Club Mate
Member
- Aug 1, 2025
- 25
- 86
Wadau, habari zenu.
Simaanishi kwamba biashara ya kuuza chenji ipigwe marufuku au wauzaji washughulikiwe. Hapana. Lakini ukweli ni kwamba, uwepo wa watu wanaofanya biashara ya kuuza noti ndogo na sarafu mtaani ni kiashiria tosha cha uhaba wa chenji kwenye mzunguko. Ni wazi kuwa wafanyabiashara wadogo, makonda wa daladala, bodaboda na madereva wa bajaji wamekosa sehemu rasmi za kupata chenji.
Ukichanganya hili na ile tabia ya wafanyabiashara wetu kutegemea mteja ndiye atafute chenji (aje na hela kamili), huu udhaifu wa BoT kwenye mzunguko wa pesa unageuka kuwa kero kubwa sana ya kila siku.
Zaidi ya hapo, ukosefu wa chenji unasababisha upandaji wa bei usio na mantiki pale gharama za maisha zinapopanda. Kwa mfano, inawezekana kupanda kwa bei ya mafuta kumeongeza gharama ya ruti ya bodaboda kwa Tsh. 200 tu, lakini kwa kisingizio cha "hakuna chenji," bei inapandishwa kabisa kwa Tsh. 500. Hata chapati mtaani kutoka Tsh. 500 inaruka hadi 1,000 kwa visingizio hivi hivi.
Hata kwenye ma-supermarket wanatumia mwanya huu huu. Badala ya kukupa chenji yako, wanaona ni bora wakupe pipi.
Mabenki na mawakala nao wanachangia sana hii shida. Mara nyingi ukienda ATM unatoa noti za 10,000 tu. Hivyo, pesa nyingi zinazozungushwa mtaani na wafanyakazi zinakuwa ngumu sana kuzitumia kwenye manunuzi ya bidhaa au huduma ndogo ndogo.
BoT inabidi ishughulikie hii ishu haraka sana. Imekuwa kero kubwa, na kusema ukweli ni aibu kwa Benki Kuu kuona hela yao inauzwa kwa faida mtaani bila wao kuchukua hatua yoyote ya msingi kuhakikisha chenji inapatikana kote.
Nawasilisha.