ya tukio hilo naamini wewe ndo ulijua kuwa Musa yu hai mbinguni je ungekuwa na hadithi ipi hapa ya kusema?(Maana hakika hapa ungesema pia Musa ni mfu, au kuna mahali umeona kwa Biblia Mungu alimfufua Musa?) kaka nakukaribisha uje nikufundishe neno (kama uko Dar, najitolea bure tufanye kusoma biblia na kufundishana pamoja) maana kuna maeneo mengi huielewi biblia ndugu yangu.
 
Kwa nini bikira Maria hatokei Monrovia Liberia awape watu dawa ya Ebola wasife kwa mafungu kama nzi?

Uwezo anao, upendo anao, kwa nini hatokei huko anaenda kutokea Iowa?

Swali lako ndugu linatofauti yoyote na kusema kama Mungu anapenda watu na anauwezo kwanini anaacha watu wanakufa sana Palestina na sehemu zingine za dunia? Au mbona wanasayansi wanahangaika kupata dawa ya UKIMWI miaka zaidi ya 30 sasa na asiwasaidie?

Anayeweza kujibu ajibu 😊
 
Kwan Maria alivyozaa Yesu,,yule mmewe Yusufu hakulala naeee
Hakuzaa wadogo zake Yesu!!?? Kwa hiyo bikra iliendelea tu kujirudiaa????
 
asante kwa hiyo wataka kuniambia maria alikuwa kama kasha tu la kupitishia/kubebea mzigo?
tuanze na maswali rahisi, kwa nini ilikuwa yeye na si mwingine?
na huko kutokuwa na mahusiano ya ki-DNA na maria nani alikuambia ni kweli? nifahamuvyo mie kwa sayansi yangu duni (mind you nimegraduate kwa degree ya Engineering Biotechnology) ili mtoto awepo/afanyike kunahitajika sperm and egg, sasa yesu hakukuwa na sperm from a man, je leo pia wataka kutupa ufunuo mpya kuwa hakukuwa na egg from a mother?
je ndugu yangu wataka kuchanganya concept ya roho na mwili?
maana wengi pia hawaelewi concept hii ya roho na mwili katika biblia. unakaribishwa kwa ufafanuzi zaidi wa chochote.

Maria alipata mimba kwa huwezo wa Roho mtakatifu ( Njia za Mungu hazichunguziki). Nimejarib kutumia neno Uhusiano wa ni ki-DNA ili huweze nielewa kuwa Maria ni mwanadamu na position yake itabaki kuwa hiyo. Alitumiwa kama walivyo tumika binadamu wengine,
mitume walitumika katika positions zao.
 
Swali lako ndugu linatofauti yoyote na kusema kama Mungu anapenda watu na anauwezo kwanini anaacha watu wanakufa sana Palestina na sehemu zingine za dunia? Au mbona wanasayansi wanahangaika kupata dawa ya UKIMWI miaka zaidi ya 30 sasa na asiwasaidie?

Anayeweza kujibu ajibu 😊

Zaidi ya hapo, kwa nini mungu mwenye uwezo wote na ujuzi wote aumbe ulimwengu ambao mabaya yanawezekanika?

Ukichunguza sana utaona hizi habari za mungu kuwepo zina ujinga kibao.
 
Nashukuru kunijulisha kuwa ni Eliya pekee aliyepalizwa. Ila ni kweli pia kuwa Musa na Enok wako hai mbinguni.

Naamini katika ufufuo. Lakini Biblia imeweka wazi kuwa ufufuo una majira yake yatakuja. Sio mtu afe leo then immediately afufuliwe aendelee kuishi peponi. Wafu hawako hai (wamekufa) mpaka hapo Yesu atakapowafufua siku ya mwisho.

Mfano wa Yesu na yule mwizi msalabani, maana yake ni kuwa alimsamehe na amempa pas ya kuurithi ufalme wake (siku ya mwisho na watakatifu wengine waliolala katika Yesu Kristo) sio kuwa yeye ametangulia!! Ndio sababu walikufa wote lakini aliyefufuka ni Yesu peke yake, yule mwizi alibaki mfu mpaka leo anasubiri ufufuo ila yeye ana advantage kuwa ataingia mbinguni maana Mungu alishamwambia pale msalabani.

