Ilaaniwe siku niliyozaliwa

ILAANIWE SIKU NILIYOZALIWA - 17

Endelea nayo.

Martini alitetemeka kwa uwoga na kupiga kelele. " mwacheni mwananguuu nitawaua wote wanaharamu nyie" aliongea kwa sauti martini.

Sauti upande wa pili ikiwa imebadilishwa kwa programu maalum ilimjibu. " kama utatuua basi hakuna namna, itabidi tumbake mwanao hili hata kama utatua tuwe tumemfaidi mwanao"

" Hapana msifanye ivyo,niambieni mnataka nini mimi nitawapa.Semeni chochote ,Naomba mwacheni mwanangu tafadhali" aliongea martini na kulia kama mtoto mdogo.

" ok sawa,Acha kutufatilia .Achana na habari ya kifo cha rafiki yako baba helena,na achana kabisa na habari yako ya kunifatilia.Hili ni onyo la mwisho.Usipoelewa tutamfanyia mwanao unyama usiowahi kuhusikia"

" sawa ,sawa ,sawaaaa,sawa" martini alijibu huku akilia kuwa ataachana na upelelezi wake.Pale pale simu ilikatwa.

Mzee komba alimwambia yule kijana avae nguo na asimbake Husna.Walimvesha nguo husna kisha wakamfunga kitambaa machoni na wakampakia kwenye gari na kwenda kumshusha nyumbani kwake,kisha wakatokomea.

Martini aliapa kutofatilia tena kesi ya mauaji ya rafiki yake.Alilia kama mtoto akiwa chumbani kwake.Akiwa amelala kitandani huku akilia alimsikia mke wake akipiga kelele .

" mwananguuu,mwanangu" aliongea mama husna na kumkimbilia mwanae na kumkumbatia.Martini alisimama na kutoka nje.HAkuamini macho yake.Mwanae alikuwa mzima wa afya.

Martini alijiapiza kutofatilia tena ile kesi.Alimkumbatia mwanae na kuingia nae ndani.

............

Majira ya saa moja usiku,Shabaan alikuwa amepanga kukutana na mzee komba.Mzee komba naye aliandaa vijana ili wamkamate na kumuua kabisa.

Mzee komba alifika sehemu waliyopanga kukutana .Muda ulienda lakini shabani hakuonekana.Walijaribu kumpigia simu lakini pia simu yake haikupatikana.

" mmm!h!,au atakuwa ameshatushtukia?" aliuliza mzee komba.

Waliendelea kukaa kwa muda mrefu bila shabaan kutokea.Walikata tamaa na kuamua kuondoka.

........

Siku zilienda miezi ilikatika bila shabaan kuonekana.Martini naye alikata tamaa kabisa,aliachana na kesi ya mauaji ya rafiki yake.Hakutaka hata kuisikia.

Alienda kwenye kaburi la baba helena na kumuomba radhi.

" nisamehe baba helena,nimeshindwa kumpata aliyesababisha kifo chako.Nisamehe sana.Nisamehe kwakuwa nimeamua kuacha kabisa kumtafuta.Nimefanya hivi kwa usalama wa mwanangu."aliongea martini huku machozi yakimtoka.

......

Kitendo cha shabaan kutoonekana kwa muda mrefu kilimpa wasiwasi mzee komba.Alipata wasiwasi kwasababu Shabaan alikuwa anajua mambo yake mengi.Alihisi labda siri zake nyingi zitakuwa wazi.ili kukabiliana na ilo akaamua kusimamisha shughuli zake kwa muda kwanza ili kupeleleza na kujua nini kinaendelea.

....

Kwa upande wa helena aliendelea kujifua pamoja na kundi la al sha baab.Alifanya mazoezi kwa nguvu zote.Kila alipokumbuka jinsi alivyotendewa alikuwa anaenda kufanya mazoezi kwa nguvu zote ili kupunguza mawazo.Alijiapiza kuja kuwachinja wale wote waliomtendea ubaya .Tangu siku ile aliyomuona joel hakumuona tena.Joel alikuwa kwenye kambi nyingine tofauti na yeye.

Ujasiri wake uliwafanya viongozi wa al sha baab wampende.Walikuwa wanamuita dada shujaa.uwezo wake ulikuwa ni mkubwa sana.Alikuwa anauwezo wa kupambana na wanaume zaidi ya ishirini peke yake.Licha ya kupendwa kwa ujasiri wake lakini aliogopwa sana na wenzake kutokana na userious aliokuwa nao.Muda wote alikuwa amenuna ,alikuwa hacheki,alikuwa kauzu kweli kweli.

Aliwachukia sana wanaume.Aliwachukia zaidi hasa alivyowaona pale kambini jinsi walivyokuwa wanawakamata wasichana wadogo kijijini na kwenda kuwabaka.Aliapa kuja kuwaua wanaume wote.Aliwachukia sana,aliamini wao ndio chanzo cha uovu uliokuwepo duniani.

...
Miaka miwili ikakatika mzee komba akaamua kuanza tena biashara yake.Aliamua kubalisha wafanyakazi wake wote,na hii ilisababishwa sana na tukio la shaaban,alihisi pengine wapo wengine ambao walikuwa wanatumiwa na serikali.

Aliwatumia hela al sha baab wamletee vijana watatu wa kazi na mlinzi mmoja.Ahmed kiongozi wa al shaabab ,alimuandalia vijana watatu pamoja na helena ambae alitakiwa aende akawe mlinzi wa mzee komba.Kutokana na ujasiri wake waliona helena ndi mtu pekee mqenye sifa za kumlinda mzee komba.Walimwambia helena ambae sasa walikuwa wanamuita Shujaa H.Helena aliwakubalia bila kinyongo kwani alikuwa na hamu kubwa ya kurudi tanzania kulipa kisasi.

Al sha baab waliwasiliana na mzee komba na kumpa sifa za helena ambao wao walikuwa wanamwita shujaa H. Mzee komba alitamani kumuona kutokana na jinsi walivyomsifia.

" huyu madam H kwa sifa zake itabidi awe mke kabisa.Atakuwa mlinzi wangu lakini pia nataka awe mke wangu." aliwaza mzee komba.

Inaendelea hapa chini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ILAANIWE SIKU NILIYOZALIWA - 18.

Tulipoishia - " huyu madam H kwa sifa zake itabidi awe mke kabisa.Atakuwa mlinzi wangu lakini pia nataka awe mke wangu." aliwaza mzee komba.

Endelea nayo.

Mzee komba alituma hela zote alizoambiwa atume.Mipango ya safari ikafanyika.Helena na wenzake watatu wakaanza safari ya kuja Tanzania kupitia kenya.

" naenda Tanzania nyumbani.Naenda kulipa kisasi kwa wale wote walionifanyia unyama na kuharibu maisha yangu.Nikiwamaliza wa kule nitarudi tena somalia kumtafuta joel,na yeye ni lazima nimpate " aliwaza Helena .

Pamoja na moyo wake kujaa kisasi ,helena pia alikuwa na hamu kubwa ya kuwaona wazazi wake.Hakujua kama baba na mama yake walishakufa muda mrefu.

" Wazazi wangu watakuwa walinitafuta sana.Bila shaka watakuwa walikata tamaa." aliwaza helena.

Walifanikiwa kuvuka mpaka na kuingia nchini kenya.Baada ya kuingia kenya walitembea kwa umbali mrefu sana .Wakafika kwenye kijiji kinachoitwa mpecho.Pale iliwabidi walale na siku ya pili waendelee na safari.

Kwakuwa mipango ilikuwa imeshafanywa,Waliingia kwenye nyumba moja ya raia wa kenya ambae anaasili ya kisomalia aitwae mohammed.Mohammed aliwapa vyumba wakalala kwa kificho na hawakuruhusiwa kutoka nje.Mohammed alikuwa ni mgambo wa al shabaab.

" mmesafiri wakati mbaya sana.Askari wa kenya wapo kwenye msako mkubwa sana kutokana na mashambulizi ya waste gate" aliwaambia.

" kwahiyo tunafanyaje? Kurudi tena somalia saizi haiwezekani.Kivyovyote vile ni lazima tufike Tanzania" alijibu seif ,ambae ni mmoja wa wale vijana ambao helena alikuwa anakuja nao Tanzania.

.........

Shabaan baada ya kufanya kazi kwa mzee komba na kujua siri zake nyingi,Aliwasilisha taarifa kwenye kitengo cha kupambana na ugaidi nchini Tanzania.Lakini wakati anarudi nyumbani kwake pwani,machale yalimcheza .Aliwasaliana na wasiri wake wakamwambia asirudi Pwani.Hivyo alibadilisha safari na kurudi dar.

Kufika dar kitengo cha kupambana na ugaidi kikaamua kumpeleka kenya ili akashirikiane na majeshi ya kenya katika kupambana na ugaidi,kwakuwa yeye alikuwa anajua mipango yao na njia zao zote wanazopita pamoja na mawakala wao.

Wakati helena na wenzake wakiwa kwa mohammed wakiongea mlango uligongwa.Mohammed akawapa ishara wakina helena haraka sana wakajificha mle ndani.

