Ikulu watakubali kunipa kibarua nilichoomba?

Kitu kikubwa ambacho Watanzania hatuwezi kukikubali ni kwamba hatujui tulikotoka,tuliko na tuendako, na hivyo basi hatujui tumejikwaa wapi,tumeangukia wapi na tutainukia wapi.
Tukijaribu kuangalia awamu nne ambazo zimetawala nchi hii,ni awamu ya JAKAYA KIKWETE ndiyo ambayo amekumbana na CHALLENGE nyingi na akaweza (kama sio kujaribu) kuzikabili kiungwana.
Nikianza na awamu ya MWALIMU,ambayo ilikuwa awamu ya kwanza,Yeye alikuwa na uzalendo wa kweli ambao kwa viwango vya binadamu wa sasa huwezi kuvikuta,aliishi maisha yale anayoyahubiri na aliamini katika haki ,ukweli,uzalendo na uchapakazi.na kupitia hayo,aliweza kujenga misingi imara sana katika nchi changa sana.Misingi ambayo Wabenzi wanajaribu kuibomoa lakini wameshindwa ingawa ki ukweli wanaitikisa.Aliiacha nchi ikiwa ina uchumi mzuri,utawala bora na kiwango cha chini kabisa cha rushwa kuliko kipindi chohote cha tawala nyingine.Nchi iliendeshwa kwa dira na mipango inayotekelezeka.
Sheikh,Alhaj ALLY HASSAN MWINYI,hakuwa na vission wala mission.alijaribu kuiga kama alivyotawala Mwalimu bila kujua mwalimu hakuwa binadamu wa kawaida katika zama hizi.mwishowe Mwinyi alivyoona hawezi akaamua kuacha Taifa lijipeleke vile litakavyo.Na hapo ndipo wale chui waliojivika ngozi ya kondoo ili kumuhadaa Kambarage,wakaamua kuvua ngozi zao na kuonyesha makucha yao.Na huu ndio ulikuwa mwanzo wa mparaganyiko tunaoushuhudia sasa.Uungwana na kutokuwa mkali katika mambo ya msingi akiwa kama Raisi kulisababishwa kuanza kujengeka kwa tabaka la mafisadi ambalo lilikuwa linaomba kila siku Mwalimu Kambarage aondoke duniani.
Ujio wa BEN WILLY MKAPA na kifo cha mwalimu Nyerere,kilifungua rasmi milango na kuondoa hofu toka kwa wale waliokuwa wakiitamani nafasi hiyo.Wakisaidiwa na Mkapa mwenyewe kama fisadi namba moja na mkuu wa nchi,walifanya kile ambacho kila mmoja wetu anakifahamu.Na kibaya za ni kitendo cha kushawishi na kufanikiwa kuliingiza Jeshi la wananchi wa tanzania(JWTZ) kushiriki katika uovu huo(rejea report ya mwanakijiji juu ya Meremeta).Jeshi lililokuwa likisifika kwa uzalendo,nidhamu na uchapakazi,likageuzwa kuwa ni tawi la mafisadi kufanya ufisadi wao.
Kama ni kujikwaa,basi hapo ndipo Nchi yetu ilipojikwaa,na lilikuwa ni pigokubwa kiasi ambacho,kuja kujipanga sawa itachukua muda mrefu sana ama tuwe tayari kujitolea damu zetu na wapendwa wetu kwa ajili ya kuiokoa nchi yetu.Ben Mkapa ana deni kubwa kwa nchi hii kiasi ambacho hata mbinguni hataweza kulilipa.Ule uchumi uliokuwa haujatengemaa vizuri tangu kipindi cha mwalimu,ukaja kusambaratika kipindi cha Mkapa,rasilimali zilizokuwa zikimilikiwa na serikali zikagawanywa katika kipindi hichohicho(naye akajigawanyia),Hata maliasili ambazo Mwalimu alisema hazitakuja oza hivyo zinaweza kusubiri,nazo ziligawanywa.
Uzalendo,undugu baina ya watanzania, na mapenzi kwa nchi vilifia hapo.na Mkapa alijua hilo na alifanya kwa makusudi.Mbaya zaidi alikuwa anajua nguvu ya KIKWETE katika CCM,na hivyo palikuwa hakuna uwezekano wa kumzuia kikwete kuchukua madaraka pindi muda ukifika.Ukijumlisha na uzalendo pamoja na record ya Jakaya katika utumishi wake,waliamua kutengeneza mazingira ambayo yatamuweka Jakaya katika nafasi ambayo hata yeye KIKWETE ataguswa endapo atataka kuwashuhulikia wahalifu.
Kikwete hakujua mkakati wa wanamtandao,mkakati wakum beba kikwete kwa kutumia fedha zao kutokana na urafiki baina yao.lakini kumbe wale vinara wa mtandao hawakuwa tayari kutoa fedha zao mfukoni bali ni kuunda makampuni hewa kwa maelekezo ya Mkapa ili fedha hizo zitumike kupigia kampeni Kikwete.Kitanzi kikawa kimeshaingia shingoni mwa Jakaya na kinamtesa hadi LEO.
Ninachomsikitikia ndugu yangu Kikwete ni kwamba,uzalendo anao,dhamira anayo na uwezo anao ila hana moyo wa kijasiri kupambana na hali hiyo au kuwatosa marafiki zake waliomfikisha hapo.Na hilo ndio anguko la raisi wetu.
Lakini ukiangalia sana,Jakaya hakuna kubwa alilolifanya la kumlamu zaidi ya kushindwa kuwachukulia hatua wahalifu wa serikali ya awamu ya tatu.Na huenda hilo ndio lilanalomuondolea sifa ya kuwa kiongozi bora na makini na hivyo kusababisha umaarufu wake uliomuingiza madarakani kwa kishindo kuporomoka.
Binafsi nayatazama mambo katika mtazamo huo,kuwa, tuliyumba awamu ya pili,tukajikwaa awamu ya tatu na sasa tumeanguka katika awamu ya nne.SASA JE! tujilaumu tulipojikwaa au tulipoangukia!!!
jibu kichwani mwako,
HATA UKIPEWA KAZI YA USHAURI KWA RAISI HUTAWEZA KUBADILISHA CHOCHOTE,Kwani raisi kama taasisi alishavikwa kitanzi ambacho asipokaka kimya,maadui wanavuta na kunyonga.hivyo usipoangalia utajikuta kazi yako ya ushauri utaona haithaminiwi nawe utageuka kuwa kama wao.

nawasilisha
 
MWKJJ, Samaki uanza kuoza kuanzia... System yote needs revamption!
 
Kuna matatu nayoweza kuchangia:-
1. Si kweli kwamba hajui what is right for his fellow Tanzanians
2. Unapopewa ushauri hulazimishwi kuufuata na
3. Hana hata hiyo nia ya kufanya chochote. kwangu yule ni failure 100%

Kwa kumalizia tu ni zile stori za pupils ku-count saa ngapi zimebaki kwenda break au kutoka shule regardless how much she/he gained from his/her attendance.
 
mwisho kabisa unatakiwa kumshauri hasirudi tena hiyo sehemu takatifu (Ikulu) Tutamwona kawajibika yeye binafsi na kufanya jambo la kiungwana
 
mimi nisingependa hii kazi upewe kwa sasa...JK hashauriki...kama kusoma hajui lakini hata picha haoni???? JK ni mnafiki na inawezekana anakubali kashindwa moyoni mwake....tumempatia madaraka, uwezo mkubwa sana lakini kwanini hawezi kuutumia kwa maslahi ya taifa...anachoremba ni nini??? Je hakushauriwa kwamba kuongoza nchi ni kazi kubwa......??
Mwanakijiji mimi naona kazi unayoifanya tayari inatosha...JK yote haya anayajua lakini hana uwezo...amejiweka pabaya...amezungukwa na wadhamini,mashemeji,washkaji ambao hawezi kuwaambia lolote...kama ni ushauri ushatoa wakutosha na umeonyesha muongozo wakati wote....kuomba kazi kwa JK si jambo jema....harakati ulizoanzisha nje zinatosha kuliko ukiingia kule ndani hatutajua umelishwa nini??? tupigane nje mpaka wafungue mlango tuwatoe tuingie wenyewe.....
 

