Ile ndege ya ATCL iliyopeleka nyama ya mbuzi Oman haiwezi kupeleka minofu ya Sangara Ulaya?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,875
Jana waziri wa fedha Mh Mpango amesema serikali imeingia mkataba na mashirika ya ndege ya nje mfano Rwandair na Ethiopian Airline kuweza kusafirisha minofu ya samaki kutokea Mwanza na mbogamboga kutoka KIA kuelekea Ulaya.

Swali dogo: Ile ndege ya ATCL iliyosafirisha nyama ya mbuzi haiwezi kufanya jukumu hili?

Maendeleo hayana vyama!
 
Mkuu
Ndege Zetu Zimetengenezwa Canada Zikaja Tanzania Zinaruka, Kwenda Ulaya Kupeleka Minofu Inaweza Kuwa Jambo Rahisi, Najiuliza Viongozi Wetu Hawalioni Hili Jambo
 
We kidogo huwa mnaonana n Polepole wkt wa mgao wa buku Saba hebu hujaribu kumdadisi atakupa jibu
 
Sangara wananuka sana hivyo tumeona ni bora kunukisha mandege ya watu ili sisi tubebe watalii. Ivi kweli ndege ibebe Samaki tena Sangara!?
 
Ina maanisha walio isababishia hasara ATC enzi hizo , waendele kuchukuliwa hatua , na kama kuna mambo mengine ya kisheria, basi masuala hayo yatatuliwe
 
Ayo Mashirika yana vibali kwenye izo njia kwa muda mrefu na hayachukui minofu ya samaki kutoka Tanzania pekeyake, kuna mizigo mingine mingi wanayo peleka pamoja na abilia.

ATC bado hawajapewa iyo njia, ata wakipewa leo inabidi watangaze ili watu/kampuni zinazotaka kupeleka mizigo huko ziombe nafasi. Ndege sio babaji kwamba dereva ana amka na kwenda njia yoyote kutafuta abiria. Njia za ulaya zina ushindani mkubwa inabidi kujipanga sio kukurupuka.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lazima uangalie na cost kama hiyo nyama na minofu ya samaki +mbogamboga peke yake zitarudisha ghalama za uendeshaji, vinginevyo inabidi washirikiane na hao ambao tayari wana soko la mizigo, na tayari walikuwa na route za huko tayari.
 
Vibari vya kwenda huko ndiyo shida, na hivi zinamendewa na wanaotudai
 
Ndege za ATCL ni za kusafirisha nyama ya mbuzi tu hata watalii wanakuja nchini kwa ndege za nchi jirani kudumisha ujirani mwema.
 
  1. Hizo ndege za abiria zinazo beba cargo, huwa zinakodiwa na cargo transporters
  2. Ndege ya ATCL pia iliwahi kukodiwa kupeleka mbuzi Dubai
  3. Ndege za wenzetu, wamevifugua viti ili kupata nafasi kubwa zaidi na kubeba mzigo mkubwa.
  4. Sisi tulibebesha mzigo kwa kuweka vi parcels kwenye viti.
  5. Gharama ya kurusha mdege mkubwa wenye mzigo mdogo ni kubwa kuliko gharama ya kurusha ndege ndogo yenye mzigo mkubwa.
  6. Hivyo hao transporters wana opt kukodisha Rwandan Air na Ethiopian Air kuja nchini kwetu kubeba mizigo yetu huku ile midege yetu imejidodea pale Airport huku sisi tukiangalia na kushangilia
  7. Sio kuwa Tanzania hatuna uwezo huo, bali hata bila ya janga la Corona, ATCL was operating on loss kwasababu bado hatuna watu wenye uwezo na akili ya ku run a successful airline business profitably
  8. Huu mtindo wa kukimbilia kununua midege kwa cash kwa mtindo wa kupiga tanchi bila kwanza kuwa na business plan, haya ndio matokeo.
  9. Hata hivyo, tusiilaumu sana ATCL, janga hili la Corona lime destabilize airline industry duniani kote mashirika kibao yamepunguza wafanyakazi kwa kushindwa kuwalipa while doing nothing, lakini sisi hatujapunguza mtu.
  10. Na kwenye usafirishaji wa mizigo, pia ATCL inajitahidi jitahidi tunapeleka cargo Comoro twice a week kwa bombardier.
P
 
Serikali haina shamba la maua Wala kiwanda Cha kusindika minofu. Waliokodi hizo ndege ni wawekezaji wenyewe.
Ni vigumu kufanya kazi na ATCL maana ghafla unaweza kukuta wameitelekeza bidhaa yako Kisha ndege imeenda Dodoma kubeba makada wa CCM
Ni kweli,serikali za ki Afrika hazieleweki.

Kila kitu ni amri kutoka juu,sijui kama ni mbinguni ama wapi
 
Back
Top Bottom