Mohammed alienda kufungua mlango.

" aaah shabaan!,karibu sana ndugu" mohammed alimkaribisha shabaan.

" asante vipi za hapa?"

" safi,sijui za wewe.Muda mwingi sana hatujawasiliana" alijibu mohammed.

" majukumu tu yamekuwa mengi.Vipi hakuna vijana wowote ambao wanasafirishwa" aliuliza shabaan kwa mtego.Shabaan alikuwa anajua kila kitu.Mtu alyekuwa anafanya kazi ya kuwavusha alishamwambia kuna watu wanne amewavusha.Ambao mmoja ni mwanamke na wengine watatu wanaume.

Yule mtu wa mpakani alimwambia shabaan akijua kuwa bado wapo naye.Hakujua kama shabaan ni shushushu.

Mohammed baada ya kuulizwa swali kama kuna watu wanasafirishwa alifikiria haraka kisha akaamua kukataa.Sababu ya kukataa ilitokana na ukweli kuwa yeye na shabaan hawakuonana muda mrefu,hivyo hakuona kama ni busara kumwambia taarifa nzito kama hiyo.

"Aisee hakuna vijana wowote wanaosafirishwa" alijibu mohammed.

" ok sawa " alijibu shabaan huku akiangaza macho kushoto na kulia.Katika kuangaza angaza macho.Alikiona kivuli cha mtu aliyekuwa amejificha nyuma ya mlango.Taratibu akawa anapeleka mkono kiunoni ili achukue bastola.

Lakini kabla hajaifikia bastola mohammed alimuwahi na kumuwekea bastola kichwani.

" sikuelewi elewi shabaan" aliongea mohammed

" aah ! Hunielewi kivipi?,kwanini umeniwekea bastola kichwani?"

" kwanini ulikuwa unataka kuchukua bastola kiunoni.Umetumwa na serikali kutuchunguza au ?" aliuliza mohammed.Shabaan hakumjibu kitu,kwa kasi ya ajabu alimpiga mtama mohammed akaanguka chini kama mzoga kisha akarukia chumba cha pili kama mshale.

Wakati anaruka kuelekea chumbani mohammed alimfyatulia risasi ,na risasi moja ikampiga mguuni.Chumba alichoingia Shabaan alikuwepo helena.ile ameingia tu,alipigwa teke la tumbo paaah.Alipotua chini alijikuta amewekewa bastola mdomoni.

Shabaan akawa mpole.Mohammed na wale vijana walipoingia walimkuta helena tayari kashamzibiti shabaan.Helena wala shabaan hakuna aliyemjua mwenzake.

Mohammed alimvuta shabaan mpaka barazani.

" Huyu mshenzi ni mwanaharamu sana.Ametusaliti.Ametumwa na askari wa kenya kuja kutuchunguza.Hapaswi kuachwa hai.Aliongea mohammed huku akimuwekea bastola kichwani Shabaaan.

" kama ametumwa kutuchunguza hakuna haja ya kutumia risasi.Tutamaliza risasi zetu bila sababu." aliongea helena kisha akachukua kisu na kuanza kumkata koromea shabaan.

Inaendelea hapa chini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
,ILAANIWE SIKU NILIYOZALIWA - 19

Tulipoishia - kama ametumwa kutuchunguza hakuna haja ya kutumia risasi.Tutamaliza risasi zetu bila sababu." aliongea helena kisha akachukua kisu na kuanza kumkata koromea shabaan.

Endelea nayo

Helena alikuwa amebadilika.Alikuwa katili sana.Wakati anaweka kisu vizuri ili amchinje vizuri.Mlango ulipigwa teke .Askari wa kenya wakaingia na kuanza kushambulia.Kwa kasi ya ajabu kama mshale helena aliruka juu na kwenda kujificha kwenye kona .

Ndani ya dakika mbili,wenzake wote watatu pamoja na mohammed walikuwa wamepigwa risasi na kuanguka chini.Alikuwa amebaki peke yake.Alichukua bastola yake ,kisha akairudisha tena kiunoni.Akachomoa visu vitatu.Kimoja akakiweka mdomoni na vingine viwili akavishika mkononi.

Alisikiliza milio ya viatu akajua idadi yao.Walikuwa askari watatu na shabaan alikuwa wa nne.Kwa kasi ya ajabu kama upepo alitoka pale kwenye kona na kuanza kuwarushia visu.Kila aliyemlenga alimpata,askari wote watatu wakaanguka chini kama mizigo.

Alimfata shabaan na kumuwekea kisu shingoni tena.Lakini kabla hajafanya lolote milio ya risasi ilisikika.Haraka sana kwa kasi ya ajabu akakimbilia chumba cha pili kisha akabomoa dirisha na kukimbia.

" amekimbilia huku,huku" shabaan aliwaambia askari walioingia mle ndani.

Waliingia chumba alichoingia wakakuta dirisha limevunjwa.Walitoka nje haraka kuangalia lakini hakuwepo mtu.Helena alikuwa ameshakimbia eneo lile.

Walimchukua shabaan na kuondoka naye.

" hawa jamaa kuna mashambulizi lazima watakuwa wamepanga.Binti aliyewakimbia pale anaonekana ni hatari sana.Al sha baab kumtuma mtu hatari kama yule lazima kutakuwa na shambulizi walilolipanga" aliongea shabaan

" na kama mngechelewa kidogo yule mwanamke angekuwa ameshanichinja.Naomba hali ya hatari itangazwe eneo hili la mpakani,na askari wote wawe tayari kwa mashambulizi muda wote" aliongea shabaan.

..............

Helena alikimbia kwa umbali mrefu.Mwishowe aliingia kwenye gofu moja lililokuwa alijaezekwa.Akavua nguo ambayo alikuwa amejifunika a!bayo ilikuwa inamuonesha macho tu.Akabaki na suruali na t shirt .Alichimba shimo dogo mle kwenye gofu akafukia silaha yake pamoja na zile nguo zake.

Akatoka kwenye lile gofu na kuanza kutembea taratibu.Hakufika mbali akasimamishwa na kijana mmoja aliyekuwa kwenye pikipiki.

" dada mambo?" alisalimia yule kijana.

Helena alimwangalia hakumjibu akaendelea na safari yake.Yule kijana hakukata tamaa akawa anamfata kwa nyuma.

" dada salaam uwa haitii mimba" aliongea yule kijana huku akimshika mkono helena.

" unasemaje?" aliuliza helena.

" mmmmh! Kiswahili chako kizuri sana.Wewe ni mtanzania?"

Helena alimwangalia hakumjibu kitu

" dada mbona inaonekana unadharau sana?,yaaani nakuongelesha hata kukujibu hutaki"

" sikiliza dada,ujue maisha hayako ivyo ,hivi kama ukinisikiliza na kunijibu wewe utapungukiwa na nini?

Helena hakumjibu akaendela kutembea.Lakini apoangalia mbele aliwaona askari wa kenya wapo kwenye msako.Haraka sana akamsogelea yule kijana na kujibebiisha.

" ulikuwa unasemaje?" helena alimwambia yule kijana kimahaba baada ya kumsogelea.

" aaah ! Aaah!,aaaaa" yule kijana alishikwa na kigugumizi gafla.Akutegemea kama angefanyiwa vile.

" unajua shida yangu nikiongea hapa unaweza nifikiria tofauti ukazani labda mimi muhuni,kiukweli mimi sio muhuni.Kama hautojali naomba panda piki piki tukaongee nyumbani" yule kijana alimwambia helena.Helena bila kusita alipanda wakaondoka.Walipo wafikia wale askari yule kijana alisimamisha pikipiki.

Moyo wa helena ukajaa hofu.

" dogo punguza bana" wale askari walimwambia yule kijana.

" aaah nipunguze nini? Yaaani akili yenu imeenda mbali sana.Mimi huyu ni dada yangu"

" dada zako kwani sisi hatuwajui.We unazani kuna mtu asiyewajua watoto wa mkuu wetu wa kazi" waliongea wale askari.Yule kijana aliwasha pikipiki na kuondoka

Maneno ya wale askari yalimshtua helena.Akaamua kumuuliza yule kijana.

" hivi baba yako anafanya kazi gani?"

" kwanini umeuliza?,Baba yangu ni askari na ndie mkuu wa vikosi vyote vya maeneo haya ya mpakani"

" mmmh! Kama ni ivyo usinipeleke kwenu mimi naogopa?"

" aah usiogope baby.Ninapokupeleka sio nyumbani kwa wazazi wangu ni nyumbani kwangu mimi." aliongea yule kijana kisha akavuta moto wa pikipiki kuelekea nyumbani kwake.

Haikuchukua muda wakawa wamefika.Alimkaribisha helena ndani.

" aya mrembo niambie sasa.Hujue muda ule nilisahau hata kukuuliza jina "

" Naitwa nasra" alidanganya helena.

" ok sawa mimi naitwa salim na hapa ni nyumbani kwangu jisikie huru kabisa"

Wakiwa wanaongea hazikupita dakika tatu mlango uligongwa.Salim alisimama na kwenda kuufungua.

