Ikulu: Mashangingi sasa basi

Ikulu: Mashangingi sasa basi

Kikwete dhaifu na Serikali yake ya kifisadi pia ni dhaifu. Hili la gharama kubwa ya kuhudumia mashangingi limepigiwa kelele miaka chungu nzima lakini Serikali dhaifu ikashindwa kuchukua hatua muafaka, yule Pinda kama Waziri Mkuu na kiongozi wa Serikalini bungeni bila hata aibu aliamua kurudisha shangingi lake tu!!! badala ya kutoa maamuzi ya kurudisha mashangingi yote Serikalini.

Nakubaliana na wewe mkuu BAK,kuna matumizi mabaya sana ya rasilimali za uma ,inashangaza sana kuona kuna magari ya kifahari mengi mno .Nilikuwa nafanya tathmini nikagundua kuwa inawezekana kabisa baazi ya maafisa wa serikali kukopeshwa magari na kuwa wanayaendesha wenyewe wanapoenda field/ofisini badala ya kuwa na lundo la watumishi(Madereva).Kama maafisa kilimo wa tarafa na kata wamekopeshwa pikipiki na wanaziendesha wenyewe kwa nini kwenye magari ishindikane!!?.Jk ni kiongozi dhaifu hilo halipingiki.
 
Chama kinachotembeza bakuli kwenye mikutano kiongozi wake anakwenda kwenye mkutano na mashangingi sita.
 
Story hiyo ilianza tangu zamani lakini hatuoni vitendo. Tumechoka kusikia wimbo huo.

Tumechoka na hizi political rhetorics za CCM dhaifu. Mbona wenzetu Kenya, Rwanda wameweza tena bila kupiga kelele nyingi kama sisi.

Hata Biblia Takatifu inasema IMANI BILA MATENDO NI BURE!
 
Chama kinachotembeza bakuli kwenye mikutano kiongozi wake anakwenda kwenye mkutano na mashangingi sita.

Kipi hicho, au ndio kile cha kaskazini?
WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.
 
Waziri wa uholanzi.jpg
(WAZIRI MKUU WA UHOLANZI AKITUMIA BAISKELI KWENDA KAZINI MWENDO WAZAIDI YA KM.2)
Hii ni Hadithi na ekaya za abunuas kama Pinda alikataa shangingi akisema ni hatua yake yakwanza kupunguza matumizi ya serikali!baada ya siku 5 zakazi waliopo chini yake wakalichukua bila ya woga!1Waziri mkuu aseme hiki sitaki!aje wachini yake afanye yale waliyokatazwa na kiongozi wao???Huyo atakuwa waziri mkuu jina lakini hii ndivyo ilivyo fanyika Tanzania na waziri mkuu Pinda hakusema kitu na mashangingi yakanunuliwa kama njugu hata maafisa ugavi nao wakawa na mashangingi hii ndo tanzania hivyo hapa mimi sijaona wakuzuia ununuaji wamashangingi!!J e hapa ninani anaweza kupanda hata bajaji kama siyo baiskeli??
 
Mbona sio vibaya kwa Tanzania kuiga mazuri? Waende Rwanda wajifunze jinsi ambavyo magari hayo yalitangazwa mnada...sio kufanya selective decision ya kuwakopesha viongozi (na kwa nini viongozi wakati rasilimali za wananchi). Huu ni mwanya mwingine wa kupoteza rasilimali. Pili haiingii akilini kuwakopesha na kisha kuwapa posha ya kununulia mafuta (its made in Tanzania only) Kwa hiyo tutataka kuaminishwa kuwa tatizo ni umiliki (kati ya government and senior officials) au ni gharama za uendeshaji magari hayo? Nadhani kwa hili serikali ijipange upya otherwise ni yale yale ya jana na juzi....hakuna umakini kwenye hili


Mkuu BUBE,

Kwa kweli huu ni ujinga, hawastahili kupewa mafuta kabisa, mi najiuliza hivi si sisi wafanyakazi ndio tunawalipa mishahara? Waangalie kwenye private sector ni watu wanagapi wanapewa mafuta na waajiri wao.