Notradammus,

Umeweka analysis nzuri sana hapo juu. Lakini hapo kny kipengele cha JK kukaa kimya ukumbuke Muomba kazi ikulu (MM) anasema katika hali kama hiyo angemshauri atumia kanuni ya LIWALO NA LIWE laiti kama atakubali kutumia kanuni hii, wananchi watakuwa nyuma yake....na hii nafikiri ni siraha nzuri sana kwa JK.....anapendwa na wengi hasa raia wa kawaida!

So to me kama JK kwa nafasi yake anaweza akafanya lolote lile kama raisi na hasa kwa manufaa ya nchi na akapata support ya Bunge na wananchi kwa ujumla.......!
 
KAzi hatokupa, msome Jenerali Ulimwengu:

 
Kikwete yuko kama kwenye puto kubwa la aina fulani. Puto hilo linaenda naye mahali popote na wakati wowote na ndilo analitegemea kupata taarifa. Kwa miaka michache sasa nimefikia hitimisho kuwa ni kwa ajili manufaa ya puto hilo Kikwete hapewi taarifa sahihi, anafichwa mambo na anakuwa mtu wa mwisho kujua.

Nakumbuka wakati wa sakata la vijana Ukraine siku nimezungumza naye na kumuelezea alishangaa sana na hakuwa anajua na akabakia kusema "kama (wizara) wameshindwa wangeniambia" ili waone jinsi gani ya kushughulikia. Matokeo yake wale Puto wakawa wanatuma ujumbe kwa mtu yeyote ambaye alitaka kuwasaidia wale vijana kuwa akifanya hivyo atakuwa anaenda kinyume na Rais.

Ni yale yale kwenye masuala ya Mapanki ambapo kuna mtu alimwambia kuwa watanzania hawali mapanki na yeye akasimama kutamka hivyo hivyo; ni vile vile aliposimama na kusema kampuni ya BAE Systems (ya rada) inamilikiwa na serikali ya Uingereza na hivyo tutaidai Uingereza fedha yetu tuliyolipa ziada ya bei halisi; Na tumeliona tena kwenye suala la uchumi ambapo yeye aliwahakikishia wananachi kuwa uchumi wetu hautaathirika kwa kiasi kikubwa kwani hatujawa connected sana katika uchumi wa kimataifa halafu miezi michache baadaye anasema tumeathirika kwa sababu tuko connected katika uchumi huo wa kimataifa.

Yote ni dalili siyo ya mtu ambaye anaficha ukweli bali mtu ambaye hajui. Rais ni mtu anayetegemea Washauri wake sana kuliko kitu kingine na anatakiwa awe na washauri ambao watamuambia ukweli, watakaopingana kwa hoja na kumpatia taarifa sahihi (ziwe nzuri au mbaya) wakati wote ili kumsaidia kufanya maamuzi sahihi.

Bahati mbaya Rais wetu amezungukwa na puto ambalo linalenga kumpa taarifa zinazoonekana nzuri. Na ninaamini wakati mwingine wanampa taarifa za kumpotosha kwa makusudi. Ndio maana sitoshangaa hao washauri ndio wamemuambia kuwa hahusiki na Richmond na sitoshangaa hawakumuambia kabisa na hajui kuna taarifa imetolewa kuhusu yeye na Richmond.

