Ikulu yaanza kumwandama Tido Mhando................ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu yaanza kumwandama Tido Mhando................

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 19, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,958
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Mwananchi linaripoti ya kuwa Mkurugenzi mstaafu wa TBC Bw. Tido Mhando mikataba aliyosaini na BBC na RFI imeanza kuchunguzwa kwa kile kinachodaiwa ni kuona kama masilahi ya taifa yalizingatiwa................................

  Swali ninalojiuliza ni kuwa hivi dhambi za Tido, kama zipo, CCM ilianza kuziona baada ya kwisha kwa uchaguzi huu tu?

  Hivi kweli BBC Idhaa ya Kiswahili na hiyo Radio ya ufaransa kweli kweli zimeleta uchochezi upi kwa kusema ukweli?

  Huyu JK kama kazi imemshinda si ajiuzulu tu asisubiri Bunge likamfukuza kazi................

  Serikali yachunguza mashirika ya BBC, RFI Wednesday, 19 January 2011 08:42

  Mwandishi Wetu
  SERIKALI ya Tanzania inalifanyia uchunguzi shirika la utangazaji la Uingereza (BBC), ikilishuku shirika hilo la Serikali ya Uingereza kwamba linafanya shughuli za uchochezi nchini. Halikadhalika, Serikali pia inafuatilia kwa karibu nyendo za Radio ya Kimataifa ya Ufaransa (Radio France International, RFI), ili kubaini iwapo hatua yake ya kuanzisha Idhaa yake ya Kiswahili inayotangazia kutoka jijini Dar es Salaam haina ajenda ya siri ndani yake.

  Kitengo cha BBC kinachotiliwa shaka na Serikali ni kile cha mfuko wa misaada wa matangazo yake ya kimataifa, yaani BBC World Service Trust (BBCWST), ambacho mapema mwaka jana kiliingia mkataba wa kulisaidia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), kwa mafunzo na vifaa. Mfuko huo wa misaada ya BBC hivi sasa unafanya kazi katika nchi nyingi duniani hasa zile zinazoendelea zikiwemo nchi kadhaa za kiafrika kwa kutumia fedha wanazozipata kutoka kwa wahisani wakisadia kuimarisha utangazaji wa kisasa.

  Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa mkataba wa baina ya TBC na BBCWST ni wa miaka mitano na unafadhiliwa na fedha kutoka Shirika la Kimataifa la Misaada ya Maendeleo la Uingereza (DFID). Nchi nyingine za Afrika zenye mkataba kama huo ni Angola na Siera Leone. Hatua ya kuchunguza ushirikiano huo wa BBCWST na TBC umo kwenye maelekezo ya barua ulizoandikiwa uongozi wa juu wa TBC, mwezi Novemba, 2010.

  Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo katika moja ya barua ya maelekezo yake, alimtaka Mwenyekiti wa Bodi ya TBC, Wilfred Nyachia kumpa maelezo ya kina kuhusu mikataba ya mashirika hayo.

  Mmoja wa maofisa waandamizi katika wizara ya Habari, Vijana, na Michezo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema kumekuwepo na wasiwasi serikalini ya kwamba BBCWST limehusika katika kuifanya TBC itangaze matukio yaliyoikera wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka wa jana.

  Kadhalika kumekuwepo na hisia miongoni mwa watu kwamba matangazo ya uchaguzi ya TBC ndiyo yaliyoifanya Serikali iamue kutomuongezea mkataba mwingine aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Tido Mhando.

  Mhando hakuongezewa mkataba na Serikali licha ya tathimini isyo rasmi ya wadau wa habari nchini kuonyeha kuwa chini ya uongozi wake shirika hilo limeweza kufanya kazi yake bila kuegema upande wowote hasa wakati wa uchaguzi, taarifa ambayo pia imo kwenye ripoti mbalimbali za waangalizi wa kimataifa na kitaifa wa uchaguzi huo. Hata hivyo, akihutubia maafisa wa habari wa wizara mbalimbali mjini Mbeya mwezi uliopita, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, na Michezo, Seth Kamuhanda alisema Serikali ilikuwa ikiyafanyia uchunguzi mashirika ya habari ya kimataifa ambayo yamekuwa yakiendesha ama kutangaza mambo ya uchochezi.

