Ilikuwa ni lazima Masogange afe?

Ilikuwa ni lazima Masogange afe?

Kuna kitu kinaendelea lakini bado hakijawa wazi sana... Ngoja mshtuko wa habari za kifo utulie... Kuna mengi yatajitokeza......
Wiki iliyopita kuna binti aliuawa gesti Chalinze... ALINYONGWA.... Lakini muda mchache kabla ya mauaji kufanyika alipigiwa simu na ndugu yake wakati wauaji wakiwa tayari chumbani kwake... Akiwasiliana kilugha na huyo ndugu yake alimwambia kuna wanawake wanne wamemvamia chumbani lakini watatu anawafahamu
Baada ya hapo simu zake hazikupatikana tena! Maiti yake iligundulika siku ya pili... Katika kufuatilia undani wake ikaonekana alikuwa kwenye mtandao wa biashara ya madawa ya kulevya... Na kulikuwa na tatizo kati yake na hao wauaji wake... Hii ilitokana na mawasiliano yaliyofumwa kwenye simu yake
Mchana wa siku aliyouliwa kulikuwa na majibizano kwa njia ya maandishi
Yeye aliandika kuwa kwakuwa wao wamemwaga mboga basi yeye atatoboa sufuria kabisa... Naye akajibiwa kuwa.. Hatasubiri afanye hivyo... Watamfuata huko huko juu.....

Baada ya mazishi kaka yake mmoja akapigiwa simu kupewa pole na kuambiwa kila kilichotokea pale msibani mpaka kuzika... (Kwahiyo wauaji walikuwepo msibani) kisha akaambiwa kuwa MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI
Baada ya kama siku tatu za mauti yake binti mwingine akakutwa kauliwa kwa kuchomwa visu mwili mzima (alikuja Kutambuliwa kama mmojawapo aliyeshiriki mauaji ya kwanza), na mwingine naye akaponea chupuchupu akiwa keshakula visu vya kutosha na sasa hajulikani alipo
Scenario nzima inaonesha ni mauaji ya visasi kati ya makundi mawili na kuna kitu kikubwa kinafichwa!!!!
Ni vigumu kwasasa kulink kifo cha Agnes na hayo mauaji mengine lakini tayari kuna watu wameshaanza kutuhumiwa. ..
Agnes Masogange amekuja kuwa maarufu zaidi baada ya kuja kuhusishwa na biashara ya madawa ya kulevya... Tuhuma dhidi ya madawa ya kulevya zilipelekea akamatwe na kufunguliwa kesi... Ni juzi tu hapa mwezi uliopita alikutwa na hatia na kuhukumiwa kulipa faini au kifungo... Alinusurika kifungo kwa kulipa faini iliyolalamikiwa na wengi
Mabush lawyer wengi walisema kuwa kesi kama ile kama huna watu wazito nyuma yako unaondoka na maji...

Kwanini kifo chake kimeacha mashaka!?
Mitandao ya hizi biashara haramu., haipatani kabisa na kitu kinaitwa polisi... Kwa baadhi ya nchi watuhumiwa hufuatwa na kuuliwa huko huko jela au mahabusu
Masogange akiwa tayari kwenye spotlight ya polisi... Nini ingekuwa future yake!? Kumbuka ni vigumu tena kumtumia kwenye hiyo biashara.. Tayari ana file.. Hivyo keshakuwa ndege mweupe!
Lakini je anafahamu mangapi!? Je hawezi kuropoka?!?
Je ni nani aliyekuwa tayari kugharamia maisha yake ya anasa wakati sasa hawezi tena kuzalisha!?
Risk ni zipi akiachwa hai?
Risk ni zipi akinyamazishwa!!?
Je baada ya kesi kwisha alikuwa na madai kwa washirika wake kibiashara!?
Kifo hupangwa na Mungu kwa wale waamini.. Lakini nyuma yake kuna sababu za kifo... Naamini siku moja ukweli utajulikana
RIP [emoji1019] Agnes!
Umenena vyema mkuu.
 
Naamini sio majibizano mabaya kwakuwa kanuni yangu ni moja huwa sijibizani na wapuuzi kwakuwa wapuuzi hawajibiwi, wapuuzi huachwa na upuuzi wao... Hakuna dharau mbaya kama mtu kuku ignore totally
 
Muacheni binti wa watu apumzike bwana, Mengi na mengine anayajua Mwenyezi Mungu..
Inawezekana yapo mengi tunayoyajua kuhusu huyu Binti lakini ni busara kukaa kimya, maana tulitakiwa tuyaseme akiwa hai labda tungemsaidia lakini amechakufa hatuwezi tena kumsaidia mwenye uwezo sasa aliyebaki ni Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma.. Muacheni binti apumzike.. Mods fungeni huu mjadala..
 
Let the bygones be bygones! She's gone and we'll surely follow.
 
Haya basi,Kufa ni lazima.
Its the most certain thing a human being can be sure of.Alafu alilazwa siku nyingi.Amefariki kwa Typhoid.Just a natural death.Sidhani kama alikuwa na madhara tena kwenye biashara ile.Alidrop akaanza kujisogeza karibu na ibada.She was targeted alipokamatwa south.So hakuwa mtu sahihi tena kumpa kazi.
Typhoid! Are you expert in post-mortem?
Is there any press on this?
Do you have any clue to what is done in drug business?
How do you bet on the sale-out possibility of the verdict reached in court! Do you really believe that Agnes's case deserved a 1.5 million fine?

Work up, pal!
 
Muacheni binti wa watu apumzike bwana, Mengi na mengine anayajua Mwenyezi Mungu..
Inawezekana yapo mengi tunayoyajua kuhusu huyu Binti lakini ni busara kukaa kimya, maana tulitakiwa tuyaseme akiwa hai labda tungemsaidia lakini amechakufa hatuwezi tena kumsaidia mwenye uwezo sasa aliyebaki ni Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma.. Muacheni binti apumzike.. Mods fungeni huu mjadala..
Naamini hujasoma hii mada vizuri na kama umeisoma hujaelewa nilichoandika... Huyo binti ni segment ya mwisho kwenye mada yote.... Lakini pia nini maana ya kuitwa GT... That means you can think beyond! But how! Wengi mmeshindiwa hapa
 
Hahahahahahaha hii comment yako imenitoe kwenye reli ya kati sasa nakwenda kwenye SDG...
Hahaha kuna wengine wanasema kifo kimepangwa na Makonda ili kuzima maandamano
Niliposikia haya nikawacheki ,nika waangalia nikasema hiiiiiiiiiiiiiiiiii
SDG ndio sawa na 1.5tr?
 
Unaweza kuuwawa then ukatengenezewa fake report ya kilicho kuuwa..

Mleta thread ameleta uzi wa kuumiza vichwa kwa watu wasio penda kuumiza vichwa...
 
Masogange kuhusu madawa hajaanza jana wala leo.. aliwahi kukaa sello sana tu...

Halafu Aggy wowowo ndio limemtambulisha sio scandal za madawa... labda kama watu wameanza kumwona mwaka juzi

Tumwache dada wa watu apumzike kwa amani... Mungu amlaze mahala pema peponi Emen!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom