Ikulu vs Gazeti la Mwananchi: JK akana kuwasamehe waliomuua Lut Jen Kombe

bibikuku

JF-Expert Member
Feb 16, 2011
832
492
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Gazeti la Mwananchi, matoleo ya jana, Jumatano, Oktoba 12 na leo, Alhamisi, Oktoba 13, 2011, limeandika habari zilizodai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alitoa msamaha wa kupunguza adhabu ya kifo iliyowakabili askari polisi wa zamani waliopatikana na hatia ya kumpiga risasi na kumwua kwa makusudi aliyepata kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Luteni Jenerali Imran Kombe Juni 30, 1996.

Gazeti hili limedai kuwa Mheshimiwa Rais Kikwete alitoa msamaha huo kwa kupunguza adhabu ya kifo iliyokuwa inawakabili makonstebo wapelelezi Mataba Matiku na Juma Muswa na kuibadilisha kuwa kifungo cha miaka miwili.

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inapenda kufafanua kuwa Mheshimiwa Rais Kikwete hajawahi na hajapata kuhusika hata kidogo kutoa msamaha wa kirais kwa kupunguza adhabu ya wauaji hao wa Luteni Jenerali Kombe tokea kuingia madarakani.Masuala yote yanayohusu polisi hao waliohukumiwa kifo kwa mauaji ya Luteni Jenerali Kombe yalifanyiwa maamuzi kabla ya Rais Kikwete kuingia madarakani Desemba 21, 2005.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
13 Oktoba, 2011
 

Ngonini

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
2,023
562
Haya sasa kama kawaida ya wazee wa kiduku, wanajibu kama siyo serikali. Kama maamuzi yalifanywa kabla ya JK na kama yalifanywa na Ikulu hiyohiyo kwanini wasitoe ufafanuzi wa swala hilo kuliko kutoa statement fupi tu inayoacha maswali zaidi ?
 

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,177
3,326
Ni suala jepesi sana, tutajua kama hao wafungwa wametoka au laah baada ya kwenda magereza husika kujua kama ni kweli au laaaah. Halafu kwa nini Ikulu isilitake gazeti kukanusha habari hiyo front page badala yake inaishia kukanusha na kutulia tu. Yupi muongo sasa Ikulu au Mwananchi?
 

Bigirita

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
15,866
7,161
Figure it out!!
Ni suala jepesi sana, tutajua kama hao wafungwa wametoka au laah baada ya kwenda magereza husika kujua kama ni kweli au laaaah. Halafu kwa nini Ikulu isilitake gazeti kukanusha habari hiyo front page badala yake inaishia kukanusha na kutulia tu. Yupi muongo sasa Ikulu au Mwananchi?
 

Kwaroz

Member
Aug 30, 2009
55
10
sasa kama maamuzi hayakufanyika wakati huu tatizo ni nini? Ni ikulu ndio ilitoa maamuzi hayo au mnataka kuiweka juu ya mkapa? Kama sio JK iweje watoke mwaka huu kama nipo sahihi? Ilitakiwa watoke kati ya 2006 au 2007 ndio miaka miwili ingekamilika. Au hiyo miaka miwili ilianza kuhesabiwa lini? Jk akubali kosa asisingizie mtu kwa kuwa ni maamuzi ya ikulu na sio mtu. Nawakilisha
 

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,177
3,326
Haya sasa kama kawaida ya wazee wa kiduku, wanajibu kama siyo serikali. Kama maamuzi yalifanywa kabla ya JK na kama yalifanywa na Ikulu hiyohiyo kwanini wasitoe ufafanuzi wa swala hilo kuliko kutoa statement fupi tu inayoacha maswali zaidi ?
Huyu Rweyemamu naona amechoka kazi kabisa, hivi hiyo habari alisaini au alisainiwa?
 

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,938
Ha ha haaaa..............

Tanzania nchi yetu nzuri sana, watu kwa kujitoa tu hawajambo.

Mimi nilitegemea ikulu ingetueleza huo msamaha ulitolewaje kwa kuzingatia katiba, sheria na mamlaka ya rais, lakini kumbe ni yale yale ya kusingizia utawala uliopita!
 

Oxlade-Chamberlain

JF-Expert Member
May 26, 2009
8,635
2,180
Mbona sijaelewa hapa? Kwahio wanamaanisha kwamba Mkapa ndio kawapunguzia adhabu au hawamjui aliyewapunguzia adhabu? Manake hamna sehemu walio kanusha kwamba habari ya kupunguziwa adhabu ni ya uongo, kwahio kosa liko pale pale sema sasa ni kwamba hajulikani aliyepunguza adhabu au ikulu inaogopa kumtaja aliyepunguza adhabu.

Kweli viongozi wetu kiboko.
 

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,534
8,615
Hata haiingii akilini, kama maamuzi yalifanyika toka mwaka 2005 (chini ya Mkapa) imekuwaje bado wafungwa hao bado walikuwa wamefungwa hadi leo?..
 

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,177
3,326
Kurugenzi ya mawasiliano ikulu yajidhalilisha tena.
Hawa jamaa ni vibuyu kabisa...
Naona ingekuwa taarifa ya CDM au CUF kuandamana ingejaa mbwembwe za kila aina ya kilugha! Maneno vizabinabina, wanafiki, wazandiki n.k yangejaa katika zaidi ya page tatu ambazo Ikulu ingejibu.
 

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,169
2,996
Ni suala jepesi sana, tutajua kama hao wafungwa wametoka au laah baada ya kwenda magereza husika kujua kama ni kweli au laaaah. Halafu kwa nini Ikulu isilitake gazeti kukanusha habari hiyo front page badala yake inaishia kukanusha na kutulia tu. Yupi muongo sasa Ikulu au Mwananchi?

Mkubwa! Nchi hii bila shaka tumeshauzwa lakini mambo yote inalenga serikali legelege iliyopo madarakani.
 

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,938
Huyu Rweyemamu naona amechoka kazi kabisa, hivi hiyo habari alisaini au alisainiwa?

Mimi naona kama kuna kitu kimejificha nyuma ya huu msamaha.

Kwanini ikulu isitoe maelezo yanayojitosheleza hata kama aliyetoa msamaha ni mkapa. Hakuna shida yoyote so long ni ofisi hiyo hiyo, katiba ni ile ile na sheria ni zile zile, watendaji wakuu ndio wamebadilika.

Statement hii inazua maswali mengi yanayohitaji majibu na majibu yenyewe yatoke kwa mtu makini, sio huyu salva aliyechoka kiasi hiki.
 

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,228
8,722
mzee wa rula, jamaa wapo huru na gazeti kwa mjibu wa gazeti la mwananchi na ikulu haijakanusha hilo ila imekanusha kuwa kikwete hakuhusika kuwaachia huru kwa wauji hao ambao kimsingi walifanya kazi hiyo kutii amri ya mkapa..
 

valid statement

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
2,844
835
kama imepunguzwa ina maana hawajatoka bado, ila kwa mambo yanavoenda ktk hii nchi, sitashangaa kuwa ni kweli raisi kawapunguzia adhabu. Lakini kilivonuka tu, wanakanusha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

3 Reactions
Reply
Top Bottom