  Radio ya RFI inayomilikiwa na Serikali ya Ufaransa, ilianza kutangaza matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili kupitia radio ya TBC FM katikati ya mwaka uliopita lengo likiwa ni kusaidia kusambaza lugha ya Kiswahili kwenye nchi nyingine za kiafrika ambako radio hiyo husikika. Maafisa kadhaa wa Serikali walihudhuria sherehe za uziinduzi wa kituo hicho mwezi Septemba mwaka jana katika hafla iliyofanyika katika ofisi za ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam. Baada ya maelekezo kutoka kwa Luhanjo, uchunguzi wa Mwananchi umegundua kuwepo kwa vikao mfululizo karibu kwa mwezi mmoja na nusu sasa kuhusu suala hilo, ambavyo vinawahusisha wajumbe wa kamati mbalimbali za bodi ya TBC.

  Mwenyekiti wa Bodi ya TBC Wilfred Nyachia, pamoja na kulijadili kwa kirefu suala hilo kwenye kikao kamili cha bodi kilichofanyika Desemba 21 mwaka 2010, pia amekuwa na mfulilizo wa vikao vingine. Wiki mbili zilizopita Nyachia alizungumza na wajumbe wote wa Bodi yake mmoja, mmoja, ana kwa ana na mapema wiki iliyopita, Mwenyekiti huyo akiwa pamoja na baadhi ya wajumbe wa bodi walikutana na viongozi wa BBCWST na RFI na baadaye wakafanya mazungumzo na baadhi ya viongozi waandamizi wa TBC. Wajumbe wengine wa bodi waliokuwepo kwenye vikao hivyo ni pamoja na Balozi Ben Mosses, Profesa Henry Mgombello na Kiongozi wa idara moja nyeti ya Serikali.

  Nyachia alipoulizwa kuhusu taarifa hizo alailiambia gazeti hili kuwa hana habari za kuwepo kwa hali hiyo, hajui lolote na wala hajaambiwa. Nyachia alisema katika bodi hiyo ya TBC yeye ni mwenyekiti wa vikao tu na si mtendaji hivyo, hilo linaweza kuwepo na yeye asijue na si ajabu. "Sina habari ya mambo hayo, kama yapo unajua siku hizi mambo si kama zamani hakuna 'executive chairman' (Mwenyekiti mtendaji) enzi za mwalimu kama walivyokuwa wakina Mwaikambo NBC," alisema Nyachia.

  Aliongeza,"Mimi ni mwenyekiti wa vikao, si executive, inawezekana lipo, lakini mimi sijui hilo." Mjumbe mmoja wa bodi ya TBC ambaye naye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema baadhi yao hawaelewi tatizo hasa ni nini. "Ni nani ambaye hafahamu umahiri wa BBC kwenye shughuli za utangazaji, na ni nani ambaye hangependa wafanyakazi wake wapatiwe mafunzo na BBC?", alihoji mjumbe huyo. Aliongeza, "Kama kuna kitu kingine kizuri ambacho Tido ameifanyia TBC wakati wa uongozi wake basi ni ushirikiano huu aliouunda na mwajiri wake huyo wa zamani yaani BBC".