Mara nyingi utaona kuwa Kikwete yuko ziarani mara nyingi sana na karibu Jumatano nyingi (siku ambazo magazeti mengi yanaandika habari za kisiasa) Kikwete anakuwa kwenye kaziara fulani nje ya nchi au mikoani. Na akirudi wanamfanya we busy sana kiasi kwamba hana muda wa kupata taarifa za ndani.

Ndio maana licha ya kuwa kuna tatizo la njaa linalokuja Kikwete yawezekana hajui kabisa hadi siku washauri watakapomuambia it is time to beg for more aid na yeye atatokea na kuzungumza na wafadhili kwa ajili ya msaada wa chakula.
 
Wangekuwa wanaisikiliza JF wangeongoza vizuri lakini sijui huwa hawaoni wanachoshauriwa maana kila uchao yanajirudia,haya 2010 hiyooooooooooooo.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu nitarudia kusema kwamba JK sii mjinga kama unavyofikiria. Yote uloandika JK alikuwa na taarifa isipokuwa yeye ndio kakupiga goli..Jk mtoto wa mjini na mara zote kila jambo la kufumaniza linapoingizwa kwake ni lazima ijefanye halijui hata kama analijua fika, ili apate kujua wewe unaelewa nini..ukimtega kisogo tu anakung'onga!

Ni sawa na askari wanapokuja mlangoni kwako wakakuuliza kama wewe ni Mwanakijiji, jibu rahisi litakuwa sii mimi kwani Mwanakijiji kafanya nini?..ndio JK huyo babuu.

Sakata la Ukraine alilijua fika na kusema kweli kwake yeye kama rais aliliona dogo sana ambalo lingeshughulikiwa na waziri sio yeye..Na kwa lugha ya mjini tunasema matatizo ya wale vijana wakiwa mtoni huwezi kulinganisha na matattizo alokuwa akiletewa kila siku kuhusu wananchi wasiokuwa na maji, umeme na upungufu wa chakula nchini kutokana na ukame..After all yule ulokuwa ukimtaja -LOWASSA kumbuka kuwa wakati huo huyu mkulu ndio alikuwa kipenzi cha JK na akiendesha nchi ya wajinga.. JK akitesa na honeymoon ya Urais!
Swala la Mapanki, sii kweli JK hakufahamu kitu, laa sivyo asingefunga kiwanda cha wahindi walioshiriki ktk kutengeneza ile sinema na hata kuipiga marufuku kuonyeshwa nchini..iweje aipige marufuku wakati hajui kilichokuwemo ktk sinema ile!
Mzee wangu hivi kweli wewe unaamini Warusi waliweza kuingiza silaha nchini rais wa nchi hafahamu?.. tena ndege yenyewe ikilindwa na askari wetu usiku kucha.. sidhani kama Uwanja wa Taifa kuna ndege private zinalindwa hivyo.

Swala la BAE, hivi nikuulize wewe.. kama ungekuwa rais na unajua kilichofanyika na swali kama hilo limeulizwa wakati unataka kuwalinda wote waliohusika utasema kitu gani?.. ni kanyanga gani utawavika wakuondolee usiku!.. Ndio JK huyo mkuu wangu.

Kwa hiyo, JK anakwenda na mahesabu yake, ndio maana akaitwa muungwana kwa sababu anayajua madhambi yote lakini ytupo radhi atundikwe yeye lawama lakini watu wake waendelee kupeta..
Je, ni makosa anayofanya?.. inategemea wewe umesimama upande gani..kwa sababu Politics ni mchezo mchafu sana. Msikilize mzee Malecela kama wewe sii mwana CCM utachoka naye na sii kwamba hafahamu rafu zinazochezwa.

Kifupi kosa kubwa analofanya kama rais ni pale anapoachia watu binafsi wafanyabiashara kina Rostam na Lowassa kucheza siasa..Leo hii kuna mawaziri wakiwa namatatizo kiuongozi badala ya kwenda kwa rais wanakwenda kuwaona kina Lowassa hapo ndipo utaona JK kapoteza nguvu ya rais na binafsi sielewi strategy ipi anayotumia kama sii kujitia kitanzi yeye mwenyewe..unless anayo plan B kusubiuri uchaguzi ndio kesi zote zifumke, watu watiwe ndani hadi baada ya uchaguzi..

