Ilikuwaje ukaenda kwa 'mtaalamu'?

Ilikuwaje ukaenda kwa 'mtaalamu'?

maji ya gundu

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
3,120
Reaction score
4,850
Habari zenu wana MMU naimani mko poa mnaendelea vizuri na majukumu ya kila siku.

Kwenye maisha kuna mambo mengi yanatokea unaeza ukawa umezaliwa kwene mazingira mazuri, umekuzwa kidini pasi na kujihusisha na ulozi lakini kadri unavyoendelea kuishi watu wanaku-shape kutokana na tabia zao, husda na chuki, unajikuta umeingia huko.

Kitambo sikuwahi kuwaza mambo kama haya kwa upande chanya lakini kadri ninavyokua na ninayokutana nayo, taratibu naanza kuwaelewa watu kwanini wanaenda kwa wataalamu.

Wapo wanaoenda kutafuta, wapo wanaoenda kujilinda lakini pia wapo wanaoenda kuangalia tu ramani za miili yao zimekaaje maana kuna watu hawahitaji sababu ya kukufanyia ubaya.

Wewe ilikuwaje ukaenda kwa mtaalamu? Na ulivyokuwa mwanzo na baada ya kwenda huko mambo yana tofauti gani? Kama una uwezo kwa kushare contact za wataalamu, pia tusaidiane.

Itoshe kusema, hawa wataalamu wamekuwa na msaada mkubwa sana kwa watu tofauti tofauti lakini wachache sana wanakiri na kuthamini uwepo wao.
 
Asante kumbe kuna uwezekano wa kujifunza pia!, naomba kujuzwa inawezekana kujikinga bila kuchanjwa
Epuka kabisa kuchanjwa, hiyo ni mihuri ya kiroho.. Kuna vitu na mimea ya asili ukivitumia huhitaji chale hata moja
Mfano ukifanikiwa kupata mafuta ya simba , ukaogea chumvi kisha ukajipaka kwa siku 7 mfululizo bila kujitia najisi yoyote umeula
 
Asilimia chache sana ya waafrika ambao hawajachanjwa. Watu wanachale tangu utotoni unakuja kuziona ukubwani. Unauliza unaambiwa ni dawa ulikua unaumwa. Kumbe mihuri moto
 
Asante nmekumbuka kipindi nakua familia yetu iliandamwa sana na ulozi ikabidi mzee ashughulikie hili swala, akaitwa mtaalamu akaja akafanya yake akachanja wote ila mi nilikimbia kiukweli hua sipendwi kuchanjwa toka mdogo, na majanga yananiandama mimi sana tofauti na wenzangu
 
Asilimia chache sana ya waafrika ambao hawajachanjwa. Watu wanachale tangu utotoni unakuja kuziona ukubwani. Unauliza unaambiwa ni dawa ulikua unaumwa. Kumbe mihuri moto

Tafsiri ya chale kiroho inategemea sana imani, utamaduni, na mazingira ambamo chale hizo zimefanywa. Katika mtazamo wa kiroho, chale huonekana kama alama ya agano, wakfu, au mawasiliano kati ya ulimwengu wa mwili na ulimwengu wa roho.

tafsiri kuu za kiroho:1. Alama ya Agano na WakfuKiroho, chale huchukuliwa kama "muhuri." Unapochajwa chale, unakuwa umewekwa wakfu (dedicated) kwa roho fulani, iwe ni roho za mababu, majini, au nguvu nyingine za giza. Damu inayotoka wakati wa kuchanjwa hutumika kama kiungo cha kuunganisha mtu na ulimwengu wa roho.
 
Back
Top Bottom