Ila JK ni mtu mmoja mjanja sana

Ila JK ni mtu mmoja mjanja sana

Planett

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2014
Posts
10,561
Reaction score
16,339
Leo nimeamini kua JK ni mjanja sana,. Check response yake kwenye maswali aliyoulizwa na Salama Jabir.

Salama: Kwanini watu wanakupenda sana.
JK: Waulize haohao wanaonipenda mimi sijui bwana

Salama: Lakini unajua kuwa tunakupenda
JK: (Pause kidogo)... Najua kuwa hamnichukii

Ila JK wewe sawa tu leo hujui kua watanzania tunakupenda kweli? Ila sisi tutaendelea kukupenda tuu mzee wetu.
 
Wanampenda kwasababu alikuwa rais dhaifu.
Kweli bhana. Si unaona kwa Rais strong, kila anapoanza awamu vitu hupanda. Mfano sukari mwaka 2015 kabla hajaingia ilikuwa 1500/= leo inasoma 2800/= kwa kilo.

Mafuta ya kupikia sie wanyonge, kwa Sasa yanatunyoosha, tunawaza kuanza kutumia mafuta yatokanayo na maziwa ya ng'ombe.

Hiyo cement Sasa, huyu Rais strong mpaka sasa sisi wanyonge tunafikiria kurudi kwenye ujenzi wa nyumba za miti maana kashindwa kabisa kufanya bei iwe chini.

Sijui Rais dhaifu alifanyanje fanyaje wanyonge tulinunua vitu kwa bei chee, Ila huyu strong anazidi kutunyonga sie wanyonge.
 
Wanampenda kwa sababu hakuua watu...
Wakati wake kwetu pemba hatukuzika hata paka
Kule Bara kulikua hakuna watu wasiojulokana
Media ilikua huru
Hakujenga miradi ya matrillion kijijini kwao
Hakubanbukiza kesi na kufilisi wapinzani
Hakutumia TRA, TAKUKURU, POLICE, JESHI wala MAHAKAMA kujinufaisha kisiasa
Alikua Rais mwenye Baraka tele na watanzania tulikua tuna Hali nzuri kiuchumi
 
Kila mtu anaudhaifu wake lakini hakua katili wala muuaji
Alikua Rais mwenye Baraka tele na watanzania tulikua tuna Hali nzuri kiuchumi
Eeh si ndio nyie mlisema jk ni muuaji na ndio alisababisha askari wakaua kwenye maandamano ya chadema 2011 kule arusha?
Mkaenda mbali mkasema ndio alitoa amri ya kulipuliwa bomu kule olasiti?
Mkamsema kaua watu kwenye uchaguzi igunga?
Mkamsema kampandisha cheo askari aliyemuua mwangosi.
Mkamsema katuma watu kwenye kumpiga risasi na kumuua Dr.mvungi
 
Alikuwa Raisi wa watu na sio Raisi wa vitu.

Jiwe Ni rais wa SG, Flyover, na barabara mle,mteseke,mpate maafa,msiajiriwe,msipandishwe mishahara,mtekwe,mchapwe viboko, halimuhusu.
On top of that no mBinafsi sana
Yaani anajenga kwao miradi ya mabillioni kila kukicha
Katibu mkuu wa wizara ya fedha pia ni mshika funguo za hazina ya nchi ni mtoto wa dadake
Kandarasi za ujenzi anapewa mayanga construction bila zabuni kwa sababu ni mume mwenzake
Huyu mtu adui wa nchi
 
kuna dokta moja anaitwa dokta ULIMBOKA
huyu daktari alipata kichapo kutoka kwa TISS
alipotibiwa na kurud toka SA . HAKUONGEA TENA.
juu ya kilichomkuta

kilikua kipindi cha JK

JERRY MURO
pia nae alijifanya anaijua kazi yake
ya HABARI vizuri
nae vivyo hivyo kichapo na kesi
takukuru juu...
nae KIMYAAA

Sasa napoona hapa oh jk hakua mkorofi napata shida kidogo
 
Back
Top Bottom