" aaah wewe mwanamke umefata nini tena hapa?" alifoka salim.Sauti yake iliingia ndani na helena aliisikia.Haraka helena akasimama na kwenda dirishani kusikiliza.

" nimekuambia hii mimba sio yangu.Kwanini haunielewi ? Au kwakuwa baba yangu anahela ndo mana unataka kunisingizia" alifoka salim na kumsukuma yule binti.

Binti alikuwa mdogo sana.Helena alimuonea huruma sana.Alitoka pale dirishani na kwenda kukaa chini.Salim alimtimua yule binti na kurudi ndani.

" Naomba leo nilale hapa" helena alimwambia salim.

" kuhusu ilo tu usijali,hapa kwako.Lala utakavyo." aliongea salim.

Waliongea mawili matatu.Salim akamtongoza helena na helana akamkubali bila kinyongo.Alimkubalia kwakuwa alikuwa anataka hifahdi ya kukaa pale hadi msako wa askari wanaomtafuta utulie.Salim baada ya kukubaliwa alijua kinachofata ni ngono.Lakini kila alipotaka kumshika, helena alimkatalia na kumwambia asubiri hadi usiku.

Muda ulienda ,giza likaaingia.Majira ya saa tano usiku.Salim alianza kumpapasa helena aliyekuwa amejiegesha kitandani kutokana na uchovu.Helena kila aliposhikwa kumbukumbu za nyuma zilimjia.Alikumbuka siku aliyobakwa na wale vijana.Hasira ilimpanda ,akawa anatetemeka .Salim akili yake ilishakuwa mbali ,hakujali hali ya kutetemeka kwa helena.Alimshika kwa nguvu na kujiandaa ili ambake.

Inaendelea hapa chini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ILAANIWE SIKU NILIYOZALIWA - 20

Tulipoishia - Muda ulienda ,giza likaaingia.Majira ya saa tano usiku.Salim alianza kumpapasa helena aliyekuwa amejiegesha kitandani kutokana na uchovu.Helena kila aliposhikwa kumbukumbu za nyuma zilimjia.Alikumbuka siku aliyobakwa na wale vijana.Hasira ilimpanda ,akawa anatetemeka .Salim akili yake ilishakuwa mbali ,hakujali hali ya kutetemeka kwa helena.Alimshika kwa nguvu na kujiandaa ili ambake.

Endelea nayo.

Kitendo cha kumshika miguu kwa nguvu kilimfanya helena akumbuke tukio alilofanyiwa miaka ya nyuma. Alipomwangalia salim hakumuona salim bali aliona taswira ya Joel.Salim alikuwa ameshavua nguo na alikuwa akiangaika kumshika miguu ili amuingie .

Helena huku akitetemeka alimpiga salim konde moja hatari sana la uso.Pale pale salim alianguka chini na akawa anatapika damu.Kila alipojaribu kuinuka alishindwa.Pale pale akaanza kukohoa damu.Kitendo chake cha kukohoa damu kilimfanya helena azidi kuchukia,kwani alivyokohoa meno yake yalionekana.Kitendo cha meno kuonekana kilimfanya helena aone kama anamcheka.

" unanicheka joel,unacheka joel " aliongea helena huku akimsogelea salim aliyekuwa ameanguka chini.

Salim alishangaa kuitwa joel.Lakini kabla hajasema lolote alipigwa teke la mdomoni hali iliyoperekea meno yamtoke na damu izidi kutoka.Helena alikaa sawa na kumuangalia salim ambaye yeye alikuwa anamuona kama joel.

Salim alikuwa uchi wa mnyama.Helena alipoziona sehemu zake za siri alikasirika zaidi.

" unalingia huu upumbavu sio" aliongea helena kisha akazishika sehemu za siri za salim na kuanza kuzivuta.Alizivuta kwa nguvu lakini hazikutoka.

" ngoja" aliongea helena kisha akachukua chupa ya bia iliyokuwa mezani na kuipiga chini ikapasuka.Baada ya kuipasua alichukua kipande cha chupa na kuanza kuzikata sehemu za siri za salim.Salim alikuwa ameshapoteza fahamu.Helena alizikata na kuzitoa.Damu ilitapakaa .Machozi yakawa yanamtoka helena na akawa analia kwa uchungu.

Alikaa chini kwenye zile damu na kujiinamia.Alilia sana.Alipokuja kuinua macho alishtuka kumuona salim akiwa kapoteza maisha yupo chini.

" aaah! Nimefanya nini?,huyu sio Joel " alishangaa helena.Akili yake ilijua mtu anayemfanyia ukatili ule ni joel.

Kwa hofu kubwa alisimama na kutoka eneo lile.Alijiangalia mkononi alikuwa kalowa damu.Haraka sana akachukua maji yalikuwa kwenye ndoo akanawa.Akafungua mlango na kuchungulia nje hakukuwa na mtu yeyote,sana sana giza lilikuwa totoro.Akatoka taratibu na kuanza kukimbia.

Kichwani mwake alikuwa na ramani yote ya eneo lile.Wakati wapo mafunzoni walifundishwa ramani ya eneo lile kwakuwa walikuwa na mipango ya kuja kulishambulia.

.......

Masaa yalienda siku zikakatika ,helena kwakutumia njia za panya na mbinu alizofundishwa alifanikiwa kufika jijini nairobi.Akiwa nairobi bila ya nauli Alipanda basi la kuja dar es salaam.Kwenye siti ya basi aliyokaa, alikaa na kijana machachari aitwae john.

John alivutiwa na urembo wa helena na akaanzisha mazungumzo naye.

" dada habari " alisalimia john

" safi kaka mambo"

"Poa ,unajua sio vizuri tukasafiri pamoja hadi dar bila kujuana.Mimi naitwa john sijui mwenzangu unaitwa nani?"

" Naitwa nasra" alidanganya helena.

" ok nasra.Jina nzuri sana.Nimefurahi kukufahamu.Mimi ni mfanyabiashara nachukua bidhaa dar nazileta hapa nairobi.Sijui mwenzangu unafanya shughuli gani?"

"Mimi ni mwanafunzi wa chuo,nasoma chuo kikuu pale nairobi"

Wakiwa kwenye mazungumzo.Basi lilliwashwa na safari ya kwenda dar ilianza.Hawakufika mbali konda akawa anapita kukagua tiketi.Walipita siti moja hadi nyingine.Alipofika walipokaa helena na john.John alitoa tiketi na kukabidhi.Helena yeye akajifanya yuko bize kuitafuta,alifungua kimkoba chake kidogo na kuangalia.Alikuwa ni kama mtu aliyepoteza kitu flan.

"Aah jamani tiketi mbona nilikuwa hayo hapa." aliongea helena huku akijifanya kuitafuta.

Konda alipoona hapewi tiketi na muda unaenda akawa mkali.

" dada usinizingue,naomba tiketi haraka " alifoka konda.

" aaah! Kwani nimekuambia sikupi?,si unaona naitafuta hapa.Kulipa nimelipa halafu unaninyanyasa" alijibu helena huku akiendelea kuitafuta tiketi ambayo kiukweli haikuwepo.

Konda alipoona anapewa maneno bila tiketi akaamua kuwa mkali na kuanza kumtukana matusi helena.Kitendo kile kilimuuzi john.

" kijana kuwa na adabu basi?,kwani nauli yenyewe sh ngapi mpaka umtukane ivyo.Shika hela yako hii" alifoka john akatoa Tsh 75 elfu na kumkabizi konda.

Konda alichukua hela na kukata tiketi .

"Aaah kwanini umempa hela.Kwanini tulipe nauli mara mbili?" aliongea helena.

" usijali achana naye ,nimeona nimpe tu .Haiwezekani akakunyanyasa mtoto mzuri wakati mimi nipo "

Waliongea mengi sana,john kila alipomuangalia helena .Tamaa ya ngono ikawa inamwingia .Alimshawishi helena wakishuka waende anakofikia yeye john.Kwakuwa helena akuwa na pakufikia ilibidi akubali.

Walifika ubungo wakashuka ,kisha wakachukua tax na kuwapeleka kwenye hotel ya kifahari.

" hapa ndipo ninapofikiaga,karibu sana" john alimkaribisha helena.

Waliingia chumbani kisha wote wakajitupa kitandani kwa uchovu.Akili ya helena ilikuwa akiwaza jinsi ya kufika kwao pwani wakati akili ya john ilikuwa kwenye ngono.

" mmmh umechukua chumba kimoja tu?" helena alimuuliza john

" ndio kwani kuna ubaya?"

"Ubaya upo,mwanamke na mwanaume tutakaaje chumba kimoja? " aliuliza helena.

" kuhusu ilo ondoa shaka ,hapa tunalala tu.Mimi sikufanyi chochote bila ruhusa yako.Kuwa na amani kabisa.Unajua hii hotel ni gharama sana,ndio mana nimechukua chumba kimoja tu" aliongea john.

"Mmmmh! Sawa " alijibu helena kisha akasimama na kwenda bafuni kuoga.Ndani ya nusu saa akawa ametoka bafuni.

Kutokana na maji aliyooga nguo yake ilikuwa imenasa kwenye maji ivyo kupelekea maungo yake kuonekana.Umbile lake zuri alilojaliwa likawa linaonekana vizuri.

John uchu ukamshika akamsogelea na kumshika.Helena alisogea pembeni .Kitendo cha helena kujisogeza pembeni kilimkera john.

" aaah! Yaani wewe nimekulipia nauli,nimekununulia chakula njiani halafu unaleta jeuri yako hapa,hutaki nikushike umekuwa dada yangu" aliongea john kisha akamshika helena kwa nguvu na kumtupia kitandani.

" utake usitake lazima unipe.Mimi sio kaka yako" aliongea john

ITAENDELEA SEHEMU ZILIZOBAKI ZA SIMULIZI HII YA KUSISIMUA NISIWACHOSHE KWA KUWABANDIKIA SIMULIZI NDEFU SANA

salute mkuu inasisimua sana,ukija na muendelezo nitag

na ikiisha nidai hela ya bando😇😇😇😇😇
 
[11/11/2019 19:45] Mjamaa: ILAANIWE SIKU NILIYOZALIWA - 21.

Tulipoishia -
" aaah! Yaani wewe nimekulipia nauli hela nyingi,nimekununulia chakula njiani halafu unaleta jeuri yako hapo,hutaki nikushike umekuwa dada yangu" aliongea john kisha akamshika helena kwa nguvu na kumtupia kitandani.

Endelea nayo.

" utake usitake.Lazima unipe.Mimi sio kaka yako" aliongea john

Helena akiwa anashangaa kilichotokea. John alivua suruali na kupanda kitandani.Aliichana nguo aliyojifunika helena na kumziba mdomo asipige kelele.

" wewe mwanamke wa ajabu sana.Yaaani wema wote niliokufanyia halafu hutaki hata kuguswa.Shenzi sana wewe.Sasa leo nitakuonyesha" aliongea john.

" sitaki ,niachee sitaki" helena alijaribu kumsukuma john.John kadri alivyokuwa anamlazimisha ,ndivyo helena kumbukumbu za kubakwa zilivyokuwa zinamjia kichwani.

Kila kumbukumbu hizi mbaya zilipokuwa zinamjia alikuwa anatetemeka na kulia kwa woga.John hakujali kutetemeka kwa helena,alimshika miguu kwa nguvu na kutaka kumuingia.

Helena alipiga kelele lakini john alimuwahi na kumziba mdomo.Kitendo kile kilimfanya helena aione taswira ya joel.Baada ya kumuona john yeye akawa anamuona joel mbele yake.

" joel sitaki niache ,usinibake" aliongea helena kwa shida kwakuwa alikuwa kazibwa mdomo.

" aaah unanifananisha mimi na boya wako joel" aliongea john na kumshika mikono kwa nguvu helena.Helena alimuangalia john kwa jicho kali ,kisha akajigeuza kama umeme na kuruka kutoka pale kitandani.

John akiwa anashangaa mtu aliyemshika kitandani kaondokaje. Haraka sana na yeye akageuka nyuma kumuangalia helena,ile anageuka tu akapigwa na teke kali la mguu wa kushoto ,akaangukia kitandani.Helena alimfata pale pale kitandani akamkaba kooni na kuanza kumpiga usoni mfululizo.

Alimpiga ngumi nzito usoni mfululizo.John pale pale akapoteza fahamu.Helena akili yake ikawa kama amepagawa alienda mezani akachukua glass iliyokuwa mezani,akaipasua na kumchoma nayo usoni.Alimchoma nayo mfululizo usoni ,uso wote wa john ukawa hautamaniki.

Alimwacha kitandani,Akasogea pembeni akawa anapiga kelele kama kichaa.Aligeuka akamuangalia john aliyekuwa amelala kitandani.Akawa kama mtu aliyekumbuka kitu ,haraka sana akachukua kipande cha ile glass na kwenda kumkata john sehemu za siri .Alizikata na kuzitupa chini kisha akazikanyaga kanyaga,kwa hasira.

Aliendelea kupiga kelele mle ndani kama mwendawazimu.Kelele zake ziliwafanya wahudumu waje na kugonga mlango.Kitendo cha wahudumu kugonga mlango kilimrudisha kwenye akili yake ya kawaida.

"Aaah! Nimefanya nini?" alijiuliza .Alimwangalia john pale kitandani alikuwa ameshapoteza maisha.

Akili yake ilifanya kazi haraka ,akawasha tv .Kisha akasogea mlangoni bila kufungua mlango akawauliza wahudumu shida yao nini?

" mnataka nini?,mbona mnatusumbua ?" aliongea kwa mahaba pale mlangoni.

" punguzeni kelele basi?,mapenzi yenu yasiwe kero kwa wengine" aliongea muhudumu.

" sawa " alijibu helena.

Baada ya wahudumu kuondoka helena alihema kwa nguvu na kukaa chini pale mlangoni.Machozi ya uchungu yalikuwa yanamchiririzika mashavuni.

" nimefanya nini mimi?" alijiuliza moyoni.

" mmmmh! Hapana" alijisemeha moyoni kisha akasimama na kuelekea chooni.Alichukuwa ndoo la maji na kuja kulimwaga pale kitandani ambapo damu ilikuwa imetapakaa.

Alienda tena chooni akakinga ndoo la maji mengine na kuja kulimwaga tena pale kitandani.Alifanya ivyo kama mara sita.Chumba kizima kikawa kimejaa maji.

Alijiweka sawa na kunawa damu zilizomrukia usoni kisha akatoka nje kwa tahadhari kubwa.Alitembea haraka haraka mpaka nje ya ile hotel.Alipotoka nje kabisa ya eneo la hotel alihema kwa nguvu akageuka nyuma kuiangalia ile hotel kisha akatimua mbio.

..........

Alizurula pale mjini kwa muda wa siku tatu.Baadae kwakuunga unga akafanikiwa kusafiri mpaka pwani.Kufika pwani moja kwa moja akaelekea kwenye tarafa yao na mwisho akawa amefika mtaani kwao.

Alitembea kwa haraka hadi nyumbani kwao.Alishangaa kukuta nyumba yao imebaki kuwa gofu.Akiwa anashangaa alipita dada mmoja akamsimamisha na kumuuliza.

" Dada habari?"

" Safi za kwako"

" Nzuri!,nilikuwa naulizia hii nyumba imepatwa na majanga gani ? Na wenye nyumba saizi wanaishi wapi?"

"Mmmh! Wewe utakuwa mgeni hapa.Mwenye hii nyumba na familia yake wote waliungua moto kwenye ajali ambayo iliteketeza hii nyumba"

" mmmh! Unataka kusema wote wamekufa?" aliuliza helena kwa mshtuko.

" ndio.Baba ,mama na mtoto wao helena wote waliungua moto"

Helena miguu ilimwishia nguvu na pale pale alianguka chini kama mzigo akapoteza fahamu.Yule dada alishtuka na kurudi nyuma kwa woga.Watu waliokuwa karibu na pale walisogea na kumuuliza yule dada.

" Dada umemfanya nini mwenzako?" walimuuliza

" Hapana !,sijamfanya kitu.Mimi nashangaa tu kaanguka.Kaniuliza swali nimemjibu ndio akaanguka."

Walimtikisa pale chini na kumpa huduma ya kwanza.Haikuchukua muda fahamu zake zikarejea.Alisimama watu wakawa wanamuuliza maswali mengi lakini hakujibu kitu.Watu wa pale mtaani hawakumjua kama ni helena ,japo baadhi walisema atakuwa ni ndugu yake na helena kwakuwa amefanana nae.

" huyu atakuwa ni dada yake helena.Ona walivyofanana"aliongea mzee moyo.

Helena alisimama akaangalia kushoto na kulia kisha akaondoka eneo lile bila kujibu maswali ambayo walikuwa wanamuuliza.Akiwa anaondoka moyoni alikuwa akijisema " hapana baba hajafa,haiwezekani wakafa wote,haiwezekani" alijisemeha moyoni helena.

Alikuwa amechoka sana na hii ilitokana na kutokula muda mrefu,pia kusafiri muda mrefu bila kupumzika nako kulichangia mwili wake kuchoka sana.

" nimefika nyumbani lakini nyumba imeungua moto.Bado sina pakula wala kulala..Ngoja niende kwa baba mkubwa.Yeye ataniambia kama kweli baba na mama wamekufa au la na kama wamekufa ataniambia tatizo lilikuwa nini.itabidi kwanza nitafute ukweli kuhusu familia yangu ndipo nianze kumtafuta mtu waliyesema nije kumlinda.Kwasasa hakuna jinsi itabidi nikaishi kwa baba mkubwa "aliwaza helena moyoni.

Alitembea kuelekea nyumbani kwa baba yake mkubwa.Umbali ulikuwa mrefu na ilibidi apande gari lakini kwakuwa hakuwa na nauli alitembea kwa mguu mpaka akafika.

