Nakuja kwenye hili. Sina uhakika kama hili linafanyika pia kwa Waprotestant pia, au kama ni baadhi au wote, ila kwa kuwa mimi ni RC, nitajibu kwa faith ya Kanisa Katoliki. RC huwa wanatumia reference za aina tatu katika mafundisho ya imani ya Kanisa, ambayo ni Maandiko Matakatifu (Biblia), Mapokeo Matakatifu, na Ualimu wa Kanisa. Katika Mapokeo Matakatifu, tunafundishwa kwamba watakatifu wa Mungu wapo mbinguni, na kwa msingi huo, Mama Maria yupo mbinguni.
Utaweza kuuliza, kwa nini mnaenda zaidi (sio kinyume) ya yaliyoandikwa katika Biblia? Jibu lake lipo humo humo katika Biblia! Ni kwamba si kila kitu alichotenda na kuagiza Kristu kimeandikwa na kalamu, yaani kwa njia ya maandishi. Yohana 21:25 "Kuna mambo mengine mengi aliyofanya Yesu, ambayo kama yangeandikwa yote, moja baada ya lingine, nadhani hata ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa."
Kwa mantiki hiyo, mapadre wa RC wanakuwa wamesoma mambo mengi sana ndio maana hata upeo wao wa mambo huwa ni mkubwa ukilinganisha na wachungaji wengi (sio wote), kwani wanakuwa wamelazimika kusoma vya kutosha kuhusu Maandiko Matakatifu (Biblia), Mapokeo Matakatifu, na Ualimu wa Kanisa.