Ile kiu ya kusubiria Toleo la Phantom X2 sasa imeisha

TECNO Tanzania

Senior Member
Jul 6, 2016
192
216
Kampuni ya simu ya TECNO katika kuendeleza kutoa bidhaa zilizo bora na zinazoendana na technologia ya kisasa, tunakuletea lile toleo la kubwa Zaidi kwenye mtiririko wa PHANTOM ambalo watumiaji wengi wa simu janja wamekuwa wakiulizia sasa limefika sokoni na linapatikana kwenye maduka yetu nchi nzima.

PHANTOM X2 ndo ile Flagship ya maana ambayo kila mteja ambaye ameshawai kuitumia simu hii huwa anatamani kuendelea kutumia mtirirko wa matoleo haya ya PHATOM tu kwani zimekuwa simu zenye ubora zaidi zikiwa na kasi kubwa ya utendaji na ubora wa hali ya juu.

Simu hii imekuja na sifa kuu ambazo zimeboreshwa zaidi katika mtiririko wa PHANTOM. Na sasa tunasema ni ‘Zaidi ya kawaida’ (Beyond ExtraOrdinary).
20221208-090521.jpg


DISPLAY- 6.8’’-inch ultra-wide cinema like screen Ratio
Toleo hili la Phantom X2 limekuja na kioo kipana zaidi kikiwa na 6.8’’ inch na ni kioo kilicho jipinda kikimpa mtumiaji uhuru na burudani isiyo na kifani pale ambapo atakuwa anatazama mahudhui mbali mbali kwenye simu hiyo kama vile kutazama video, kucheza michezo mbalimbali (Video games) au kuingia kwenye mitandao ya kijamii, simu hii ina onyesho la Wide Color Gamut na kasi ya 120Hz, ikiboresha simu kwa uwazi, mwangaza na usahihi wa rangi kwa matumizi mazuri ya kutazamwa. Lakini pia kioo kilicho undwa kwenye toleo hili ina aminika kuwa na Glass ngumu sana ata pale simu itakapo dondoka sio rahisi kuvunjika(CORNING GORILLA GLASS VICTUS).

20230113_141114.jpg


CAMERA- 64MP Ultra Clear Night Portrait
PHANTOM X2 imekuja na kamera yenye 64MP yenye lensi ya RGBW iliyotengenezwa kwa ufanisi mkubwa sana ilikuipa picha yako ubora wa juu zaidi. Kamera yake imewekwa viwango vipya ili kuiwezesha kunasa kwa usahihi picha angavu katika mazingira tofauti tofauti hasa wakati wa mwanga hafifu. Lakini pia kwenye upande wa kamera ya mbele toleo hili limekuja na 32MP ambapo mtumiaji anaweza kupiga picha na kutengeneza video nzuri, safi na zenye ubora.

WhatsApp Image 2023-01-10 at 08.49.41.jpeg


DESIGN- Unibody Doublecurved Design
Muundo wa Unibody uliopinda mara mbili katika pande zote mbili za simu hii ni kipande cha sanaa kinachosawazisha nadharia za siku zijazo na kukupa hisia kali kiganjani hasa pale unapo ishikilia simu yako. Jipatie umaridadi mkubwa usio na kifani pale unapo gusa na kushika simu yako. Pia pembe za PHANTOM X2 zimenakshiwa kwa mipako inayofanana na almasi kwa asilimia 71% ilikuipa mvuto simu yako. Ukiachana na muundo huu wa upinde PHANTOM X2 imekuwa ya Kwanza duniani kuwa na kioo chenye Madoa cha 3.5D cha Lunar (3.5D Lunar Crater Dazzling Stained Glass)

20230113_141121.jpg


STORAGE- LPDDR5 PC Level Large Memory

Uhifadhi mkubwa wa kumbukumbu kwenye simu hii ina ipa uwezo wa kuendesha programu na faili nyingi kwa wakati mmoja. Pia uboreshaji wa uhifadhi ili kuongeza nafasi ya hifadhi, huacha simu ikiwa na kumbukumbu ya kutosha kila wakati. Toleo hili limekuja na uwezo wa uhifandi kumbukumbu ikiwa na RAM ya LPDDR5 yenye kasi ya juu 8GB + 5GB RAM unayoweza kuiongeza mwenyewe. Lakini pia kwenye upande wa ROM inatumia UFS 3.1 ROM ambayo ni nzuri sana ikiwa na 256GB.

20230113_141055.jpg


PROCESSOR- MediaTek Dimensity 9000
Chip ilyo tumika kwenye ya simu hii imekuwa mahiri na ya kwanza yenye kasi ya TSMC N4 (ya kiwango cha 4nm). Processor ya MediaTek Dimensity 9000 inaongoza kwenye kusaidia utendaji mzuri wa simu hasa ikiwa inakasi ya 5G.

20230113_141103.jpg


NETWORK- 5G All- scene Network Optimization
Tukiwa tunaendelea kukimbizana na kasi ya technologia tumeleta toleo la PHANTOM X2 ikiwa imekuzwa na teknolojia ya 5G inayoongoza katika ufanisi pale unapofanya matumizi ya kimtandao. Toleo hili linakupa uhuru wa kufanya kazi mtandaoni wakati wowote na mahali popote. Hii husaidia kufanya mawasiliano daima yawe na kasi kubwa. Kwenye upande wa mtandao simu hii ina IDA Injini ya 3.0 ambayo inatoa uboreshaji hasa sehemu zenye mtandao dhaifu na matumizi kidogo ya nishati pale unapokuwa mtandaoni.

20230113_140930.jpg


BATTERY- 5160mAh Extra Large Battery
Betri yake ikiwa ime ongezewa uwezo na sasa imekuja na 5160mAh ambayo ni Kubwa Ziada. Hii Inaipa simu yako ufanisi mkubwa hasa kwenye utunzaji wa nishati na kumuwezesha mtumiaji kutumia simu hii kwa muda mrefu bila kupata changamoto za kuchaji simu mara kwa mara. Lakini katika upande wa kuichaji tole hili lina 45W super chaji ikimaanisha kwa unaweza kuchaji simu yako kwa muda mfupi zaidi ambapo ndani ya dakika 20 unaweza kuchaji hadi 54% na ndani ya dakika 60 unaweza kuchaji hadi 100%.

Bei na Upatikanaji wa Toleo la PHANTOM X2
Toleo hili linapatikana katika maduka yetu nchi nzima. Bei elekezi ya PHANTOM X2 ni 1,300,000/=
Kwa mawasiliano Zaidi unaweza Kutupata kwenye namba zifuatazo; 0744 545 254 au 0678 035 208.
 
Tuheshimu ujuzi wa watu..
Chief-Mkwawa pita huku
Sio simu mbaya mkuu, ni flagship yenye processor ya mwaka Jana, ila Tecno wana overprice sana simu zao, michina mingi yenye cpu za mwaka jana unaipata around $300 to $400 na kuanzia $500 unapata flagship za mwaka huu, simu kama Redmi K60 series.na Oneplus 11.
 
Sio simu mbaya mkuu, ni flagship yenye processor ya mwaka Jana, ila Tecno wana overprice sana simu zao, michina mingi yenye cpu za mwaka jana unaipata around $300 to $400 na kuanzia $500 unapata flagship za mwaka huu, simu kama Redmi K60 series.na Oneplus 11.
Imeisha hiyo..

Mleta mada jibu umepata, tuendelee na ujenzi wa taifa.
 
Sio simu mbaya mkuu, ni flagship yenye processor ya mwaka Jana, ila Tecno wana overprice sana simu zao, michina mingi yenye cpu za mwaka jana unaipata around $300 to $400 na kuanzia $500 unapata flagship za mwaka huu, simu kama Redmi K60 series.na Oneplus 11.
Oneplus 11 nitapata wapi hii simu original brand? Msaada
 
Nakumbuka 2017 nilinunua Phantom 6 Plus ,camera ilikufa baada ya muda mfupi sana yaani 700k yangu iliniuma sana.
Ulirogwa???🤣🤣🤣 tecno ni simu ya kupewa bure utunze line sio utoe pesa yako ukanunue
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom