Lupweko
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 24,940
- 26,796
Kwa namna fulani nimekujibu swali lako. Nina maana hii, si lazima kila umuombacho Mungu utapewa hapo hapo au kwa namna unayotaka wewe. Unaweza ukapewa kwa namna nyingine au wakati mwingine au vyote viwili. Wewe unasema Mama Maria awaponye WaLiberia kwa ugonjwa wa Ebola, umefanya juhudi gani? Wewe binafsi umemuomba Mungu kwa hilo? Umeomba Maria msaada wa maombezi yake? Naye anakuombea, hatoi unachokiomba.Hujajibu swali.
Au unaongea tu ili umjaribu kama ibilisi alivyomjaribu Yesu hapo kwenye mnara? Au unataka ishara tu? Angalia hii:
[SUP]11[/SUP]Mafarisayo walikuja, wakaanza kujadiliana na Yesu. Kwa kumjaribu, wakamtaka afanye ishara kutoka mbinguni. [SUP]12[/SUP]Yesu akahuzunika rohoni, akasema, "Mbona kizazi hiki kinataka ishara? Kweli nawaambieni, kizazi hiki hakitapewa ishara yoyote." [SUP]13[/SUP]Basi, akawaacha, akapanda tena mashua, akaanza safari kwenda ngambo ya pili ya ziwa.