Ikulu: Makonda ni kijana muadilifu

Ikulu: Makonda ni kijana muadilifu

Ikulu imekejeli kauli zinazotolewa kwa lengo la kupinga uteuzi wa Paul Makonda kuwa mkuu wa wilaya,kauli hizo ni zile zinazodai kuwa Makonda amekosa maadili na pia hana nidhamu na badala yake Ikulu imedai kuwa Makonda ni kijana muadilifu.

CHANZO:Mtanzania

Mimi ni kada Wa Ccm lakini siungi uteuzi Wa huyu pimbi makonda.

Teamlowasa .
 
Ikulu gani...!? Hivi siku hizi tuna ikulu!!? Ingekuwa ni mnyama angekuwa kwenyekundi la wanyama waliotoweka miaka 7 iliyopita...!!
 
Hao wanaosema Makonda ni muadilifu, wao nao ni waadilifu? Ikulu kumejaa genge la wahuni woge!
 
Ben mimi naamini wewe ni kati ya watu makini hapa jamvini hebu nipe sababu tatu za msingi na isiwe majungu ya kisiasa zinazoeleza kwa nini makonda hafai kuwa DC
 
1:Mtu asiyefuata kanuni na taratibu za chama chake hawezi kufuata kanuni na sheria za mahali pa kazi.Wakati kimaadili na kikatiba ndani ya chama chake inakatazwa mtu kutoa tuhuma kwa kiongozi ndani ya chama bila kutumia vikao halali

2:Mtu aliyechafua Masheikh na Maaskofu na kuwaunganisha kwenye kundi la watu wavivu na matapeli wanaopenda hela za haraka hafai kuwa Mkuu wa Wilaya ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambayo ufanisi wake unategemea ushirikishwaji wa makundi mbalimbali katika kulinda amani wakiwepo viongozi wa Dini

3:Kitendo cha kuungana na vijana wa chama chake kumletea vurugu mzee Warioba,kiongozi mwenye historia iliyotukuka ndani na nje ya Tanzania ni utovu wa maadili na inajenga picha mbaya kabisa kwa watu wa kada tofauti

Zingatia,Sababu nyingine ya msingi zaidi kwa kuwa ukuu wa Wilaya au Mkoa ni mfumo unaopingwa sana basi hata yeye tu kuteuliwa kuwa DC moja kwa moja hapaswi kuwa DC kwa sababu huo mfumo hatuutaki kabisa.

Mfumo wa U-DC hautakiwi so pia Hafai kuwa DC
 
Ben kwa hili LA makonda Leo nakuunga mkono japo kiitikadi Tupo tofauti.

Makonda hafai hata ubalozi Wa nyumba kumi
 
Ikulu inasema Inakanusha pia Mboni Mhita hana makalio makubwa.

Na kwamba u dc wake haukutokana na kuwa na makalio bali ni mvuto wa DC mwenyewe.

Hii ndio lkulu yetu, yasiyo na umuhimu hukanushwa haraka
 
Back
Top Bottom