TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Gazeti la Mwananchi, matoleo ya jana, Jumatano, Oktoba 12 na leo, Alhamisi, Oktoba 13, 2011, limeandika habari zilizodai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alitoa msamaha wa kupunguza adhabu ya kifo iliyowakabili askari polisi wa zamani waliopatikana na hatia ya kumpiga risasi na kumwua kwa makusudi aliyepata kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Luteni Jenerali Imran Kombe Juni 30, 1996.
Gazeti hili limedai kuwa Mheshimiwa Rais Kikwete alitoa msamaha huo kwa kupunguza adhabu ya kifo iliyokuwa inawakabili makonstebo wapelelezi Mataba Matiku na Juma Muswa na kuibadilisha kuwa kifungo cha miaka miwili.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inapenda kufafanua kuwa Mheshimiwa Rais Kikwete hajawahi na hajapata kuhusika hata kidogo kutoa msamaha wa kirais kwa kupunguza adhabu ya wauaji hao wa Luteni Jenerali Kombe tokea kuingia madarakani.Masuala yote yanayohusu polisi hao waliohukumiwa kifo kwa mauaji ya Luteni Jenerali Kombe yalifanyiwa maamuzi kabla ya Rais Kikwete kuingia madarakani Desemba 21, 2005.
Imetolewa na:Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu,DAR ES SALAAM.13 Oktoba, 2011
bibikuku nakuaminia sana mkubwa
Kusainiwa au kutokusainiwa sio hoja, jua kuwa ni taarifa ya ukweli huwa sijawahi kuweka kitu cha kutunga ama hisia hapa jamvini
Makubwa mwenzangu, ishakuwa inji ya matamko.
Mimi naona kama kuna kitu kimejificha nyuma ya huu msamaha.
Kwanini ikulu isitoe maelezo yanayojitosheleza hata kama aliyetoa msamaha ni mkapa. Hakuna shida yoyote so long ni ofisi hiyo hiyo, katiba ni ile ile na sheria ni zile zile, watendaji wakuu ndio wamebadilika.
2+2=4 sio 22..inasemekana hawa mabwana wapo mtaani kitambo tu wala hio adhabu hawakuitumikia,danganya toto
Mr u went too personal that u derail from the typical facts u were to deliver..,next tym,at least try to spam on topic.,actual u intend to teach but eventually u skunked...,the paper cooked the story too systematically that press release was necessary...!Heshima kwenu wakuu!!
kila wakati ninaposoma habari kuhusu utendaji wa "wakoloni weusi" wa Tanzania ninabaki mdomo wazi...
Ningependa kuchukua nafasi hii "kumfundisha" Salvatory Rweyemamu na vibaka wenzake 2 simple rules of mass communication
* Habari iliyokanushwa ni habari iliyotolewa mara mbili i.e. by the time you deny or you rectify any piece of information, you involuntarily participate in its propagation. So kabla ya kukanusha angalia kama ukanushaji wako unasaidia katika kuzima moto au ktk kuuneza in this case I should say you left more questions tha answers!!!!
** unapoziba kiraka( i.e ambiguous information) make sure "dabwada" unalotumia ni la higher quality ukilinganisha na kiraka unachotaka kuziba otherwise it's much more "productive" to leave the kiraka to stay.
You(Mr:Rweyemamu) didn't respect any of the 2 na hii inathibitisha namna ulivyo kilaza. Sasa swali la kujiuliza kama jamaa ni kilaza namna hiyo hao wa chini yake wakoje??? God forbid, I dont wanna even to imagine...
Nyerere alikuwa anapenda kusema kuwa viongozi wabovu( read Kikwete) ni kama mizoga,wana tendency ya kukaribisha kunguru(read wahauri wabovu Salvatory and his likes)....
God bless Tanzania and it's people!!!!
hao jamaa wameachiwa kuja kufanya kazi maalumu!! watch out.
Hata haiingii akilini, kama maamuzi yalifanyika toka mwaka 2005 (chini ya Mkapa) imekuwaje bado wafungwa hao bado walikuwa wamefungwa hadi leo?..
Mr u went too personal that u derail from the typical facts u were to deliver..,next tym,at least try to spam on topic.,actual u intend to teach but eventually u skunked...,the paper cooked the story too systematically that press release was necessary...!
Siasa ni Mchezo Mchafuhao jamaa wameachiwa kuja kufanya kazi maalumu!! watch out.