  Imefahamika ya kwamba uchunguzi wote huo umefanywa kwa nguvu, baada ya kumalizika kwa mkataba wa Tido, huku taarifa nyingine zikidai kwamba Mkurugenzi Mkuu huyo wa zamani wa TBC ambaye anatajwa kuwa mhusika mkuu katika suala hilo huku alihusishwa katika mchakato unaoendelea hivi sasa. Baadhi ya wafanyakazi wa TBC waliozungumza na Mwananchi kuhusu hali ya TBC kwa sasa, walisema wasiwasi mkubwa uliopo ni muelekeo mzima wa hali ya uongozi wa shirika hilo.
  Walisema awali hali ya shirika ilikuwa imeanza kupata mwelekeo mzuri unaoeleweka, lakini sasa haifahamiki ni nani mwenye kufanya uamuzi kuhusu shirika hilo la umma ambalo miaka mitatu tu iliyopita ilifanya sherehe kubwa ya uzinduzi, kutoka kuwa taasisi ya Serikali na kuwa shirika kamili la umma la Utangazaji, mgeni rasmi akiwa Rais Jakaya Kikwete. Kwenye hotuba yake ya uzinduzi huo, Rais Kikwete alisema mabadiliko hayo maana yake ni kuwa kuanzia wakati huo TBC ni shirika la utangazaji la umma wa Watanzania wote, litakaliokuwa na uamuzi wake wenyewe na hasa katika masuala ya uandishi wa habari kwa kuzingatia misingi ya weledi na linalotarajiwa katika muda usio mrefu kujitegemea wenyewe kimapato.
  "Lakini sasa tunaona mambo yanakwenda kinyume na hayo, labda Rais pekee ndiye aliyejua ni nini maana ya mabadiliko aliyoyafanya maana kwa sasa amri nyingi zinatokea wizarani," waliongeza, huku wakitoa mfano wa kipindi maalum cha ghasia za hivi karibuni zilizotokea mkoani Arusha kilichorushwa hapo mwishoni mwa wiki. Uchunguzi unaonyesha kwamba kwamba kipindi hicho kilisimamiwa na mkurugenzi wa idara nyeti ya Serikali aliyewataka kutumia vifaa vya shirika hilo kukiandaa kisha kutangazwa siku ya Jumamosi na Jumapili na TBC1 pamoja na TBC Taifa.

  Tayari kipindi hicho kimezua mjadala mkubwa miongoni mwa wananchi, huku wataalamu wa mambo ya habari wakisema haikuwa sahihi kutangazwa kipindi kilicholalia upande mmoja tu na kwamba kiweledi idara ya Polisi ingefanya mkutano na vyombo vyote vya habari na kutoa picha zote walizotaka kuonyeshea utetezi wao kuhusu tukio hili. Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi wa TBC, Joe Rugarabamu alipoulizwa alisema kurushwa kwa kipindi hicho ni matakwa ya polisi na kwamba walilipia kipindi hicho.

  "Ile ni kama baada ya tukio upande mmoja umetoa maelezo yao nawe umekwenda kuwahoji polisi, nao wameeleza upande mmoja unaowahusu wao, walitaka kitoke na wamelipia," alisema Rugarabamu. Alipotakiwa kueleza wamelipia kiasi gani cha fedha, Rugarabamu alisema, "Siwezi kusema kwa sasa kwani nipo nje ya ofisi". Alipotakiwa kuzungumzia hatua hiyo ya Serikali kuwachunguza na kutaka kuwafukuza nchini, mkurugenzi wa RFI nchini, Victor Robert Wile alisema hawaweze kukurupuka na kulizungumzia hilo hadi watakapopata taarifa kamili juu ya kuwepo kwa mkakati huo wa Serikali.
  "Hatuwezi kulizungumzia hilo, sisi tuna msemaji wetu, tukipata hilo kwa undani tutazungumzia, lakini sasa hatuwezi kukurupuka," alisema Victor Robert Wile. Hivi karibuni, wakati wa sherehe za Mapinduzi Zanzibar, kwa kuzingatia mabadiliko mazuri yaliyotokea tangu kuanzishwa kwa TBC, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar nayo ilitangaza kuanzisha kwa Shirika lake la Utangazaji la Zanzibar, kwa kuziunganisha Sauti ya Tanzania Zanzibar na Televisheni Zanzibar.  Mwananchi limedai ya kuwa uchunguzi huo ni kufuatia maagizo ya kibosile mmoja pale IKULU........................
   