They should dish out money from their pockets kama watu wengine sio kuwa wanyonyaji, sote tunatoka jasho ili kukidhi mahitaji yetu ya kila siku, mie siku nikikosa hela ya mafuta narukia daladala, why not them shiit
 
mengi tutasema lakini bado uamuzi huu ni kwa maslahi ya taifa .... naunga mkono Ikulu kwa uamuzi huu.
 
Wana pagawa tu tu...

Mie toka nianze kusikia lakini hadi juzi wiki tatu zilizo pita nimeona kigogo mmoja wa serikari kanunuliwa V8 kwa pesa za

wananchi!


Naionea huruma sana sana serikali hii chakavu ya raisi dhaifu,.................

Hizi ni ahadi pia...na wanachi wanarekodi na kuja kupima baadae.

Hilo la kwanza,

La pili ni kwamba kwayaliyokwisha nunuliwa si yanaendelea kutumika tena kwa gharama kubwa mno!!!

Kwanini wasitangaze kuyapiga mnada basi kama wa nia ya dhati kweli ya kupunguza gharama za matumizi!?
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Ikulu: Mashangingi sasa basi [/TD]

Serikali kwanini inaona aibu kutekeleza ushauri unaotolewa na CDM? Ushauri huu umekuwa ukitolewa na CDM toka awali.
 
Yani kati ya kitu kinachonisababishia vidonda vya tumbo ni kuona haya mashangingi mjini....
 
Watz tunapenda mambo makubwa kuliko uwezo wetu, yaani matumizi yako juu kuliko uzalishaji. Rwanda imepiga hatua kama iliyopata uhuru miaka 50, siku na saa ambazo si za kazi raisi anajiendesha mwenyewe, kwetu mpaka saa 8 za usiku utakuta gari ya serikali na dereva wake amepark bar anamsubiri bosi wake.

Hapo kwenye RED kama ni kweli Rwanda wamefikia hatua hiyo, basi naanza kauamini kuwa Rwanda is no longer part of AFRICA! Kama umeona huyo Katibu mkuu kiongozi kashindwa kujibu nani na nani watapokonywa mashangingi basi ujue hayo mashangingi tutaendelea kuyaona yakilandalanda na namba za ST..... na DFP........!

Utashangaa gali la kamanda wa polisi wa LINDIi ni la kifahari kuliko la mkuu wa polisi LONDON! Naendelea kuamini kuwa hapa Tz kwa hali ya uchumi wetu hakuna kiongozi anastahili kutumia V8 inayomilikiwa na serikali PERIOD!

 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Ikulu: Mashangingi sasa basi [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Thursday, 21 June 2012 19:49 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Boniface Meena na Fidelis Butahe
Mwananchi

OFISI ya Rais, Ikulu imesema Serikali itaanza kuwakopesha viongozi wake wa ngazi mbalimbali magari madogo ya gharama nafuu ili waachane na mashangingi yanayotumika sasa.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue aliliambia gazeti hili kuwa mpango huo unaotarajiwa kuanza Julai mwaka huu, una lengo la kupunguza matumizi ya Serikali kwa kuondokana na magari makubwa yenye gharama kubwa za uendeshaji.

Balozi Sefue alisema mpango huo unaanza katika mwaka huu wa fedha ambapo yatachambuliwa magari yanayofaa na yatapendekezwa yatumike katika shughuli gani.

Alipoulizwa kama mabadiliko hayo yatawagusa mawaziri na majaji, Balozi Sefue alisita kulijibu hilo (Kikwete dhaifu)na badala yake alisema kuwa bado suala hilo lipo katika mjadala.

"Hili jambo bado linajadiliwa, haya yote yatafanyika katika mwaka huu wa fedha," alisema Balozi Sefue. Mwaka wa fedha unaaza Julai mosi mwaka huu.

Akifafanua zaidi alisema, "Kwanza tutatizama gari husika linatumia mafuta kwa kiwango gani, pia tutatizama hata gharama nyingine kama ufundi," alisema Balozi Sefue.

Alisema kuwa utaratibu huo ukianza viongozi wanaotumia magari ya Serikali wataanza kukopeshwa magari hayo na kupewa posho kwa ajili ya kuweka mafuta.

"Ni kipaumbele cha Serikali kuangalia hilo mwaka huu na hata katika bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/13 imeelezwa wazi, lengo ni kupunguza gharama za uendeshaji," alisema Sefue.

Aliongeza, "Badala ya kumpa mtu gari tunamkopesha halafu tunakuwa tunampa mafuta ili kupunguza matumizi Serikalini."

Alisema katika uchambuzi huo wataangalia ni kiongozi gani atahitaji gari la Serikali na yupi atatakiwa kukopeshwa na kwamba hali hiyo itafuatana na kazi za mtumishi husika.

"Tunaangalia hili la magari, lengo ni kuwa na magari ya aina fulani lakini si ya kifahari na tutawakopesha watumishi," alisema Sefue.

Alisema kuwa katika uchambuzi huo pia watazingatia ubora wa gari husika ikiwa ni pamoja na kustahimili kusafiri masafa marefu, kulingana na majukumu ya mtumishi.

"Yapo mambo ambayo Serikali imeyapanga na lazima yatekelezwe," alisema Sefue.

Alipoulizwa kama mpango huo ni utekelezwaji wa mpango uliotolewa na Wizara ya Ujenzi mwaka 2004 wa kubana matumizi ya magari ya Serikali alisema hilo linaweza kutolewa ufafanuzi na Wizara ya Ujenzi yenyewe.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Herbert Mrango alipoulizwa kuhusu utekelezaji wa mpango huo alisema hawezi kuzungumzia mambo ya Serikali kwenye simu.

Wakati Balozi Sefue akisema hayo tayari kuna baadhi ya viongozi Serikalini wameshajikopesha magari hayo akiwemo Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu.

Suala la Ndulu kujikopesha gari lilielezwa hivi karibuni na Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe alipokuwa akisoma bajeti mbadala ya kambi rasmi ya upinzani bungeni.

Zitto alisema Serikali inatakiwa kupunguza mzigo wa matumizi ya magari ya Serikali kwa kupiga mnada baadhi ya ‘mashangingi' na kuweka mfumo wa kukopesha magari kwa watumishi wote wa umma wanaostahili magari kama alivyofanya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

Balozi Sefue alipoulizwa kuhusu suala la Ndulu kujikopesha gari alisema hajuI bali huo unaweza ukawa ni utaratibu wa Bodi ya Wakurugenzi ya BoT ndiyo ambayo inaweza ikawa imepitisha hilo.
"Kwa maana ya framework hakuna kinachomzuia kufanya hivyo," alisema.

Katika mkutano wa 7 wa Bunge, Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), John Cheyo alieleza kuwa kumekuwa na matumizi yasiyo ya lazima katika uendeshaji na ukarabati wa magari hayo na hadi Juni 30, 2010 Serikali ilikuwa inamiliki magari yenye thamani ya Sh5 trilioni.
Alisema mwendelezo wa ununuzi wa magari unaofanywa na Serikali unaongeza gharama za uendeshaji na kusisitiza kwamba matumizi hayo si ya lazima kwa Serikali yenye uchumi mdogo uliozidiwa na madeni.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

ITS good move ila madereva muanze kutafuta kazi.......
 
Pinda ni kunguru mwoga. Ndiyo maana katika mawaziri wakuu wadhaifu Pinda ni top. Yeye kazi yake ni kulalama tu wakati mamlaka ya kuchukua hatua anayo. I am sorry, lakini ukweli ni kwamba imefika mahali ninamdharau sana waziri mkuu wetu.
ki mamlaka pinda ana uwezo huo kinadharia tu. ki vitendo Pinda hana uwezo huo, unless JK angekuwa upande wake. The same way JK alivyomteua Pinda kuwa waziri mkuu ni the same way JK ana-uwezo wa kumuondoa Pinda madarakani. System ya serikali ya TZ haimfanyi waziri mkuu kuwa huru kwenye madaraka, anakuwa kibaraka tu wa rais. Vinginevyo system ibadilishwe.
 
Back
Top Bottom