kaka huo ni uelewa wako binafsi na sio uelewa wa wasoma biblia na uhalisia wa tukio. ok nikuambie tu na ujue vile hujui maandiko vizuri, wakati yesu alipokuwa akieleza kuhusu ile habari ya tajiri la lazaro masikini, alisema nini? naye tajiri yule alipokuwa katika mateso makali aliinua macho yake na tazama alimuona Lazaro akiwa ameketi na Ibrahimu wakifurahi, akapaza sauti kuu akamwambia Baba Ibrahimu, nakuomba umwambie lazaro achovye kidole chake katika maji naye aje anipoze koo langu maana ninateswa sana....habari ikaendelea zaidi ya hapo soma bible au nikupe mstari ukitaka (unajua habari hii au huijui?)sasa kama wewe wakazana kuwa hata Ibrahim ni mfu, na walio hai ni hao tu unaowataja hapa ina maana yesu alikuwa anadanganya?
habari ya huyo mwizi....: kwa hiyo wataka kutuambia yesu alimsamehe kwa kumwambia leo utakuwa pamoja nami paradisoni?
ndo wapi huko paradisoni? na why aseme amini amini nakuambia leo hii (na wala asiseme siku ya mwisho ntakufufua) au wewe unafahamu sana kuliko yesu hata kumtafsiria anayoyasema? au wewe wajua kuliko Yesu ndugu yangu?
 
Zaidi ya hapo, kwa nini mungu mwenye uwezo wote na ujuzi wote aumbe ulimwengu ambao mabaya yanawezekanika?

Ukichunguza sana utaona hizi habari za mungu kuwepo zina ujinga kibao.

Hapana hazina ujinga. Mimi naamini Mungu yupo na nimeshamuona!

Na ukichunguza kwa akili za kibinadam utachemka au kudata kabisa. Cha kwanza kabisa amini bila shaka yeyote kuwa Yesu ni Bwana! Yesu ni Mungu na ndiye aliyeufanya ulimwengu (sio dunia tu), ulimwengu (the 9 planets) ukawepo.

Biblia ninayoiamini mimi imeandikwa "mpumbavu amesema moyoni mwake hakuna Mungu". Hivyo ilijua kutakuwa na wapumbavu aina yako (kama unasema hakuna Mungu).

Lakini kila mtu na imani yake ndugu.
 
Mpumnavu kati yangu na wewe ni nani?

Mimi ninayekuuliza maswali ambayo huna majibu yake au wewe unayeamini kitu ambacho huwezi kukielezea?

Wewe una akili gani zaidi ya za kibinadamu mpaka umuelewe mungu ambaye haeleweki kwa akili za kibinadamu?

Kila.mtu na imani yake?

Mimi sitaki imani, nataka ujuzi.
 
Samahani. Haina haja ya kupaniki. Hatushindani. Tunajadili tu. Sio kuwa nimeshindwa kutoa majibu ila hata nikisema hivi au vile, majibu yangu yata-base kwenye Biblia inayosema Mungu ni Roho nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

Pia, si mimi nisemaye mtu asiyeamini uwepo wa Mungu ni mpumbavu, again ni Biblia hiyo hiyo ninayoiamini mimi 100% inasema asemaye hakuna Mungu ni mpumbavu.

Sasa kwa vile wewe huamini uwepo wa Mungu (upumbavu kwa mujibu wa Biblia ninayoiamini), basi si rahisi tukaelewana. Hutayaamini majibu yangu maana huamini Uwepo wa Mungu, hivyo sijashindwa kujibu maswali yako.
 
Maria alipata mimba kwa huwezo wa Roho mtakatifu ( Njia za Mungu hazichunguziki). Nimejarib kutumia neno Uhusiano wa ni ki-DNA ili huweze nielewa kuwa Maria ni mwanadamu na position yake itabaki kuwa hiyo. Alitumiwa kama walivyo tumika binadamu wengine,
mitume walitumika katika positions zao.

wewe ndio wasema hapa ili kuhalalisha unachokiamini peke yako, but i stand to be corrected, mie nazungumza kwa uhalisia, kama alitumiwa kama walivotumika binadamu wengine, je waweza kuniambia ni wapi katika biblia mtu (mwanamke) ameambiwa Umebarikiwa wewe kuliko wanawake wote?je baraka ya mungu wewe mwanadamu waweza ifuta?
hakuna alikuambia kuwa maria sio binadamu, yupo?if yes ni nan?
wanachokuambia hapa watu ni kuwa Maria is Blessed, ni mama wa Yesu, na watu kuomba kwa kusema Maria utuombee, sio kuwa wanakosea...au wewe hukusoma kuwa Mungu anasikiliza maombi ya watakatifu? na utakatifu wa maria malaika alikufunulia kwa kusema wazi wazi kuwa amebarikiwa yeye kuliko wanawake wote... naamini umenielewa...but wakaribishwa kama una maswali zaidi.
 
Back
Top Bottom