Ikulu: Mashangingi sasa basi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu: Mashangingi sasa basi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jun 22, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,188
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Ikulu: Mashangingi sasa basi [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Thursday, 21 June 2012 19:49 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Boniface Meena na Fidelis Butahe
  Mwananchi

  OFISI ya Rais, Ikulu imesema Serikali itaanza kuwakopesha viongozi wake wa ngazi mbalimbali magari madogo ya gharama nafuu ili waachane na mashangingi yanayotumika sasa.

  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue aliliambia gazeti hili kuwa mpango huo unaotarajiwa kuanza Julai mwaka huu, una lengo la kupunguza matumizi ya Serikali kwa kuondokana na magari makubwa yenye gharama kubwa za uendeshaji.

  Balozi Sefue alisema mpango huo unaanza katika mwaka huu wa fedha ambapo yatachambuliwa magari yanayofaa na yatapendekezwa yatumike katika shughuli gani.

  Alipoulizwa kama mabadiliko hayo yatawagusa mawaziri na majaji, Balozi Sefue alisita kulijibu hilo (Kikwete dhaifu)na badala yake alisema kuwa bado suala hilo lipo katika mjadala.

  “Hili jambo bado linajadiliwa, haya yote yatafanyika katika mwaka huu wa fedha,” alisema Balozi Sefue. Mwaka wa fedha unaaza Julai mosi mwaka huu.

  Akifafanua zaidi alisema, “Kwanza tutatizama gari husika linatumia mafuta kwa kiwango gani, pia tutatizama hata gharama nyingine kama ufundi,” alisema Balozi Sefue.

  Alisema kuwa utaratibu huo ukianza viongozi wanaotumia magari ya Serikali wataanza kukopeshwa magari hayo na kupewa posho kwa ajili ya kuweka mafuta.

  “Ni kipaumbele cha Serikali kuangalia hilo mwaka huu na hata katika bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/13 imeelezwa wazi, lengo ni kupunguza gharama za uendeshaji,” alisema Sefue.

  Aliongeza, “Badala ya kumpa mtu gari tunamkopesha halafu tunakuwa tunampa mafuta ili kupunguza matumizi Serikalini.”

  Alisema katika uchambuzi huo wataangalia ni kiongozi gani atahitaji gari la Serikali na yupi atatakiwa kukopeshwa na kwamba hali hiyo itafuatana na kazi za mtumishi husika.

  “Tunaangalia hili la magari, lengo ni kuwa na magari ya aina fulani lakini si ya kifahari na tutawakopesha watumishi,” alisema Sefue.

  Alisema kuwa katika uchambuzi huo pia watazingatia ubora wa gari husika ikiwa ni pamoja na kustahimili kusafiri masafa marefu, kulingana na majukumu ya mtumishi.

  “Yapo mambo ambayo Serikali imeyapanga na lazima yatekelezwe,” alisema Sefue.

  Alipoulizwa kama mpango huo ni utekelezwaji wa mpango uliotolewa na Wizara ya Ujenzi mwaka 2004 wa kubana matumizi ya magari ya Serikali alisema hilo linaweza kutolewa ufafanuzi na Wizara ya Ujenzi yenyewe.

  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Herbert Mrango alipoulizwa kuhusu utekelezaji wa mpango huo alisema hawezi kuzungumzia mambo ya Serikali kwenye simu.

  Wakati Balozi Sefue akisema hayo tayari kuna baadhi ya viongozi Serikalini wameshajikopesha magari hayo akiwemo Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu.

  Suala la Ndulu kujikopesha gari lilielezwa hivi karibuni na Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe alipokuwa akisoma bajeti mbadala ya kambi rasmi ya upinzani bungeni.

  Zitto alisema Serikali inatakiwa kupunguza mzigo wa matumizi ya magari ya Serikali kwa kupiga mnada baadhi ya ‘mashangingi’ na kuweka mfumo wa kukopesha magari kwa watumishi wote wa umma wanaostahili magari kama alivyofanya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

  Balozi Sefue alipoulizwa kuhusu suala la Ndulu kujikopesha gari alisema hajuI bali huo unaweza ukawa ni utaratibu wa Bodi ya Wakurugenzi ya BoT ndiyo ambayo inaweza ikawa imepitisha hilo.
  “Kwa maana ya framework hakuna kinachomzuia kufanya hivyo,” alisema.

  Katika mkutano wa 7 wa Bunge, Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), John Cheyo alieleza kuwa kumekuwa na matumizi yasiyo ya lazima katika uendeshaji na ukarabati wa magari hayo na hadi Juni 30, 2010 Serikali ilikuwa inamiliki magari yenye thamani ya Sh5 trilioni.
Alisema mwendelezo wa ununuzi wa magari unaofanywa na Serikali unaongeza gharama za uendeshaji na kusisitiza kwamba matumizi hayo si ya lazima kwa Serikali yenye uchumi mdogo uliozidiwa na madeni.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Story hiyo ilianza tangu zamani lakini hatuoni vitendo. Tumechoka kusikia wimbo huo.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,188
  Trophy Points: 280
  Kikwete dhaifu na Serikali yake ya kifisadi pia ni dhaifu. Hili la gharama kubwa ya kuhudumia mashangingi limepigiwa kelele miaka chungu nzima lakini Serikali dhaifu ikashindwa kuchukua hatua muafaka, yule Pinda kama Waziri Mkuu na kiongozi wa Serikalini bungeni bila hata aibu aliamua kurudisha shangingi lake tu!!! badala ya kutoa maamuzi ya kurudisha mashangingi yote Serikalini.
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  typical Tanzania, dibaji peji 100, matendo kiduchu....
   
