Kama ningepata fursa leo ya kuonana na Rais ningemwambia yafuatayo

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,601
Kama siku ya leo ningepata bahati ya kuonana na Mhe. Rais na kupata fursa ya kuzungumza naye, ningemwambia yafuatayo:

Kwanza, ningemshukuru kwa kutoa ajira nyingi sana kwenye kada ya Afya na Ualimu lakini panatakiwa pawepo na mchakato rasmi ili kuondoa upendeleo. Ningemshauri pawepo hata na "online aptitude test" za kumpima uwezo, ujuzi na utayari wa muombaji kwenye kada husika.

Pili, ningemshauri aanzishe chombo maalumu wa kusikiliza kero na changamoto za Wananchi kwa wizara, idara, taasisi na mamlaka zote za Serikali. Hii itasaidia mashauri, kero na changamoto za Wananchi kufuatiliwa kwa haraka kwa sababu utaratibu wa sasa wa Taasisi husika kusikiliza kero zinazowahusu wao wenyewe inaweza kuwa inachangia taasisi kutowajibika kwa kero hizo ipasavyo.

Tatu, Ningemshauri kupeleka wataalamu wa masuala ya biashara, uwekezaji na ujasiriamali kwenye balozi zetu ili wakasaidie kutangaza fursa zilizopo nchini kwenye maeneo hayo. Hii itasaidia kufanikisha diploma ya uchumi kwa haraka na ufanisi zaidi.

Nne, ningemshauri juu ya uwezekano wa TTCL kuuza bando za internet kwa Bei nafuu. Huduma za internet ndizo zinazovutia watu kutumia mtandao husika. Hivyo itasaidia kuinua mapato kwa taasisi hiyo.

Tano, juu ya suala la hasara la ATCL ningemshauri Mhe.Rais ATCL ifanye kazi na wizara ya maliasili na utalii kwamba Air Tanzania ndio itumike kusafirisha watalii kuja na kurudi. Air Tanzania itoe punguzo maalumu kwa watalii watakaotumia huduma hiyo. Air Tanzania ibebe dhamana nzima ya mtalii ndio iwe na jukumu la kumhakikishia mtalii huduma muhimu kwa utalii wake.

Je, wewe ungemshauri nini?
 
Back
Top Bottom