 2. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Itakuwa ni msiba mkubwa kwa hiyo ikulu ya rushwa na mauaji ya raia.
  Mtu unyimwe kazi baada ya utendaji wa kutukuka tena uandamwe????
   
 3. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wafanye hivyo tu mara baada ya kutujulisha maslahi ya taifa katika mikataba ya Richmond, Dowans, Meremeta, EPA, Umeme MW 600 na nyingine nyingi tu kabla ya kukimbilia hayo.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,958
  Trophy Points: 280
  Mafisadi pale Ikulu wakiongozwa na JK hawapo tayari kabisa ukweli juu ya tuhuma kebekebe zinazowakabili umma wa watanzania wazijue kwa hiyo wanatafuta mazingira ya kuanza news blackout and censorship...................
   
 5. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Viongozi wetu ndivyo walivyo
  Hawana aibu, hawamwogopi hata Muumba wao
  Wajichunguze wenyewe kwanza ndio warudi kwa Mhando
  Wanataka watu wote wajipendeke kwao na kuwashangilia kwa maovu yao
   
 6. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Nchi hii ina matatizo lukuki na tunaelekea shimoni hakuna jitihada za wazi kivitendo kubadili ueleko,mambo yasiyo na tija ndo wamekazania..
   
 7. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #7
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dawa ya News Censorship kwa hii karne ya 21 ni rahisi sana watu kuiruka. Andika habari yako na kwa pale pale ofisini kwako rusha kila kitu hewani jf tena bila hata ya wahariri kupunguzia makali yoyote.

  Pili, pindi serikali itakapoanza tu KU-NCHIMBI vyombo vya habari nchini basi naona hatari kubwa kwa NYARAKA NYINGI SANA TENA NYETI serikalini kurundikana mtandaoni kila kukicha sana tu.

  Yote hayo ni kuchota maji kwa kikapu.
   
 8. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Mikataba mibovu ya madini mbona wameshindwa kuchunguza!! hau ndio tuseme nchni haina Kiongozi
   
 9. N

  Ntuya Senior Member

  #9
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hayo ndio matatizo ya kuongozwa na waswahili, I mean watu wa pwani...kazi hawawezi, kuongoza hawawezi...kazi yao majungu na fitina tu. Wote wanabaka demokrasia na uhuru wetu.
   
 10. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Give the dog a bad name and hang it!

  :frusty:
   
 11. B

  Baba Tina Senior Member

  #11
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Serikali ya chama cha mapinduzi siku zote haina rafiki wa kudumu leo wamesahau tido alivyo ibadili tvt kuwa tbc na ikapendwa na wengi. Chattanda nae akae sawasawa.
   
 12. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  What can Nigeria do to live up the promise of its postcolonial dream? First, we will have to find a way to do away to do away with the present system of political godfatherism. This archaic practice allows a relative handful of wealthy men - many of them half-baked, poorly educated thugs - to sponsor their chosen candidates and push them right through to the desired political position, bribing, threatening and, on occasion, murdering any opposition in the process.

  Source: Chinua Achebe, New York, 15 January 2011
   
 13. coby

  coby JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 342
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
 14. coby

  coby JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 342
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Serikali yachunguza mashirika ya BBC, RFI Send to a friend
  Wednesday, 19 January 2011 08:42
  0
  digg

  Mwandishi Wetu
  SERIKALI ya Tanzania inalifanyia uchunguzi shirika la utangazaji la Uingereza (BBC), ikilishuku shirika hilo la Serikali ya Uingereza kwamba linafanya shughuli za uchochezi nchini. Halikadhalika, Serikali pia inafuatilia kwa karibu nyendo za Radio ya Kimataifa ya Ufaransa (Radio France International, RFI), ili kubaini iwapo hatua yake ya kuanzisha Idhaa yake ya Kiswahili inayotangazia kutoka jijini Dar es Salaam haina ajenda ya siri ndani yake.