Kufika pale alimkuta baba yake mkubwa akiingia nyumbani kwake.Alimkimbilia ili amkumbatie.

" baba mkubwa,babaaa" aliongea helena huku akimkimbilia baba yake mkubwa aitwae Aron.

Aron alipogeuza macho alimwona helena akimkimbilia.Moyo wake ulilia paaah.Alishangaa kumuona pale .Akili yake ilifanya kazi kwa spidi ya ajabu akaona kitu cha kufanya ni kumfukuza na kumkataa kabisa.

" nikileta upumbavu milioni 159 za mirathi nitazikosa.Hapa dawa ni kumtimua huyu binti.Hakuna njia nyingine zaidi ya kumkataa tu" aliwaza moyoni Aron.

" kwangu mimi ameshakufa". Aliwaza aron ambaye ni baba yake mkubwa helena.

Ndimi
Mjamaa samwely kisinga
[12/11/2019 17:11] Mjamaa: ILAANIWE SIKU NILIYOZALIWA - 22

Tulipoishia - " nikileta upumbavu milioni 159 za mirathi nitazikosa.Hapa dawa ni kumtimua huyu binti.Hakuna njia nyingine zaidi ya kumkataa tu" aliwaza moyoni Aron.

" kwangu mimi ameshakufa". Aliwaza aron ambaye ni baba yake mkubwa helena.

Endelea nayo

Helena alimkimbilia na kumkumbatia baba yake mkubwa ambae ni Aron.Aron kwa hasira akamsukuma chini .Helena akaanguka kama mzigo.

" hivi wewe unakichaa?, unayemwita baba yako nani?" alifoka aron.

Helena akazani pengine baba yake amemsahau kwakukwa ni muda mrefu umepita tangu waonane.

" aaah baba mkubwa,umenisahau mimi mwanao.Mimi ni helena ,mtoto wa mdogo wako Noel" aliongea helena.

" Helena yupi? Helena mtoto wa mdogo wangu ameshakufa.Hebu ondoka hapa upesi kabla sijakuitia mwizi"

"Hapana baba mkubwa.Mimi sijafa.Ona ni mimi mwanao ," aliongea helena huku akimsogelea baba yake mkubwa na kumshika mikono.

Aron aliitoa mikono ya helena na kuisukuma pembeni.

" mbona unanichafua.Nani amekuambia unishike?,hebu ondoka hapa sasa hivi kabla sijapiga kelele za mwizi.Naomba ondoka haraka" alifoka aron.

Maneno ya baba yake mkubwa yakamfanya helena abaki mdomo wazi.Hakuamini macho yake.

" yaaani baba mkubwa leo ananikataa kabisa.Anasema nimekufa!,nimekufaje wakati nipo hai.Hivi nimebadilika sana au ?" alijiuliza helena maswali mfululizo bila majibu.

Kwa unyonge alisimama na kuondoka eneo lile.Kichwa chake kilivurugika.Hamu ya nyumbani ikamwishia.Alikuwa anatembea bila kujua anaenda wapi.

Mawazo makali aliyokuwa nayo yalimfanya asisikie njaaa.

" inamaana ni kweli baba na mama wamekufa? ,Hapana haiwezekani,hivi naota au?, Lazima nitakuwa naota,haiwezekani.Baba na mama hawawezi kufa .Hapana hawajafa.Mimi naota.Ngoja nifanye kitu ili nishtuke kwenye hii ndoto" aliwaza helena kisha akausogelea ukuta uliokuwa jirani akaupiga kichwa.

Aliamini labda akiupiga kichwa atashtuka toka kwenye usingizi.Alipiga mara ya kwanza hakushtuka.Akapiga mara ya pili pia hakushtuka,alijipiga ukutani mfululizo damu zikaanza kumvuja.

" mbona sishtuki kwenye hii ndoto? Au ni kweli wazazi wangu wamekufa kwa ajali ya moto?" aliwaza helena huku damu na machozi vikitiririka kwenye mashavu yake.

Kwa huzuni kubwa akakaa chini kwenye ule ukuta.Kutokana na uchovu na kutokulala siku nyingi, pia purukushani alizopitia mwili wake uliitaji kupumzika.Pale pale alipokaa usingizi ukaanza kumnyemelea akawa anasinzia,na mwishowe akapitiwa na usingizi.

" mmmh huyu nani amelala hapa? Hawa ndo wezi hawa" aliongea juma baada ya kumuona helena kalala kwenye ukuta wa nyumba yake.Aliingilia ndani akachukua ndoo ya maji akammwagia .

" mwaaaah " alimmwagia maji helena.Helena alishtuka na haraka akasimama.

" utalalaje kwenye upenu wa nyumba yangu? Toka haraka ,juzi tu nimeibiwa hapa.Sitaki kukuona aisee" alifoka juma.

Helena alimwangalia bila kumjibu kitu.Akili yake ilikuwa mbali,hakujua hatma ya maisha yake ni nini?

" naongea na wewe? Mbona unanitolea tu macho?,hebu ondoka hapa haraka sana?" alifoka juma.

Helena taratibu akawa anatembea kama mtu aliyelazimishwa.Alikuwa ameshakata tamaa ya maisha.Akiwa hajafika mbali kwa mbele aliwaona vijana wawili anaowajua wakimkimbilia.

" madam H, madam. H" waliita wale vijana huku wakimkimbilia helena.

Helena alipowaangalia vizuri aliwajua.Alikuwa said na zuber,vijana aliofanya nao mafunzo ya kijeshi nchini somalia.

" Madam H,kumbe ni mzima.Watu wanajua kuwa umekufa baada ya kushambuliwa." aliongea said

Helena akiwa na uchungu moyoni,aliwaangalia kisha akawaambia wampeleke wanakoishi akapimzike.

" kuhusu ilo usijali,kwani boss ambae tumekuja kumfanyia kazi alisikitika sana kusikia umekufa baada ya kushambuliwa nchini kenya.Nina uhakika atafurahi sana kukuona." aliongea zuber wakaenda hadi kwenye gari lao kisha safari ya kuelekea nyumbani kwa boss wao ambaye ni mzee komba ikaanza.

.......

Aron baba yake mkubwa helena roho ilikuwa inamuuma kwa kile alichokifanya.Moyo na akili yake vilimtambua kabisa helena ila alimkana kwasababu ya tamaa za mirathi.

" hivi nimekuaje mimi?, hii roho mbaya nimeitoa wapi? ,naanzaje kumkataa kabisa mtoto wa mdogo wangu kisa mali " aliwaza Aron.

" yule ni helena kabisa.Na nilijua kabisa kuwa atakuwa mzima maana ata ile maiti tuliyozika nilijua siyo yake ila nilijifanya sijui.daaah!, sijui nafanyaje sasa." aliwaza aron.

Akiwa kwenye mawazo simu yake ya mkononi ililia.Kuangalia ilikuwa ni namba toka kwa watu wa mirathi.Alipokea na kuiweka sikioni.

" ndugu habari yako?"

" safi habari za kwako pia?"

" mimi mzima,nilikuwa nakutaarifu kuwa cheki yako ya mirathi iko tayari ,ivyo njoo kesho asubuhi uichukue"

"Asante!,asante sana" aliongea Aron huku akifurahi.Moyo wake ulilipuka kwa furaha baada ya kupokea taarifa hiyo.

" siamini,aisee siamini!,yaani milioni 159 zinaenda kuwa zangu. Kwanza nitaenda dar kununua gari la kutembelea.kisha nita nita..." aliwaza Aron huku akiwa na mawenge.Hakuwahi kushika hata milioni tano za kwake.Leo kaambiwa anaenda kupata milioni 159.

"Katika hili Helena anisamehe tu.Kiukweli anisamehe tu.mmmmh! Laikini kama yupo hai na yupo hapa hapa ,anaweza kuniletea shida huyu.Dawa yake ni kumuua tu.Ndio akifa nani atajali. Hakuna atakayejua kama ni mimi kwanza" aliwaza aron.

" sasa namuuaje.Njia nzuri ni kwakutumia mganga.Tena inabidi nifanye haraka kabla ndugu wemgine hawajamuona.Mmmmh hapa hakuna kupoteza muda.Leo hii hii namuua.Ngoja niende kwa mganga" aliwaza aron kisha akaingia chumbani kwake akavaa koti na kutoka nje kuelekea kwa mganga.

Alifika kwa mganga wake aitwae mlopo.Akamueleza shida yake.

" kama ni ilo ,ilo ni swala ndogo.Kwakuwa ni ndugu yako ,tena ni mtoto wa mdogo wako,basi kazi haitakuwa ngumu.Leo hiii hii anakufa.kesho hataiona" aliongea mganga kisha akaingia ndani kuchukua kioo na kutoka nacho nje.

AKafanya uganga wake kwenye kile kioo ikatokea sura ya helena.

" bila shaka mtu mwenyewe ni huyu au" aliuliza mganga

" ndio ni yeye"

" sawa kama ni yeye chukua kisu hiki na umchome kwenye kioo hapa.Ukimchoma tu na yeye popote alipo ataanguka chini na kupoteza maisha hapo hapo" aliongea mganga na kumkabidhi kisu Aron.

