Iltokea siku moja msanii wa nyimbo za Asili akazuia mvua isinyeshe sehemu walipo washabiki tu!

Iltokea siku moja msanii wa nyimbo za Asili akazuia mvua isinyeshe sehemu walipo washabiki tu!

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
11,252
Reaction score
24,088
Hii siyo ya kusimuliwa na watu niliona kwa macho yangu.

Katika mkoa wa Geita wilaya ya Nyang'hwale kata ya kafita na kijiji cha Lushimba.

Msanii wa nyimbo za Asili Bhudagala alikuwa akitoa show katika kijiji hicho.

Basi wingu zito lilitanda likiashiria mvua kubwa sana itashuka muda sio mrefu.watazamaji hofu ikawaingia wengine wakaanza kukimbia ili kuikwepa mvua hiyo!

Msanii huyo jina tajwa hapo juu akawaambia watazamaji rudini rudini huko mnakoenda ndo mvua itawanyeshea lakini hapa halitaanguka hata tone moja la mvua.

Maana nina mahema mengi sana ya kuikinga isiwanyeshee. Baada ya kusema maneno hayo akasema maneno fln kwa kilugha then akamwambia Dj achia mziki uendelee.

Dk si nyingi mvua kubwa ilinyesha sana pembeni lakini katu haikugusa eneo la kiwanja alipokuwa akifanyia show yake.

Mvua ilikuwa kubwa kiasi kwamba huwezi muona mtu akiwa umbali wa mita 7 hivi.

Maji yali tiririka mengi sana na majaruba kujaa maji lakini hakuna mtu aliyedondekewa au kunyeshewa na tone moja la mvua ile.

Baada ya mvua kuisha hakuna mtu aliyeamini wengi waliokuwa mbali na show ile walikuja uwanjani kushuhudia ambapo walikuta msanii pamoja na wachezaji wake wakitimua vumbi tu huku wakikata mauno.

Tukio hilo lilinikuta katika kijiji hicho Tajwa hapo juu.

Na ilikuwa mwaka 2018-19 hivi.Kwa wasio amini unaweza kwenda kijiji Tajwa hapo juu mkapate ushuhuda zaidi.

Nina imani kabisa kama Dini hizi zisingezagaa kila chocho kuna mambo makubwa mno tungekuwa tunayaona yakifanyika bila kificho.

Mfano hukohuko Nyang'hwale kuna kijiji kinaitwa Bukungu mara kadhaa fisi walikuwa wanauliwa na kukutwa wana simu au rozali wamevaa nk

Huko simiyu ndo kama hivyo tena iko wazi kwa matukio ya ajabu ajabu.
 
Nikifa mke wangu asiolewe unaishi nyangh'wale .

Kiufupi wasukuma na ushirikina ni pete na kidole .Mwaka jana hapa kharumwa uwanja wa sabasaba alipiga shoo kisima majabala aise ilitinga bonge la mvua lakini haikunyesha.


Ukienda huko itirima simiyu huko ndipo kuna zizi la waganga yani hapq nyumba hapa mganga.
 
Mzee bukungu napajua mwaka 2020 waliua fisi anashanga halafu na hii ya lushimba nimeisikia .
We jamaa unaishi hapa kharumwa
N mwenyeji wa huko mkuu. Bukugu kuna fisi alikutwa na simu mwingine shanga,rozali na wengine wengi wana hirizi na namba.

Bumanda -kangele walikuta ana mkoba wenye matunguli
 
Nikifa mke wangu asiolewe unaishi nyangh'wale .

Kiufupi wasukuma na ushirikina ni pete na kidole .Mwaka jana hapa kharumwa uwanja wa sabasaba alipiga shoo kisima majabala aise ilitinga bonge la mvua lakini haikunyesha.


Ukienda huko itirima simiyu huko ndipo kuna zizi la waganga yani hapq nyumba hapa mganga.
Mimi ni Mzaliwa mganza chato mkuu hivyo maeneo hayo niliyotaja huwa naenda kila mara japo kwa sasa siishi mganza wala msalala nipo geita
 
Back
Top Bottom