Ilaaniwe siku niliyozaliwa

ILAANIWE SIKU NILIYOZALIWA - 25

Tulipoishia -
" mmmmh ni balaaa,alimteka mtoto wake wa kike,kisha akawapa vijana wake wambake kwa zamu,kama iyo haitoshi aliiteketeza familia yake yote kwa moto" aliongea saidi.

Endelea nayo.

Maneno ya saidi yalikuwa ni kama kisu moyoni kwa Helena.Aliishiwa nguvu akajikuta amekaa chini.Taratibu sura yake ikaanza kubadilika,mwili wake wote ulianza kutetemeka kwa hasira.

" aaah !madama H mbona ivyo?" aliuliza said kwa uwoga.

Helena hakumjibi kitu,alimpiga pigo moja shingoni pale pale saidi akapoteza fahamu.Alichukua silaha yake na kuingia kwenye kile chumba walichokuwa wanafanya mkutano.

Kama kichaa alianza kuwamimina risasi mfululizo.Kila aliyekuwa anamlenga alikuwa hamkosi.Kelele za risasi ziliwafanya walinzi waliokuwa nje waingie ndani haraka na wao waanze kushambulia.

Walishambuliana mle ndani kwa muda mrefu sana.Mafunzo aliyoyapata kwa al sha baab yalimsaidia sana helena.Alifanikiwa kuwapiga risasi walinzi wengi sana.

Mzee komba baada ya kuona hali ni mbaya,alipita mlango wa siri akatokea nje.Lakini ile anafika nje tu,alikutana na shabaan akiwa na askri wengine uso kwa uso. Walimkamata na kumweka chini ya ulinzi,wale askari waliingia ndani na kuanza kushambulia,waliwashambulia na kuwakamata vijana wengi.

Helena alipowaona askari alijificha na kuangalia kinachoendelea.Alimwona mzee komba akiwa kakamatwa,pia aliwaona wale vijana waliombaka wakiwa wamekamatwa na kupakizwa kwenye gari.

Gari ziliwasha na askari wakaondoka na wale watu.Helena moyo wake bado ulikuwa unamuuma sana.Hakuridhika wale watu kukamatwa,alitaka wafe wakiwa mikononi mwake.Akaamua kuzifata gari kwa nyuma .Alizafata hadi zilikoishia,Mzee komba na wenzake hawakupelekwa polisi,walipelekwa kwenye nyumba ya siri ya usalama wa taifa kwa ajili ya kuhojiwa.

Helena aliiangalia nyumba waliyoingizwa kisha akarudi kujipanga vizuri.Majira ya saa saba usiku alienda kwenye ile nyuma na kuvamia akiwa na visu vingi bila bunduki.

Kwakutumia mbinu za kijeshi alifanikiwa kuingia ndani.Alizunguka mle ndani kumtafuta mzee komba na wale vijana waliombaka.Kutokana na giza na ukimya uliotawala mle ndani aliangaika sana,lakini mwishowe alifanikiwa kuwaona joel na wale vijana waliombaka.Kwakutumia funguo bandia alifungua selo yao na kuingia ndani.

Joel akiwa amelala alihisi maumivu makali ya tumbo,alishtuka na kujishika tumboni,alishangaa kukuta amechomwa kisu cha tumbo.Alimwangalia aliyemchoma alikuwa helena,alitaka kupiga kelele helena alimziba mdomo na kumkata koromeo .Alinyosha mkono ili amshike helena ,Lakini kabla hajamshika akakata roho.

Purukushani alizozifanya joel ziliwafanya vijana waliokuwa mle waamke na kuanza kupiga kelele baada ya kuona damu.Kwa kasi ya ajabu ,huku akiwa kama amechanganyikiwa helena alianza kuwachinja mmoja baada ya mwingine.Kila aliyejaribu kupambana naye aliambulia patupu.
ndani ya dakika kumi chumba kizima kikawa kimejaa damu na maiti.Helena mwili wake wote ulikuwa umelowa damu.

Aliitafuta maiti ya joel akaipata,bila huruma akaanza kuichoma visu mfululizo,alijua kwakufanya hivyo hasira zake zitapungua lakini kila alipomchoma ndipo kumbukumbu za nyuma zilipomjia na kuzidi kumchoma zaidi.

Kelele alizokuwa anazipiga wakati anamchoma visu ziliwafanya askari waliokuwa wanalinda nje waje ndani haraka.

Sauti za viatu vya watu wakija ndani zilimfanya helena asimame pale alipo na kwenda kujificha kwenye nyuma ya mlango.Askari waliingia mle ndani wote,baaa ya kuingia wote helena alitoka na kuwafungia mlango kwa nje.