.......

Kwa upande wa wale vijana walimchukua helena wakampeleka kwa mzee komba.Mzee komba alifurahi sana kumuona madam H,sifa alizopewa zilimfanya atamani sana kukutana na madam H ambae ni helena.

Helena alikuwa hajui kama mzee komba ndiye aliyehusika na matatizo yake.Walikutana wakasalimiana.Lakini mzee komba alipomuangalia Helena vizuri alishtuka.

" wewe mbona kama ni........

Inaendelea hapa chini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[12/11/2019 17:17] Mjamaa: ILAANIWE SIKU NILIYOZALIWA - 23

Tulipoishia - Helena alikuwa hajui kama mzee komba ndiye aliyehusika na matatizo yake.Walikutana wakasalimiana.Lakini mzee komba alipomuangalia Helena vizuri alishtuka.

" wewe mbona kama ni........

Endelea nayo.

Mzee komba alimsogelea helena ," wewe kama nimewahi kukuona sehemu.Sura yako sio ngeni sana" aliongea mzee komba.

" utakuwa umenifananisha mzee .Mimi sikumbuki kukuona popote" alijibu helena.

Helena alikuwa hamjui mzee komba kwakuwa siku ile mzee komba anaingia kumpiga picha helena alikuwa amezimia.

Waliongea mawili matatu.Mzee komba alimshukuru sana helena kwakuja.Kama makubaliano ya mwanzo yalivyokuwa ,helena au kwa jina lingine madam H kazi yake ilikuwa ni kuwa mlinzi wa Mzee komba.Popote ambapo mzee komba ataenda helena naye ilitakiwa awepo.

Ukiachana na kumlinda .Mzee komba moyoni mwake alikuwa na mipango ya kumfanya helena awe bimdogo wake.Baada ya kumuona alivutiwa zaidi.

Wakiwa wanaongea gafla helena alianguka chini huku akiwa anashika tumbo.

" Tumbo,tumbo " alilalamika helena pale chini.

" Tumbo limefanya nini?" walimuuliza

" nahisi kitu kama kisu kimenichoma tumboni" aliendelea kulalamika helena huku akilishika tumbo lake.

Walimsogelea na kumuangalia tumbo.Cha ajabu hakukuwa na kitu chochote kilichomchoma tumboni.

" mmmmh! Huu mchezo," aliguna na kuongea mmoja wa walinzi wa mzee komba ambae ni mganga.Mzee komba mbali na kuwa na walinzi wa kawaida,Lakini pia uwa anatembea na mganga .Yule mlinzi wake ambae ni mganga,baada ya kuona hamna kitu tumboni,aliwaaambia wenzake wamuache pale pale chini kisha yeye akakimbia chumbani kwake akatoka na kikopo chenye unga mweusi.

Haraka sana akamrisha helena kwa nguvu.

" kula ,kula haraka. Meza, kula " aliongea yule mlinzi ambae ni mganga pia.

Helena haraka sana akaimeza ile dawa na maumivu ya tumbo pale pale yakaacha.Yule mlinzi alimwangalia helena kisha akamwambia.

" unabahati sana.Tungechelewa kidogo ungekufa. iyo dawa uliyoimeza imerudisha tego kwa mtu aliyetaka kukuua wewe"

" mmmmh! Atakuwa nani huyu.Au wale walionibaka wanataka kuniua tena ?" aliwaza helena.

.......

Aron kule kwa mganga baada ya kuchoma kisu kile kioo ,haikuchukua muda akaanguka chini na kuanza kulalamika tumbo.Ndani ya dakika tatu akakauka pale pale chini.

Mganga mlopo alimsogelea na kumtikisa. Alikuwa tayari kasha kufa.

" mmmmh! " Aliguna yule mganga.Aliwaza afanye nini.Haraka akamwita msaidizi wake na kumueleza tukio lilivyotokea.Wakashauriana chakufanya.

" hapa tukisema tuwaambie watu kuwa amekufa,kesi itakuwa kubwa kwetu." aliongea mganga.

" mmmh! Sasa tunafanyaje?

" Dawa hapa ni kuita tax na kumuwaisha hospital,yeyote atakayetuuliza tutasema tumeona hali yake imekuwa mbaya ndio maana tumeamua kumkimbiza hospital.Tukifika hospital najua watatuambia tumemchelewesha ameshakufa"

" baada ya hapo ndipo tutawaambia ndugu zake kuwa ndugu yao amekufa yupo hospital.Tukifanya hivi tutaepuka msala.Maana saizi ukisema mtu amefia hapa na alikuja mzima itakuwa kesi kubwa" aliongea mganga.

Walifanya kama walivyokubaliana.Waliita tax wakampeleka hospital.Hospital wakaambiwa wamemchelewesha amekufa.Baada ya hapo wakawapigia ndugu zake na kuwapa taarifa kuwa ndugu yao amekufa.

Mshtuko kwa ndugu ulikuwa mkubwa sana.Kilichowashtua ni ukweli kuwa Aron hakuwa anaumwa.Na siku ile baadhi ya ndugu walimuona alikuwa mzima wa afya.

Ndugu waliwahi hospital kuthibitisha kama ni kweli .Walionyeshwa maiti ya ndugu yao,wakamtambua ni yeye.Kilio kikawa kikubwa sana.Taratibu za mazishi zikafanyika.Wakamzika.

Baada ya Aron kufa.Habari ya mirathi ikasimama.Ilibidi ndugu wakae chini tena kumteua mtu mwingine ambaye atasimamia mirathi.

.................

Siku zilienda, miezi ikakatika.Mzee komba hakutaka kumlazimisha helena awe mke wake,alikuwa anamshawishi taratibu kwa vitendo.Alianza kumshawishi kwa kumtendea mema mengi.Helena alikuwa kama malikia,na taratibu akaanza kumpenda mzee komba.

Lugha nzuri,na matendo mazuri aliyokuwa anamfanyia yalimfanya helena amuone mzee komba kama ni mtu mwema.

" ukiwa tayari utaniambia,sitakulazimisha kitu chochote mpaka pale mwenyewe utakapokuwa tayari.Nataka uwe mke wangu nimekupenda sana.Nataka na wewe unipende kama mimi ninavyokupenda.Sitaki mapenzi yetu yawe ya ngono ,japo muda ukifika itabidi tukutane kimwili" aliongea mzee komba.

Maneno ya mzee komba yalimfanya helena amuone mzee komba kama ni mwanaume wa tofauti sana.Wanaume wote aliowahi kukutana nao walikuwa wanataka ngono siku ya kwanza tu,kwa mzee komba ilikuwa tofauti,na utofauti huo ulimfanya helena taratibu aanze na yeye kumpenda mzee komba.

ili kujionesha kama ni mwema sana.Mzee komba allimficha helena baadhi ya shughuli zake,hasa zile zilizohusu kuteka watu na kuua watu.

Siku moja mzee komba alimchukua helena na kwenda nae kwenye kituo cha watoto yatima.Kufika pale alitoa msaada mkubwa sana.Walipika chakula pale kituoni na kula pamoja.Helena alijisikia raha sana.

Muda ukaenda wakarudi nyumbani.Kufika nyumbani helena akaamua kutomuwekea mzee komba kizuizi chochote,aliamua kumkubalia awe mumewe.Alimshika mkono na kumvuta kuelekea chumbani kwake.

Kufika kule kwa mahaba mazito helena alifunga mlango kisha akamsukumia mzee komba kitandani.Mzee komba alianguka kama mzigo .Helena kwa mahaba mazito alimsogelea na kuanza kumvua shati

ILAANIWE SIKU NILIYOZALIWA - 24

Tulipoishia - Kufika kule kwa mahaba mazito helena alifunga mlango kisha akamsukumia mzee komba kitandani.Mzee komba alianguka kama mzigo .Helena kwa mahaba mazito alimsogelea na kuanza kumvua shati.

Endelea nayo.

Akiwa anamvua shati mzee komba kwa mahaba mazito.Simu ya mzee komba iliita.Alitaka kutoipokea lakini alipoangalia namba ilikuwa ni namba ya kijana wake muhimu sana.Aliipokea na kuiweka sikioni.

" halooo" aliongea mzee komba

" haloo mzee habari?"

" unanipotezea muda.Umenipigia simu ili uniambie habari au? ,hebu sema haraka ulichotaka kuniambia" aliongea mzee komba huku akimuangalia helena kwa uchu.

" mzee nina taarifa mbaya sana.Shaban yupo Tanzania ,na yupo hapa hapa pwani anatufatilia"

" mmmmh! Unasemaje?" aliuliza mzee komba kwa mshangao.

" kama nilivyokuambia mzee."

" basi haraka sana niitie vijana wangu wa kazi wote,ili niongea nao"

" sawa mzee,kwahiyo unataka kuongea nao lini?"

" unauliza lini tena wakati kuna mtu anatupeleleza.Nataka niongee nao leo hii" alifoka mzee komba kisha akaiweka simu mezani.Mudi yake ilishaharibika.Alimgeukia helena na kumwambia

" samahani mpenzi ,leo ilikuwa ndiyo sio ya kwanza mimi na wewe tukutane kimwili,ila naona haitawezekana,tutafanya siku nyingine" aliongea mzee komba huku akionekana kama mtu mwenye wasiwasi.Taarifa ya shabaan kurudi kuwachunguza ilimchanganya.

Hofu aliyoionesha mzee komba machoni ilimpa udadisi helena.Akataka kujua ni kitu gani kilichomchanganya mzee komba vile.

Majira ya saa moja jioni mzee komba akaondoka kuelekea walikopanga kuonana na vijana wake.Helena kwasababu ya shauku ya kutaka kujua nini kilichompa hofu mzee komba akaamua kumfata kwa nyuma na gari nyingine bila mzee komba kujua.

Mzee komba alifika kwenye nyumba moja ya kifahari akafunguliwa mlango na kuingia ndani.Helena aliiangalia ile nyumba ,akawaza kisha akaamua kuzunguka nyuma ya nyumba na kuruka ukuta.

Baada ya kuruka ukuta kwa mwendo wa kunyata aliingia ndani na kuanza kumtafuta mzee komba mle ndani.Akiwa anazunguka kwa siri siri mle ndani alimuona mzee komba akiwa na vijana ishirini wakiwa kwenye meza kubwa wakizungumza.

Katika wale vijana waliokuwepo pale alimuona joel na wale vijana wengine waliombaka.Mapigo yake ya moyo yakawa yakaanza kwenda kasi .Akataka kuingia.Lakini kabala hajaingia kuna mtu alimshika bega .

Kugeuka kumwangalia alikuwa ni saidi.

" aaah madam H,unafanya nini hapa?" aliuliza saidi

Helena hakumjibu kitu.

"Sikiliza madam H,ujue mzee komba hataki kabisa kuchunguzwa,akijua unamchunguza kama hivi atakachokuja kukufanya hutokuja kukisahau.Shauri yako mwenyewe. Kuna askari mmoja anaitwa noel alikuwa anamfatilia na kumvurugia mipango yake.Alichomfanya ni balaaa." aliongea said

Jina noel ni jina la baba yake helena.Baada ya kumsikia said amelitaja haraka sana helena akamuuliza saidi

" alimfanya nini huyo noel?" aliuliza helena.

" mmmmh ni balaaa,alimteka mtoto wake wa kike,kisha akawapa vijana wake wambake kwa zamu,kama iyo haitoshi aliiteketeza familia yake yote kwa moto" aliongea saidi.

Inaendelea hapa chini sehemu ya mwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ILAANIWE SIKU NILIYOZALIWA - 25

Tulipoishia -
" mmmmh ni balaaa,alimteka mtoto wake wa kike,kisha akawapa vijana wake wambake kwa zamu,kama iyo haitoshi aliiteketeza familia yake yote kwa moto" aliongea saidi.

Endelea nayo.

Maneno ya saidi yalikuwa ni kama kisu moyoni kwa Helena.Aliishiwa nguvu akajikuta amekaa chini.Taratibu sura yake ikaanza kubadilika,mwili wake wote ulianza kutetemeka kwa hasira.

" aaah !madama H mbona ivyo?" aliuliza said kwa uwoga.

Helena hakumjibi kitu,alimpiga pigo moja shingoni pale pale saidi akapoteza fahamu.Alichukua silaha yake na kuingia kwenye kile chumba walichokuwa wanafanya mkutano.

Kama kichaa alianza kuwamimina risasi mfululizo.Kila aliyekuwa anamlenga alikuwa hamkosi.Kelele za risasi ziliwafanya walinzi waliokuwa nje waingie ndani haraka na wao waanze kushambulia.

Walishambuliana mle ndani kwa muda mrefu sana.Mafunzo aliyoyapata kwa al sha baab yalimsaidia sana helena.Alifanikiwa kuwapiga risasi walinzi wengi sana.

Mzee komba baada ya kuona hali ni mbaya,alipita mlango wa siri akatokea nje.Lakini ile anafika nje tu,alikutana na shabaan akiwa na askri wengine uso kwa uso. Walimkamata na kumweka chini ya ulinzi,wale askari waliingia ndani na kuanza kushambulia,waliwashambulia na kuwakamata vijana wengi.

Helena alipowaona askari alijificha na kuangalia kinachoendelea.Alimwona mzee komba akiwa kakamatwa,pia aliwaona wale vijana waliombaka wakiwa wamekamatwa na kupakizwa kwenye gari.

Gari ziliwasha na askari wakaondoka na wale watu.Helena moyo wake bado ulikuwa unamuuma sana.Hakuridhika wale watu kukamatwa,alitaka wafe wakiwa mikononi mwake.Akaamua kuzifata gari kwa nyuma .Alizafata hadi zilikoishia,Mzee komba na wenzake hawakupelekwa polisi,walipelekwa kwenye nyumba ya siri ya usalama wa taifa kwa ajili ya kuhojiwa.

Helena aliiangalia nyumba waliyoingizwa kisha akarudi kujipanga vizuri.Majira ya saa saba usiku alienda kwenye ile nyuma na kuvamia akiwa na visu vingi bila bunduki.

Kwakutumia mbinu za kijeshi alifanikiwa kuingia ndani.Alizunguka mle ndani kumtafuta mzee komba na wale vijana waliombaka.Kutokana na giza na ukimya uliotawala mle ndani aliangaika sana,lakini mwishowe alifanikiwa kuwaona joel na wale vijana waliombaka.Kwakutumia funguo bandia alifungua selo yao na kuingia ndani.

Joel akiwa amelala alihisi maumivu makali ya tumbo,alishtuka na kujishika tumboni,alishangaa kukuta amechomwa kisu cha tumbo.Alimwangalia aliyemchoma alikuwa helena,alitaka kupiga kelele helena alimziba mdomo na kumkata koromeo .Alinyosha mkono ili amshike helena ,Lakini kabla hajamshika akakata roho.

Purukushani alizozifanya joel ziliwafanya vijana waliokuwa mle waamke na kuanza kupiga kelele baada ya kuona damu.Kwa kasi ya ajabu ,huku akiwa kama amechanganyikiwa helena alianza kuwachinja mmoja baada ya mwingine.Kila aliyejaribu kupambana naye aliambulia patupu.
ndani ya dakika kumi chumba kizima kikawa kimejaa damu na maiti.Helena mwili wake wote ulikuwa umelowa damu.

Aliitafuta maiti ya joel akaipata,bila huruma akaanza kuichoma visu mfululizo,alijua kwakufanya hivyo hasira zake zitapungua lakini kila alipomchoma ndipo kumbukumbu za nyuma zilipomjia na kuzidi kumchoma zaidi.

Kelele alizokuwa anazipiga wakati anamchoma visu ziliwafanya askari waliokuwa wanalinda nje waje ndani haraka.

Sauti za viatu vya watu wakija ndani zilimfanya helena asimame pale alipo na kwenda kujificha kwenye nyuma ya mlango.Askari waliingia mle ndani wote,baaa ya kuingia wote helena alitoka na kuwafungia mlango kwa nje.

Baada ya kuwafungia ile anatoka tu aliwekea bastola kichwani.Aliivyogeuza macho yake kumuangalia aliyemuwekea bastola,alikutana uso kwa uso na martini,ambae alikuwa ni rafiki wa baba yake.

Martini alishangaa kumuona mtu aliyemshikia bastola ni mwanamke.Akawauliza wenzake.

"Kuna mwingine huko?" ,ila kabla hajajibiwa,helena kwa spidi ya ajabu alipiga mkono wa martini bastola ikaruka juu.ile martini anashtuka akakuta helena ameshaikamata bastola na kumwekea yeye kichwani.

" nionyeshe aliko mzee komba" aliongea helena.

Martini akawa anajiuma uma ,kitenda cha kujiuma uma kilimkera helena akamkandamiza zaidi ile bastola kichwani.Martini hakuwa na jinsi akaongoza njia mpaka walikomfungia mzee komba.

Kufika alipofungiwa mzee komba ,helena alimsachi martini akamkuta na pingu,akamfunga nayo kwenye chuma kilichokuwa pembeni kisha akamsogelea mzee komba.

" kosa langu ni nini? Familia yangu imekukosea nini?" aliuliza helena huku akitokwa na machozi

Swali lile lilimfanya mzee komba amuangalie vizuri helena.Alijaribu kuvuta kumbukumbu akakumbuka unyama aliomtendea.

" nakuuliza wewe? Kosa langu ni nini?, baba yangu na mama yangu wamekukosea nini?"

Mzee komba alimwangalia helena kwa huzuni sana.Nafsi yake ilianza kujuta yale ya nyuma.

" najua ata nikikuomba msamaha haina maaana yeyote,hautaweza kunisamehe.Sina la kukuambia helena,ninachoweza kusema ni kuwa sikutakiwa kuzaliwa,"

" yaaani pamoja na yote hutaki kuomba ata msamaha" alifoka helena.