Kila siku hawa mafisadi wanazidi kupanda umaarufu na hakika uchaguzi ujao utakuwa baina ya JK na kundi la Lowassa! It won't suprise me if 2010, hawatajaribu kumwondoa (an atempt for his life!).
Waswahili wanasema Mjqnja ni yule anayejifanya hajui kumbe anajua, na mjinga ni yule anayejifanya kujua kumbe hajui!.
 
Last edited:
[/QUOTE]
Nakuhakikishia kuwa, bora amekaa kimyaaa kuliko kufikiria hatua dhidi ya wachezaji wenzake kwani mfumo wa CCM, huyo JK ni captain tu wa team nzima sii owner wala team coach...

Na akijaribu tu kufungua mdomo wake bila kutumia usanii atakombwa hadi yeye.......
 

Hivi ni lini anatarajia kuachia hiyo ofisi? sooner or later?
 
Mzee MJJ hata ukipata kibarua cha kumshauri JK usitegemee atafuata ushauri wako kwa sababu hawezi kufuata ushauri wa kumwangamiza kutokana na madudu yote yaliyofanyika ya EPA,RICHMOND,MEREMETA,IPTL n.k. yeye pia ni mhusika mkuu, hivyo basi ushauri wangu kwa watanzania ni kupigania mabadiliko ya katiba ndilo suluhisho lililobaki kwetu na vizazi vijavyo.
 
Naam nimewapata.mwenyehoja kasema kikwete hana washauri wazalendo. wachangiaji wakaongezea haambiliki kwamba washauri anawapeleka puta,wengine kwamba he was the key player kwenye ufisadi kuchukuwa hatua ni kujifunga goli.wengine ni kwamba si mzalendo hana nia.wengine ni kwamba hana mamlaka ni coach (morinyo) na siyo abramovich.wengine ni kwamba tumpe tena nafasi KWA SHARTI MOJA, kipindi kijacho asitafute ufadhili kutoka kwa mafisadi.Sasa naomba ushauri uenda mambo yote ni sahihi.JE WENYE NCHI TUFANYE LIPI JEMA
 
Cheche imetema cheche baada ya cheche hizo sioni hatua za serikali kuzuia moto kwani mwazo wa moto ni cheche.Imekua kawaida kwa serikali na washauri wa Rais kukimbilia kumlinda rais katika mambo ya kipumbavu lakini ktk hili naona ni maji ya shingo bado hawana au bado watunga hadithi kuhusu swala hili.Shukurani kwa kazi yenu.Inabidi wabunge waombe majibu kuhusiana na kashfa hii.MUNGU USICHOKE KUIBARIKI TANZANA!
 
Mkuu wazo na ushauri mzuri lakini ulikuutuma siko.Washauri wa Rais hawako Ikulu hao walipo Ikulu ni vipaza sauti.Katika ushauri waka unautuma kwa mtengenezaji wa kipaza sauti ambae hawajibiki kwa vyoyote kwa kauli inayotoka katika kipaza sauti.Ushauri inabidi kuutuma kwa Rostam Aziz na mafisadi hawa dio marais wetu JK ni Rais kivuli.MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Hivi kweli JK kama yeye hana akili, utashi, udadisi, ung'amuzi, utambuzi na wala hashtuki, hasomi alama, nyakati au hawafahamu vizuri hao wanaomzunguka kuanzia mkewe, wanawe, ndugu, maswahiba, marafiki,....
URAIS umempunguzia uwezo wa kufikiri, kuamua, kutenda....
SIDHANI. Nchi inasonga mbele jamani. Baadhi yetu hatutaki kuyaona hata yale mazuri machache anayoyafanya! Tunataka afanye/aamue tunavyotaka sisi ambao si "MARAIS"!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…