  Kitengo cha BBC kinachotiliwa shaka na Serikali ni kile cha mfuko wa misaada wa matangazo yake ya kimataifa, yaani BBC World Service Trust (BBCWST), ambacho mapema mwaka jana kiliingia mkataba wa kulisaidia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), kwa mafunzo na vifaa. Mfuko huo wa misaada ya BBC hivi sasa unafanya kazi katika nchi nyingi duniani hasa zile zinazoendelea zikiwemo nchi kadhaa za kiafrika kwa kutumia fedha wanazozipata kutoka kwa wahisani wakisadia kuimarisha utangazaji wa kisasa.

  Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa mkataba wa baina ya TBC na BBCWST ni wa miaka mitano na unafadhiliwa na fedha kutoka Shirika la Kimataifa la Misaada ya Maendeleo la Uingereza (DFID). Nchi nyingine za Afrika zenye mkataba kama huo ni Angola na Siera Leone. Hatua ya kuchunguza ushirikiano huo wa BBCWST na TBC umo kwenye maelekezo ya barua ulizoandikiwa uongozi wa juu wa TBC, mwezi Novemba, 2010.

  Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo katika moja ya barua ya maelekezo yake, alimtaka Mwenyekiti wa Bodi ya TBC, Wilfred Nyachia kumpa maelezo ya kina kuhusu mikataba ya mashirika hayo.

  Mmoja wa maofisa waandamizi katika wizara ya Habari, Vijana, na Michezo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema kumekuwepo na wasiwasi serikalini ya kwamba BBCWST limehusika katika kuifanya TBC itangaze matukio yaliyoikera wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka wa jana.

  Kadhalika kumekuwepo na hisia miongoni mwa watu kwamba matangazo ya uchaguzi ya TBC ndiyo yaliyoifanya Serikali iamue kutomuongezea mkataba mwingine aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Tido Mhando.

  Mhando hakuongezewa mkataba na Serikali licha ya tathimini isyo rasmi ya wadau wa habari nchini kuonyeha kuwa chini ya uongozi wake shirika hilo limeweza kufanya kazi yake bila kuegema upande wowote hasa wakati wa uchaguzi, taarifa ambayo pia imo kwenye ripoti mbalimbali za waangalizi wa kimataifa na kitaifa wa uchaguzi huo. Hata hivyo, akihutubia maafisa wa habari wa wizara mbalimbali mjini Mbeya mwezi uliopita, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, na Michezo, Seth Kamuhanda alisema Serikali ilikuwa ikiyafanyia uchunguzi mashirika ya habari ya kimataifa ambayo yamekuwa yakiendesha ama kutangaza mambo ya uchochezi.

  Radio ya RFI inayomilikiwa na Serikali ya Ufaransa, ilianza kutangaza matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili kupitia radio ya TBC FM katikati ya mwaka uliopita lengo likiwa ni kusaidia kusambaza lugha ya Kiswahili kwenye nchi nyingine za kiafrika ambako radio hiyo husikika. Maafisa kadhaa wa Serikali walihudhuria sherehe za uziinduzi wa kituo hicho mwezi Septemba mwaka jana katika hafla iliyofanyika katika ofisi za ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam. Baada ya maelekezo kutoka kwa Luhanjo, uchunguzi wa Mwananchi umegundua kuwepo kwa vikao mfululizo karibu kwa mwezi mmoja na nusu sasa kuhusu suala hilo, ambavyo vinawahusisha wajumbe wa kamati mbalimbali za bodi ya TBC.