Baada ya kuwafungia ile anatoka tu aliwekea bastola kichwani.Aliivyogeuza macho yake kumuangalia aliyemuwekea bastola,alikutana uso kwa uso na martini,ambae alikuwa ni rafiki wa baba yake.

Martini alishangaa kumuona mtu aliyemshikia bastola ni mwanamke.Akawauliza wenzake.

"Kuna mwingine huko?" ,ila kabla hajajibiwa,helena kwa spidi ya ajabu alipiga mkono wa martini bastola ikaruka juu.ile martini anashtuka akakuta helena ameshaikamata bastola na kumwekea yeye kichwani.

" nionyeshe aliko mzee komba" aliongea helena.

Martini akawa anajiuma uma ,kitenda cha kujiuma uma kilimkera helena akamkandamiza zaidi ile bastola kichwani.Martini hakuwa na jinsi akaongoza njia mpaka walikomfungia mzee komba.

Kufika alipofungiwa mzee komba ,helena alimsachi martini akamkuta na pingu,akamfunga nayo kwenye chuma kilichokuwa pembeni kisha akamsogelea mzee komba.

" kosa langu ni nini? Familia yangu imekukosea nini?" aliuliza helena huku akitokwa na machozi

Swali lile lilimfanya mzee komba amuangalie vizuri helena.Alijaribu kuvuta kumbukumbu akakumbuka unyama aliomtendea.

" nakuuliza wewe? Kosa langu ni nini?, baba yangu na mama yangu wamekukosea nini?"

Mzee komba alimwangalia helena kwa huzuni sana.Nafsi yake ilianza kujuta yale ya nyuma.

" najua ata nikikuomba msamaha haina maaana yeyote,hautaweza kunisamehe.Sina la kukuambia helena,ninachoweza kusema ni kuwa sikutakiwa kuzaliwa,"

" yaaani pamoja na yote hutaki kuomba ata msamaha" alifoka helena.

Martini aliyekuwa pembeni amefungwa pingu baada ya maelezo ayo akamtambua helena.Kwa mshangao mkubwa akamuuliza.

" aaah! Wewe ni helena. Mtoto wa naoel. Nisamehe na mimi nilishindwa kumtafuta aliyemuua baba yako.Huyu mzee nilimuamini lakini huku mwisho nimekuja kugundua ata mimi amenifanyia ubaya mkubwa." aliongea martini

Helena kila alipomuangalia mzee komba hasira ilizidi kumpanda,aliokota kipande cha nondo kilichokuwa pale chini na kumpiga nacho kichwani.Martini akawa anamsihi asimuue amuache sheria ifate mkondo wake.

" naomba usimuue helena,muache sheria ifate mkondo wake,usiichafue mikono yako na damu yake" aliongea martini lakini helena hakumwelewa.Alimshika mzee komba na kuanza kumpiga mfululizo usoni na kile kipande cha chuma.

" niambie ,tulikukosea nini? Sema tulikukosea nini " aliongea helena.

" nisamehe helena,nisamehe martini kwa yote niliyokufanyia, nimetenda uovu mwingi sana.Naomba mnisamehe,nisameheni" aliongea mzee komba huku akivuja damu.

Maneno ya mzee komba hayakupunguza hasira ya helena,alichukua kisu na kumchoma nacho tumboni mfululizo.Martini alipiga kelele kumzuia helena asifanye vile lakini halikuwa amechelewa,helena alimchoma visu mfululizo tumboni mzee komba.

" kwanini unajiaribia maisha helena.Nani alikuambia kuua ndio dawa" alifoka martini.

Helena alitupa kisu chini na kukaa chini.

" kuzaliwa kwangu kumeleta matatizo duniani,ILAANIWE SIKU NILIYOZALIWA " aliongea mzee komba kwa shida na pale pale akakata roho.

Haukupita muda askari wengi wakafika eneo lile.Kati ya waliofika shabaan alikuwepo.Shabaan aliingia kile chumba alichokuwa helena ,na martini .kufika mle alikuta maiti ya mzee komba ipo chini.

Martini alimuomba shabaan amsaidie helena kutoka mle ndani kwa siri bila kukamatwa,na pia akamuifadhi nyumbani kwake.

Kama alivyoelekezwa na martini alimtoa helena kwa siri bila kujulikana,na moja kwa moja akampeleka nyumbani kwake.

.........

Siku zilienda helena akaenda kwa ndugu zake.Wakampokea,wakafanya taratibu mafao yote ya wazazi wake akapewa yeye.Akaanzisha biashara,maisha yakaenda kwa amani kabisa.Akawa rafiki mkubwa sana wa shabaan.kutokana na uwezo wake wa kijeshi ,Martini na shabaan wakamfanyia mpango akaingia jeshini,akawa askari.

Mwisho.....Maoni muhimu.

................

Sent using Jamii Forums mobile app
Story nzuri sn. Shukrani sn mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom