Ila sio siri, Harris Kapiga wanakera!!

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
3,865
5,683
ni huyu Machugu wa star tv na huyu kapiga wa clouds tv!
nakerekwa mno na tabia zao zifuatazo ambazo ambazo mi huwa naona hazina maana;

1. kujichekesha chekesha. muda wote wa habari wamekuwa ni wa kujilazimisha kuchekacheka na kutabasamu....huyu Kapiga ktk eneo hili ndo amezidi maana si kwa kuchekacheka vile,inazidi mpaka inakuwa kero.
2. vionjo vya kujitikisatikisa (gestures) kwa wingi. mara waangalie saa, mara warusherushe mikono, mara wapige salute.....inaboa kwakweli wakati mwingine.
3. kutoa maoni/kuongeza maneno baada ya habari. taarifa inaweza kuwa imewasilishwa vizuri tu na mhusika aliyopo field, lakini akishamaliza lazima wao watie vijineno vya hapa na pale wakati mwingine havina maana yoyote na vinapelekea kuondoa ladha iliyopatikana tayari.

waache/wapunguze bwana!

maoni yangu lakini, sina taaluma yoyote ile ya habari
 
Mambo kama hayo huwezi kuyaona ITV wala eatv tv ya burudani hata kwa bahati mbaya. Habari haihitaji conclusion
 
Back
Top Bottom