Ikulu yaanza kumwandama Tido Mhando................

Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo katika moja ya barua ya maelekezo yake, alimtaka Mwenyekiti wa Bodi ya TBC, Wilfred Nyachia kumpa maelezo ya kina kuhusu mikataba ya mashirika hayo.

Business as usual. Kuhangaika na dagaa wakati mapapa na manyangumi yanadunda kiuraiiiiini. Huyu mzee anastaafu lini?
 
Gazeti la Mwananchi linaripoti ya kuwa Mkurugenzi mstaafu wa TBC Bw. Tido Mhando mikataba aliyosaini na BBC na RFI imeanza kuchunguzwa kwa kile kinachodaiwa ni kuona kama masilahi ya taifa yalizingatiwa................................

Swali ninalojiuliza ni kuwa hivi dhambi za Tido, kama zipo, CCM ilianza kuziona baada ya kwisha kwa uchaguzi huu tu?

Hivi kweli BBC Idhaa ya Kiswahili na hiyo Radio ya ufaransa kweli kweli zimeleta uchochezi upi kwa kusema ukweli?

Huyu JK kama kazi imemshinda si ajiuzulu tu asisubiri Bunge likamfukuza kazi................

habari nzuri lakini umekosa mambo machache. Tido Mhando sio mstaafu. Mtu anayefanyakazi kwa mkataba
sio pensionable staff.
kuhusu dhambi kubwa sio dhambi alizofanya Tido bali CCM wamgundua nua vyombo vy habri ni muhimu katika kulinda uchafu wao kwa hiyo hawawezi kuacha viwe huru kama walivyotaka. Wanajua itawacost kwa madhambi yao. So lazima wafanye kila linawelowezekana kuturudisha kwenye ule mfumo wa RTD.
 
Sasa wachawi wa CCM wamekwisha bado Makamba ambaye anajibu ovyo Mchawi huyu wa uchaguzi wa kuwaaangusha Vigogo wamemuonea sana mchawi wa CCM ni makamba, Edward L.N na NM pamoja na kiongozi wetu aliyewatukana wafanyakazi na walimu. CCM imechokwa sana , mie sitaki kuajiliwa na serikali kwa kuwa siwezi kuvumilia kumweleza mabaya wafanyayo CCm kwa kuogopa kupoteza ajira. CCm wajanja pale Arusha waliwachukua vijana wapya kutoka CCP wanaojaribu kama bunduki kweli inaweza kuua na kuwafundisha jinsi ya kujilazimisha asila kama ukitumwa na bosi wako ndio maana risasi walizitoa kama mjugu, chukulia mwanza ambapo CCP Moshi iko mbali hamna kitu kama hicho, mchawi mwingine ni police ambayo ilishindwa kunyanyasa raia wakati wa kupiga kura mpaka Boss kijana Mzee wa majivuno A.K.A. Bitozi Nyangema Masha alishindwa vibaya kwa kuwa police wenye akili waliwaachia Raia watimize haki yao ya msingi, baaday ya hapo AGP Mwema alifanya mabadiliko ya haraka kuwabadilisha makamanda wote wa Mikoa na Wilaya alipoulizwa alisema ni mabadiliko ya kawaida tu. Mwanahabari wa Zamani wa RAI ya Rosta mlamba miguu Rweye ndiye chanzo cha kufukuzwa au kutoongezea mikataba ya Mhando, huyu ana hulka mbaya ya kujikomba , eti msemaji wa IKULU au mchochezi wa IKULU ndio maana alikimbiwa na Mke(samahani hasira zimezidi)
 
Huu ni uongozi wa visa na visasi. Baada ya uchaguzi wanamuona kila mtu mchawi, walianza kumpeleka Basilio Matei yule aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Arusha makao makuu (au benchi ) ili asome magazeiti,. Huyu aliwakatalia kushiriki wizi wa kura. Tido akafuatia na wengine wako njiani wakae mkao wa kura. Huyu bwana hana legitimacy hapo ikulu nafsi yake inamsuta anatapatapa kama kichaa.
 
Huko serikalini kwa sasa kunanuka/kumeoza... ni uchafu mtupu unaoendela huko... Kuna mama amekuja hapa ofsn anaomba msaada (mtoto wa dadake amefaulu anatakiwa kwenda shule na yeye hana uwezo kwa kuwa mwenyewe ni mjane) huyo mtoto wa dadake naye wazazi wake wote ni marehemu so huwa anakaa naye.

Akashauriwa na baadhi ya watu hapa ofisini aende ofisi ya raisi kuna kitengo cha misaada kama hiyo... Mama ametuambia alishaenda zaidi ya mara 10.. Yaani kwanza ukibahatika kusikilizwa kwanza unaulizwa kama ulipiga kura na kama ulipiga ulimchagua nani!!!!!!!!!!! VERE BAD.. WE'RE FINISH!!!!!!!
 
looh kumbe investigation juu ya Tido ilianza 2011??

Sasa hizi Tuhuma za visa na visasi zinatoka Wapi??

kwanini upinzani wanapenda kuishi kwa kutegemea uzushi na ulaghai??
 
Mafisadi pale Ikulu wakiongozwa na JK hawapo tayari kabisa ukweli juu ya tuhuma kebekebe zinazowakabili umma wa watanzania wazijue kwa hiyo wanatafuta mazingira ya kuanza news blackout and censorship...................
Miongoni mwa wanaosifu utawala wa jk kwa sasa.
 
Hayo ndio matatizo ya kuongozwa na waswahili, I mean watu wa pwani...kazi hawawezi, kuongoza hawawezi...kazi yao majungu na fitina tu. Wote wanabaka demokrasia na uhuru wetu.
Leo unasema nini kuhusu jk?
 
Kama alivyokimbia Kenya kujinusuru na mkono wa mtukutu rais Daniel Arap Moi mwanzoni mwa miaka ya 90!!

Tido anajuuuta kukubali kuitema BBC na kuja kufanya kazi katika serikali ya mkwere.

Serikali iliyojaa visasi na chuki huku tija ya utendaji kazi ikiwa zero.
Duuh,saiz mbona huyu mkwere anasifiwa?
 
Huko serikalini kwa sasa kunanuka/kumeoza... ni uchafu mtupu unaoendela huko... Kuna mama amekuja hapa ofsn anaomba msaada (mtoto wa dadake amefaulu anatakiwa kwenda shule na yeye hana uwezo kwa kuwa mwenyewe ni mjane) huyo mtoto wa dadake naye wazazi wake wote ni marehemu so huwa anakaa naye.

Akashauriwa na baadhi ya watu hapa ofisini aende ofisi ya raisi kuna kitengo cha misaada kama hiyo... Mama ametuambia alishaenda zaidi ya mara 10.. Yaani kwanza ukibahatika kusikilizwa kwanza unaulizwa kama ulipiga kura na kama ulipiga ulimchagua nani!!!!!!!!!!! VERE BAD.. WE'RE FINISH!!!!!!!
Jk alikua kiongozi bora sana.
 
Back
Top Bottom