Ikulu vs Gazeti la Mwananchi: JK akana kuwasamehe waliomuua Lut Jen Kombe

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Gazeti la Mwananchi, matoleo ya jana, Jumatano, Oktoba 12 na leo, Alhamisi, Oktoba 13, 2011, limeandika habari zilizodai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alitoa msamaha wa kupunguza adhabu ya kifo iliyowakabili askari polisi wa zamani waliopatikana na hatia ya kumpiga risasi na kumwua kwa makusudi aliyepata kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Luteni Jenerali Imran Kombe Juni 30, 1996.

Gazeti hili limedai kuwa Mheshimiwa Rais Kikwete alitoa msamaha huo kwa kupunguza adhabu ya kifo iliyokuwa inawakabili makonstebo wapelelezi Mataba Matiku na Juma Muswa na kuibadilisha kuwa kifungo cha miaka miwili.

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inapenda kufafanua kuwa Mheshimiwa Rais Kikwete hajawahi na hajapata kuhusika hata kidogo kutoa msamaha wa kirais kwa kupunguza adhabu ya wauaji hao wa Luteni Jenerali Kombe tokea kuingia madarakani.Masuala yote yanayohusu polisi hao waliohukumiwa kifo kwa mauaji ya Luteni Jenerali Kombe yalifanyiwa maamuzi kabla ya Rais Kikwete kuingia madarakani Desemba 21, 2005.

Imetolewa na:Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu,DAR ES SALAAM.13 Oktoba, 2011

mmh! kuna kitu. nina wasiwasi walikuwa wanaangalia upepo utakuaje kama wakifanya hivyo.
 
Mimi naona kama kuna kitu kimejificha nyuma ya huu msamaha.

Kwanini ikulu isitoe maelezo yanayojitosheleza hata kama aliyetoa msamaha ni mkapa. Hakuna shida yoyote so long ni ofisi hiyo hiyo, katiba ni ile ile na sheria ni zile zile, watendaji wakuu ndio wamebadilika.


2+2=4 sio 22..inasemekana hawa mabwana wapo mtaani kitambo tu wala hio adhabu hawakuitumikia,danganya toto
 
Mimi naona kama kuna kitu kimejificha nyuma ya huu msamaha.

Kwanini ikulu isitoe maelezo yanayojitosheleza hata kama aliyetoa msamaha ni mkapa. Hakuna shida yoyote so long ni ofisi hiyo hiyo, katiba ni ile ile na sheria ni zile zile, watendaji wakuu ndio wamebadilika.


2+2=4 sio 22..inasemekana hawa mabwana wapo mtaani kitambo tu wala hio adhabu hawakuitumikia,danganya toto

Karibu kila mwaka Rais hutoa misahama ya wafungwa na hutangazwa hadharani, iweje msamaha huu wa wauaji ufanyike kwa siri wakati misamaha ya waiba kuku hutangazwa? Serikali kuna kitu gani kinachoendelea kufichaficha ukweli huo wakati hao wauaji walikuwa watumishi waajiriwa na serikali. Kwa vile amri anayopewa askari ni kutoka juu, na tunaposema kutoka juu ina maana mlolongo wote kuanzia rais na waandamizi wake.

Kwa hoja ya Ikulu kuwasafisha kwa kuwafutia adhabu ya kifo badala ya kuwapa adhabu ya kifungo cha maisha inawaacha huru ni dalili tosha kwamba rais na seriakli yake wameridhia mauaji yaliyofanywa na wafungwa hao. Huu ndio utawala unaofuata sheria?
 
Heshima kwenu wakuu!!
kila wakati ninaposoma habari kuhusu utendaji wa "wakoloni weusi" wa Tanzania ninabaki mdomo wazi...
Ningependa kuchukua nafasi hii "kumfundisha" Salvatory Rweyemamu na vibaka wenzake 2 simple rules of mass communication

* Habari iliyokanushwa ni habari iliyotolewa mara mbili i.e. by the time you deny or you rectify any piece of information, you involuntarily participate in its propagation. So kabla ya kukanusha angalia kama ukanushaji wako unasaidia katika kuzima moto au ktk kuuneza in this case I should say you left more questions tha answers!!!!

** unapoziba kiraka( i.e ambiguous information) make sure "dabwada" unalotumia ni la higher quality ukilinganisha na kiraka unachotaka kuziba otherwise it's much more "productive" to leave the kiraka to stay.

You(Mr:Rweyemamu) didn't respect any of the 2 na hii inathibitisha namna ulivyo kilaza. Sasa swali la kujiuliza kama jamaa ni kilaza namna hiyo hao wa chini yake wakoje??? God forbid, I dont wanna even to imagine...

Nyerere alikuwa anapenda kusema kuwa viongozi wabovu( read Kikwete) ni kama mizoga,wana tendency ya kukaribisha kunguru(read wahauri wabovu Salvatory and his likes)....

God bless Tanzania and it's people!!!!
Mr u went too personal that u derail from the typical facts u were to deliver..,next tym,at least try to spam on topic.,actual u intend to teach but eventually u skunked...,the paper cooked the story too systematically that press release was necessary...!
 
Kwa kuwa kosa lilifanyika mwaka 1996, then Mwinyi na Nyerere hawakulifanyia uamuzi.
Watu wawili wanabaki Mkapa au Kikwete.
Kama ni kweli kwamba adhabu ilipunguzwa ikawa miaka miwili, then assuming that Mkapa made this decision on his last day in office, watu hawa wangekuwa nje before or soon 2008. Kwa sababu haikuwa hivyo sidhani kama Mkapa alihusika.
Hapa kuna utata.
 
kweli nimeamini ikulu haina watu makini kuanzia jk na wapambe wake hiyo barua imekaa kibabebabe na wala haina maelezo ya kujitosheleza sasa kama sio yeye aliewasamehe? wametokaje jela? na ninani alie toa msamaha? yaaani hao jamaaa vilaza sana. wanaidhalilisha ikulu yetu. xxxshennzxx
 
Hata haiingii akilini, kama maamuzi yalifanyika toka mwaka 2005 (chini ya Mkapa) imekuwaje bado wafungwa hao bado walikuwa wamefungwa hadi leo?..

hawa jamaa sidhani kama waliwahi kuishi jela, walikuwa uraiani wanakula bata, sasa na wao wako hatarini maana wana siri muhimu sana ya kwamba nini kilitokea
sio muda wata RIP hasa baada ya watu kujua wako mtaani na serikali inakana jinsi walivyofika huko
sarakasi hii wameangukia pua wote kwa ujumla, sidhani kama watawaudisha jela, ila nina hakika wanaweza kuwa komba pia
 
Mr u went too personal that u derail from the typical facts u were to deliver..,next tym,at least try to spam on topic.,actual u intend to teach but eventually u skunked...,the paper cooked the story too systematically that press release was necessary...!

Heshima kwako bro!
A certain philosopher(don't remember he name...sorry) used to say " if you don't stand for what you believe, then either your creed is worthless or you are worthless"
Now what I said regarding Kikwete and his gang is not personal - I think everyone in good faith can witness and testify the inability of the man to govern surely he's able to rule but not to lead, hope you know the difference between the two!!!

Regarding "kufundisha" I didn't find a better terminology but if you have one please forward it to me for future reference(s): in any case I didn't navigate in the merit of the issue instead what I did was simply to provide 2 simple rules of mass communication which he should know better than I do because the guy earns his daily bread thanks to that...

As far as "VIONGOZI WABOVU" is concerned, I surely don't own the copyright and I kindly mentioned the source so I don't know what is your argument so far!!!!

Hauhitaji kuwa na degree ya uongozi ili kujua kwamba Kikwete ni kiongozi mbovu!!!! Labda umekuwa disturbed na neno VIBAKA - those guys starting with Kikwete and the members of his family down to the members of his gang(read CCM aka MAGAMBA) are looting the natural resources as well as the finance of our country - how should I call them???? I'm afraid I was even fairly diplomatic.
 
Jamaa wamenukuliwa wakiwa kitaa maeneo ya mo town.SWALI.Nani aliyeidhinisha hawa jamaa watoke,jamani?
 
nchi hii, inawezakana hata Col. Muamar Gaddafi yumo humu lakini sisi hatujui
 
hiyo adhabu imepunguzwa na Mkapa au Kikwete? mbona wanatuchanganya hawa akina Rweymamu?
 
hakuna haja ya kuumiza vichwa ili kujua ni nani aliyetoa msamaha huo, kwa mujibu wa katiba mwenye uwezo wa kutoa msamaha huo ni rais wa nchi na tukio lilitokea 1996 wakati mkapa yuko madarakani na baada ya mkapa ni kikwete aliyefata kuwa rais, na kwa kuwa kurugenzi ya mawasiliano ikulu imekanusha kuwa jk hakuhusika kutoa msamaha huo hata kama maelezo yao hayajitoshelezi kutuambia ni nani aliyetoa msamaha huo but common sense inatuonesha dhahiri kuwa kurugenzi ya mawasiliano ikulu imepoint finger kwa mkapa. tuelewe kuwa msamaha huo lazima utolewe na rais na marais wahusika wa sakata hilo ni kati ya mkapa au kikwete, nyerere na mwinyi hawahusiki kwa kuwa tukio lilitokea wakiwa hawapo madarakani kwa hiyo kazi ipo kwa ndugu mkapa kujitetea au kueleza umma huku akielewa wazi kuwa 'mtuhumiwa' mwenzake jk keshautema msala huo na hivyo kumaanisha kidole amenyooshewa yeye! na akikaa kimya maana yake ni kuwa amekubali kuwa yeye ndo alietoa msamaha huo wenye kutia mashaka hasa ukizingatia ndugu imran kombe aliuwawa wakati wa kipindi chake na hivyo tuhuma hizi zinaelekea kwake kwa kuzingatia maelezo niliyotoa hapo juu.
 
Back
Top Bottom