  Mwenyekiti wa Bodi ya TBC Wilfred Nyachia, pamoja na kulijadili kwa kirefu suala hilo kwenye kikao kamili cha bodi kilichofanyika Desemba 21 mwaka 2010, pia amekuwa na mfulilizo wa vikao vingine. Wiki mbili zilizopita Nyachia alizungumza na wajumbe wote wa Bodi yake mmoja, mmoja, ana kwa ana na mapema wiki iliyopita, Mwenyekiti huyo akiwa pamoja na baadhi ya wajumbe wa bodi walikutana na viongozi wa BBCWST na RFI na baadaye wakafanya mazungumzo na baadhi ya viongozi waandamizi wa TBC. Wajumbe wengine wa bodi waliokuwepo kwenye vikao hivyo ni pamoja na Balozi Ben Mosses, Profesa Henry Mgombello na Kiongozi wa idara moja nyeti ya Serikali.

  Nyachia alipoulizwa kuhusu taarifa hizo alailiambia gazeti hili kuwa hana habari za kuwepo kwa hali hiyo, hajui lolote na wala hajaambiwa. Nyachia alisema katika bodi hiyo ya TBC yeye ni mwenyekiti wa vikao tu na si mtendaji hivyo, hilo linaweza kuwepo na yeye asijue na si ajabu. "Sina habari ya mambo hayo, kama yapo unajua siku hizi mambo si kama zamani hakuna 'executive chairman' (Mwenyekiti mtendaji) enzi za mwalimu kama walivyokuwa wakina Mwaikambo NBC," alisema Nyachia.

  Aliongeza,"Mimi ni mwenyekiti wa vikao, si executive, inawezekana lipo, lakini mimi sijui hilo." Mjumbe mmoja wa bodi ya TBC ambaye naye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema baadhi yao hawaelewi tatizo hasa ni nini. "Ni nani ambaye hafahamu umahiri wa BBC kwenye shughuli za utangazaji, na ni nani ambaye hangependa wafanyakazi wake wapatiwe mafunzo na BBC?", alihoji mjumbe huyo. Aliongeza, "Kama kuna kitu kingine kizuri ambacho Tido ameifanyia TBC wakati wa uongozi wake basi ni ushirikiano huu aliouunda na mwajiri wake huyo wa zamani yaani BBC".  Imefahamika ya kwamba uchunguzi wote huo umefanywa kwa nguvu, baada ya kumalizika kwa mkataba wa Tido, huku taarifa nyingine zikidai kwamba Mkurugenzi Mkuu huyo wa zamani wa TBC ambaye anatajwa kuwa mhusika mkuu katika suala hilo huku alihusishwa katika mchakato unaoendelea hivi sasa. Baadhi ya wafanyakazi wa TBC waliozungumza na Mwananchi kuhusu hali ya TBC kwa sasa, walisema wasiwasi mkubwa uliopo ni muelekeo mzima wa hali ya uongozi wa shirika hilo.

  Walisema awali hali ya shirika ilikuwa imeanza kupata mwelekeo mzuri unaoeleweka, lakini sasa haifahamiki ni nani mwenye kufanya uamuzi kuhusu shirika hilo la umma ambalo miaka mitatu tu iliyopita ilifanya sherehe kubwa ya uzinduzi, kutoka kuwa taasisi ya Serikali na kuwa shirika kamili la umma la Utangazaji, mgeni rasmi akiwa Rais Jakaya Kikwete. Kwenye hotuba yake ya uzinduzi huo, Rais Kikwete alisema mabadiliko hayo maana yake ni kuwa kuanzia wakati huo TBC ni shirika la utangazaji la umma wa Watanzania wote, litakaliokuwa na uamuzi wake wenyewe na hasa katika masuala ya uandishi wa habari kwa kuzingatia misingi ya weledi na linalotarajiwa katika muda usio mrefu kujitegemea wenyewe kimapato.

  "Lakini sasa tunaona mambo yanakwenda kinyume na hayo, labda Rais pekee ndiye aliyejua ni nini maana ya mabadiliko aliyoyafanya maana kwa sasa amri nyingi zinatokea wizarani," waliongeza, huku wakitoa mfano wa kipindi maalum cha ghasia za hivi karibuni zilizotokea mkoani Arusha kilichorushwa hapo mwishoni mwa wiki. Uchunguzi unaonyesha kwamba kwamba kipindi hicho kilisimamiwa na mkurugenzi wa idara nyeti ya Serikali aliyewataka kutumia vifaa vya shirika hilo kukiandaa kisha kutangazwa siku ya Jumamosi na Jumapili na TBC1 pamoja na TBC Taifa.