 5. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Pinda ni kunguru mwoga. Ndiyo maana katika mawaziri wakuu wadhaifu Pinda ni top. Yeye kazi yake ni kulalama tu wakati mamlaka ya kuchukua hatua anayo. I am sorry, lakini ukweli ni kwamba imefika mahali ninamdharau sana waziri mkuu wetu.
   
 6. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hivi mfanyakazi wa serikali ambae hafanyi kazi kwenye independent department or agency of the government wa juu kabisa analipwa TShs ngapi? Hawa ambao km ana-first degree anaanza na TGS D, na viwango vingine.

  Maana wengi malalamiko mishahara midogo.... kumkopesha gari lenye ubora, linalostahimili masafa marefu kulingana na utumishi wa umma.... are they in a position to pay kwa mapato yao ya mshahara?

  It's a good move but in strong working system. Wasi wasi wangu kwa mfumo na muundo wetu watapewa magari, wanachota humo humo serikalini kuyalipia, claims tu za mafuta (fuel allowance)zitatosha kulipia.

  Ni wazo zuri though. Km ni wizara pool iwe na magari machache..... madereva vibarua hivyooooooo vinaota nyasi.......
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,188
  Trophy Points: 280

  Kikwete dhaifu, Pinda dhaifu, Serikali fisadi dhaifu.
   
 8. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  labda sasa hivi wamejifunza!
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  Jun 22, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Sefue naye dhaifu kama babake. Anatoaje taarifa hajua itawagusa akina nani.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,188
  Trophy Points: 280
  Wala hujakosea Mkuu, kulikuwa na haja gani ya kukurupuka kama hajui ni nani watakaoguswa na maamuzi haya kuhusu mashangingi.
   
 11. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mbona sio vibaya kwa Tanzania kuiga mazuri? Waende Rwanda wajifunze jinsi ambavyo magari hayo yalitangazwa mnada...sio kufanya selective decision ya kuwakopesha viongozi (na kwa nini viongozi wakati rasilimali za wananchi). Huu ni mwanya mwingine wa kupoteza rasilimali. Pili haiingii akilini kuwakopesha na kisha kuwapa posha ya kununulia mafuta (its made in Tanzania only) Kwa hiyo tutataka kuaminishwa kuwa tatizo ni umiliki (kati ya government and senior officials) au ni gharama za uendeshaji magari hayo? Nadhani kwa hili serikali ijipange upya otherwise ni yale yale ya jana na juzi....hakuna umakini kwenye hili
   
 12. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #12
  Jun 22, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Naomba nisisitize tena hoja yako hii ndugu yangu.

  wapande ndege waende Rwanda. Kule watajifunza kuwa anayepewa gari na dereva ni Raisi, Spika na Jaji mkuu peke yao. Wengine wote wanakopeshwa na kujiendeshwa (au kuajiri madereva) wenyewe.

  Kwa hapa Tanzania, mi napendekeza wafuatao tu ndio wapewe magari na dereva
  1. Raisi
  2. makamu wa raisi
  3. Waziri mkuu
  4. Spika
  5. Jaji Mkuu

  Watendaji wengine wote wa serikali wakopeshwe magari kwa mkopo nafuu, wapewe laki 2 za mafuta kwa mwezi, na wajiendeshe wenyewe. Kama kuna ambaye anataka dereva, aajiri kwa hela yake...
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,188
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana nawe ila hawastahili kulipwa posho ya kununulia mafuta, kama watalipwa posho basi iwe inakatwa kodi ili kupunguza gharama kubwa za Serikali.
   
 14. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #14
  Jun 22, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Story hii inafanana na ile serikali kuhamia dom.
   
 15. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #15
  Jun 22, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  This is Isidingo the Need, episode 20000.............
  Hakuna jipya katika habari hii! Inamaana toka PM atoe maagizo enzi hizo hii issue ipo kwenye majadiliano tu.

  Kweli hii serikali mufilisi na dhaifu.
   
 16. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #16
  Jun 22, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Watz tunapenda mambo makubwa kuliko uwezo wetu, yaani matumizi yako juu kuliko uzalishaji. Rwanda imepiga hatua kama iliyopata uhuru miaka 50, siku na saa ambazo si za kazi raisi anajiendesha mwenyewe, kwetu mpaka saa 8 za usiku utakuta gari ya serikali na dereva wake amepark bar anamsubiri bosi wake.
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Jun 22, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kauli hizi ziliwahi kumgarimu Magufuli mpaka waka mpa sumu kidogo afe...akaja pinda akasema serikali haitanunua magari ya kifahari yakanunuliwa nae akapewa moja akaona noma akasema mimi nitatumia lile kwangu la zamani labda mmpe msaidizi wangu, pinda hakuchukua hatua yoyote licha ya kuonyeshwa dharau ya hali ya juu sana..
   
 18. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #18
  Jun 22, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  ukiona hivyo ujue ni series ya maigizo yanayoendelea kwa watz!
   
 19. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #19
  Jun 22, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Silly government in a silly season with a dhaifu prezidaa.
   
 20. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #20
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nami nashindwa kushangaa!
   
Loading...