Martini aliyekuwa pembeni amefungwa pingu baada ya maelezo ayo akamtambua helena.Kwa mshangao mkubwa akamuuliza.

" aaah! Wewe ni helena. Mtoto wa naoel. Nisamehe na mimi nilishindwa kumtafuta aliyemuua baba yako.Huyu mzee nilimuamini lakini huku mwisho nimekuja kugundua ata mimi amenifanyia ubaya mkubwa." aliongea martini

Helena kila alipomuangalia mzee komba hasira ilizidi kumpanda,aliokota kipande cha nondo kilichokuwa pale chini na kumpiga nacho kichwani.Martini akawa anamsihi asimuue amuache sheria ifate mkondo wake.

" naomba usimuue helena,muache sheria ifate mkondo wake,usiichafue mikono yako na damu yake" aliongea martini lakini helena hakumwelewa.Alimshika mzee komba na kuanza kumpiga mfululizo usoni na kile kipande cha chuma.

" niambie ,tulikukosea nini? Sema tulikukosea nini " aliongea helena.

" nisamehe helena,nisamehe martini kwa yote niliyokufanyia, nimetenda uovu mwingi sana.Naomba mnisamehe,nisameheni" aliongea mzee komba huku akivuja damu.

Maneno ya mzee komba hayakupunguza hasira ya helena,alichukua kisu na kumchoma nacho tumboni mfululizo.Martini alipiga kelele kumzuia helena asifanye vile lakini halikuwa amechelewa,helena alimchoma visu mfululizo tumboni mzee komba.

" kwanini unajiaribia maisha helena.Nani alikuambia kuua ndio dawa" alifoka martini.

Helena alitupa kisu chini na kukaa chini.

" kuzaliwa kwangu kumeleta matatizo duniani,ILAANIWE SIKU NILIYOZALIWA " aliongea mzee komba kwa shida na pale pale akakata roho.

Haukupita muda askari wengi wakafika eneo lile.Kati ya waliofika shabaan alikuwepo.Shabaan aliingia kile chumba alichokuwa helena ,na martini .kufika mle alikuta maiti ya mzee komba ipo chini.

Martini alimuomba shabaan amsaidie helena kutoka mle ndani kwa siri bila kukamatwa,na pia akamuifadhi nyumbani kwake.

Kama alivyoelekezwa na martini alimtoa helena kwa siri bila kujulikana,na moja kwa moja akampeleka nyumbani kwake.

.........

Siku zilienda helena akaenda kwa ndugu zake.Wakampokea,wakafanya taratibu mafao yote ya wazazi wake akapewa yeye.Akaanzisha biashara,maisha yakaenda kwa amani kabisa.Akawa rafiki mkubwa sana wa shabaan.kutokana na uwezo wake wa kijeshi ,Martini na shabaan wakamfanyia mpango akaingia jeshini,akawa askari.

Mwisho.....Maoni muhimu.

................

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ILAANIWE SIKU NILIYOZALIWA - 17

Endelea nayo.

Martini alitetemeka kwa uwoga na kupiga kelele. " mwacheni mwananguuu nitawaua wote wanaharamu nyie" aliongea kwa sauti martini.

Sauti upande wa pili ikiwa imebadilishwa kwa programu maalum ilimjibu. " kama utatuua basi hakuna namna, itabidi tumbake mwanao hili hata kama utatua tuwe tumemfaidi mwanao"

" Hapana msifanye ivyo,niambieni mnataka nini mimi nitawapa.Semeni chochote ,Naomba mwacheni mwanangu tafadhali" aliongea martini na kulia kama mtoto mdogo.

" ok sawa,Acha kutufatilia .Achana na habari ya kifo cha rafiki yako baba helena,na achana kabisa na habari yako ya kunifatilia.Hili ni onyo la mwisho.Usipoelewa tutamfanyia mwanao unyama usiowahi kuhusikia"

" sawa ,sawa ,sawaaaa,sawa" martini alijibu huku akilia kuwa ataachana na upelelezi wake.Pale pale simu ilikatwa.

Mzee komba alimwambia yule kijana avae nguo na asimbake Husna.Walimvesha nguo husna kisha wakamfunga kitambaa machoni na wakampakia kwenye gari na kwenda kumshusha nyumbani kwake,kisha wakatokomea.

Martini aliapa kutofatilia tena kesi ya mauaji ya rafiki yake.Alilia kama mtoto akiwa chumbani kwake.Akiwa amelala kitandani huku akilia alimsikia mke wake akipiga kelele .

" mwananguuu,mwanangu" aliongea mama husna na kumkimbilia mwanae na kumkumbatia.Martini alisimama na kutoka nje.HAkuamini macho yake.Mwanae alikuwa mzima wa afya.

Martini alijiapiza kutofatilia tena ile kesi.Alimkumbatia mwanae na kuingia nae ndani.

............

Majira ya saa moja usiku,Shabaan alikuwa amepanga kukutana na mzee komba.Mzee komba naye aliandaa vijana ili wamkamate na kumuua kabisa.

Mzee komba alifika sehemu waliyopanga kukutana .Muda ulienda lakini shabani hakuonekana.Walijaribu kumpigia simu lakini pia simu yake haikupatikana.

" mmm!h!,au atakuwa ameshatushtukia?" aliuliza mzee komba.

Waliendelea kukaa kwa muda mrefu bila shabaan kutokea.Walikata tamaa na kuamua kuondoka.

........

Siku zilienda miezi ilikatika bila shabaan kuonekana.Martini naye alikata tamaa kabisa,aliachana na kesi ya mauaji ya rafiki yake.Hakutaka hata kuisikia.

Alienda kwenye kaburi la baba helena na kumuomba radhi.

" nisamehe baba helena,nimeshindwa kumpata aliyesababisha kifo chako.Nisamehe sana.Nisamehe kwakuwa nimeamua kuacha kabisa kumtafuta.Nimefanya hivi kwa usalama wa mwanangu."aliongea martini huku machozi yakimtoka.

......

Kitendo cha shabaan kutoonekana kwa muda mrefu kilimpa wasiwasi mzee komba.Alipata wasiwasi kwasababu Shabaan alikuwa anajua mambo yake mengi.Alihisi labda siri zake nyingi zitakuwa wazi.ili kukabiliana na ilo akaamua kusimamisha shughuli zake kwa muda kwanza ili kupeleleza na kujua nini kinaendelea.

....

Kwa upande wa helena aliendelea kujifua pamoja na kundi la al sha baab.Alifanya mazoezi kwa nguvu zote.Kila alipokumbuka jinsi alivyotendewa alikuwa anaenda kufanya mazoezi kwa nguvu zote ili kupunguza mawazo.Alijiapiza kuja kuwachinja wale wote waliomtendea ubaya .Tangu siku ile aliyomuona joel hakumuona tena.Joel alikuwa kwenye kambi nyingine tofauti na yeye.

Ujasiri wake uliwafanya viongozi wa al sha baab wampende.Walikuwa wanamuita dada shujaa.uwezo wake ulikuwa ni mkubwa sana.Alikuwa anauwezo wa kupambana na wanaume zaidi ya ishirini peke yake.Licha ya kupendwa kwa ujasiri wake lakini aliogopwa sana na wenzake kutokana na userious aliokuwa nao.Muda wote alikuwa amenuna ,alikuwa hacheki,alikuwa kauzu kweli kweli.

Aliwachukia sana wanaume.Aliwachukia zaidi hasa alivyowaona pale kambini jinsi walivyokuwa wanawakamata wasichana wadogo kijijini na kwenda kuwabaka.Aliapa kuja kuwaua wanaume wote.Aliwachukia sana,aliamini wao ndio chanzo cha uovu uliokuwepo duniani.

...
Miaka miwili ikakatika mzee komba akaamua kuanza tena biashara yake.Aliamua kubalisha wafanyakazi wake wote,na hii ilisababishwa sana na tukio la shaaban,alihisi pengine wapo wengine ambao walikuwa wanatumiwa na serikali.

Aliwatumia hela al sha baab wamletee vijana watatu wa kazi na mlinzi mmoja.Ahmed kiongozi wa al shaabab ,alimuandalia vijana watatu pamoja na helena ambae alitakiwa aende akawe mlinzi wa mzee komba.Kutokana na ujasiri wake waliona helena ndi mtu pekee mqenye sifa za kumlinda mzee komba.Walimwambia helena ambae sasa walikuwa wanamuita Shujaa H.Helena aliwakubalia bila kinyongo kwani alikuwa na hamu kubwa ya kurudi tanzania kulipa kisasi.

Al sha baab waliwasiliana na mzee komba na kumpa sifa za helena ambao wao walikuwa wanamwita shujaa H. Mzee komba alitamani kumuona kutokana na jinsi walivyomsifia.

" huyu madam H kwa sifa zake itabidi awe mke kabisa.Atakuwa mlinzi wangu lakini pia nataka awe mke wangu." aliwaza mzee komba.

Inaendelea hapa chini

Sent using Jamii Forums mobile app
nyingine lini???
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom