Ile chenji ya Rada imeishia wapi?

Ile chenji ya Rada imeishia wapi?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,353
Reaction score
26,194
Eti,'chenji'(Alubaki) yetu ya Rada ya Chenge imesharudi? Eti,imeshanunuliwa madawati na vitabu Shule za Msingi? Naulizia tu viongozi...
 
Ndio maana nimekukaribisha JF, haya mambo yalishazungumziwa hapa sana!!
Tumia muda wako wa kutosha kutafuta thread za rada uone kilichojadiliwa!!
Hiyo ilishapita.Kwasasa hali ikoje? Si vibaya nikapewa update Mkuu
 
Chenji ya rada ndiyo itakayogharamia kampeni za CCM 2015, ukichanganya na hela ya pembe za ndovu inayoratibiwa na lile gaidi la kisomali tutaona mengi.
 
Pamoja na matukio mengi ambayo tumekuwa tukijadili, kuna hili la chenji ya rada naona bado hatujafahamishwa limeishia wapi.

Tuliambiwa kuwa Uingereza walishaturudishia hizo pesa na tukaahidiwa kuwa fedha hizo zitanunulia madawati ili watoto wetu wasiendelee kukaa chini.

Je kuna mwenye habari kwamba hayo madawati yalishanunuliwa kwa hiyo fedha? Nani alipewa jukumu la kuratibu matumizi ya hizo fedha?

Naomba, hasa kwa ndugu Wabunge, hilo swali liulizwe bungeni ili wananchi waweze kujua fedha hizo zimetumika vipi.
 
Ahahahaaaa wewe haujapata chako?kwishney,dili zinapotokea usilale chukua chako mapema kaka
 
Ahahahaaaa wewe haujapata chako?kwishney,dili zinapotokea usilale chukua chako mapema kaka

Ulishapata? Mimi sijapata ndio maana nauliza. Hivi kila mtu alipaswa apate chake au zile fedha zilikuwa za kununulia madawati ya watoto?
 
Back
Top Bottom