  Tayari kipindi hicho kimezua mjadala mkubwa miongoni mwa wananchi, huku wataalamu wa mambo ya habari wakisema haikuwa sahihi kutangazwa kipindi kilicholalia upande mmoja tu na kwamba kiweledi idara ya Polisi ingefanya mkutano na vyombo vyote vya habari na kutoa picha zote walizotaka kuonyeshea utetezi wao kuhusu tukio hili. Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi wa TBC, Joe Rugarabamu alipoulizwa alisema kurushwa kwa kipindi hicho ni matakwa ya polisi na kwamba walilipia kipindi hicho.

  "Ile ni kama baada ya tukio upande mmoja umetoa maelezo yao nawe umekwenda kuwahoji polisi, nao wameeleza upande mmoja unaowahusu wao, walitaka kitoke na wamelipia," alisema Rugarabamu. Alipotakiwa kueleza wamelipia kiasi gani cha fedha, Rugarabamu alisema, "Siwezi kusema kwa sasa kwani nipo nje ya ofisi". Alipotakiwa kuzungumzia hatua hiyo ya Serikali kuwachunguza na kutaka kuwafukuza nchini, mkurugenzi wa RFI nchini, Victor Robert Wile alisema hawaweze kukurupuka na kulizungumzia hilo hadi watakapopata taarifa kamili juu ya kuwepo kwa mkakati huo wa Serikali.

  "Hatuwezi kulizungumzia hilo, sisi tuna msemaji wetu, tukipata hilo kwa undani tutazungumzia, lakini sasa hatuwezi kukurupuka," alisema Victor Robert Wile. Hivi karibuni, wakati wa sherehe za Mapinduzi Zanzibar, kwa kuzingatia mabadiliko mazuri yaliyotokea tangu kuanzishwa kwa TBC, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar nayo ilitangaza kuanzisha kwa Shirika lake la Utangazaji la Zanzibar, kwa kuziunganisha Sauti ya Tanzania Zanzibar na Televisheni Zanzibar.
   
 15. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,780
  Likes Received: 579
  Trophy Points: 280
  usichokijua ni kama usiku wa giza, acheni ikulu(kama kweli) wafanye kazi ya uchunguzi TBC palioza na kama wangemwongezea Mkataba TIDO nina uhakika ingemfia Mikononi, unakataa kuidhinisha hata ununuzi wa spare za Mitambo na hatimae mitambo kufanya kazi chini ya kiwango

  Nasikia Mkataba wa wachina kuweka Mitambo ya DIGITAL ni miaka 25 ndipo tutaachiwa sasa si itakuwa mibovu baada ya miaka hiyo?
   
 16. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Real Rumanyika ... I like your comment bro..
   
 17. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #17
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Another Zimbabwe in line!
   
 18. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Tido ni mwanataaluma wa habari, kwanini akae kimya anapodhalilishwa hivi?...mi nilidhani baada ya kuwekwa kushoto ingekuwa nafasi yake sasa kuchambua kwa undani na kwa uhuru hali halisi ya tasnia ya habari nchini, maingilio ya watawala na wanasiasa kwenye taaluma hii, na nafasi ya Tanzania kwenye Dunia ya Teknolojia kwa kuzingatia mikono hii iliyofichama...
  Vinginevyo huenda kwa kukaa kwake kimya akawa anaogopa aftermath ya alichokitenda...You never know with a woman!
   
 19. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #19
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  East African MAFIA (CCM) at work!!!!!
   
 20. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #20
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Huyu atakuwa SALVA ama ZOMBA akiwa humu JF
   
Loading...