Serikali ya CHADEMA itafanya nini?
- Itawekeza katika uvunaji wa maji ya mito, maziwa, chemchem na mvua.
- Mamlaka ya Usambazaji ya maji itakuwa chini ya halmashauri za manispaa, miji na wilaya
- Itawezesha vijiji kutunza vyanzo vya maji ili visiharibiwe.
- Upatikanaji wa Maji kwa Wananchi itakuwa ni kipaumbele muhimu cha serikali ya CHADEMA.
- Itaingiza kwenye mitaala kuanzia shule ya msingi hadi sekondari dhana ya utumiaji na utunzaji wa maji.
- Tutaboresha na kukarabati miundombinu ya maji iliyopo ili kuzuia upoteaji wa maji.
- Tutahakikisha kila Mtanzania anapata maji safi na salama katika kipindi kifupi iwezekanavyo.
- Hatutabinafsisha sekta ya Maji na makampuni yote yaliyobinafsishwa yatarejeshwa chini ya mamlaka za Maji katika Halmashauri za Wilaya. CHADEMA haitaweka MAJI chini ya mikono ya Makampuni ya kigeni, ni hatari kwa usalama wa Nchi.