Ikulu, Dar: Rais Samia aongea na viongozi wa Machinga Dar es Salaam. Machinga Watambuliwa kama kundi Maalum

Sioni kama ni kosa kwa Rais kukaa chini na machinga kama jamii yenye watu wengi....Lengo ni kujadili na kusikia kero zao kutoka kwenye ground then waone namna bora ya kutatua..
Hamna wamachinga hapo, kero zao wamesemewa na Mkuu wa mkoa
 
Ndugu zangu wamachinga Dar na nchi nzima. Je, huyo jamaa yenu mlimtuma wenyewe aseme??

"Steven Lusinde, M/mwenyekiti wa Wamachinga taifa

Kwenye hotuba yako Mh. Rais uliagiza Wamachinga tupangwe vizuri. Jambo lile lilitupeleka mchakamchaka kidogo. Sasa tumepangana vizuri na mambo yamekwenda kama tulivyotarajia..."
 
Ma dc,rc na viongozi wengine wa serikali na ni wengi kuliko wahusika wa huo mkutano.
 
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu leo aanaongea na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam pamoja na viongozi wa wamachinga Ikulu ya Dar es Saam.

Kumekuwa na badiliko la sera ya wamachinga karibuni kutoka utawala uliopita kwa 'kupangwa upya' ama kwa wengine kuondolewa na vibanda vyao kuvunjwa. Pia majanga ya moto hayako nyuma
Kaongea kwa upole, tumpe kura zetu.
 
Kaongea kwa upole, tumpe kura zetu.
Screenshot_20220125-135052.png

Kwa hiyo anashukuru watu kuvumilia maumivu ya kubomolewa, kuibiwa na kuchomewa mali zao??
Kauli ya kifedhuli sana hii. Na wewe pamoa na wenzako mtampa kura
 
Sioni kama ni kosa kwa Rais kukaa chini na machinga kama jamii yenye watu wengi....Lengo ni kujadili na kusikia kero zao kutoka kwenye ground then waone namna bora ya kutatua..
Tofautisha kukaa kujadiliana na kukaa kusikiliza .
 
Mama malori kariakoo ndio shida mpya iliyopo sasa hivi,
Jiji wanapiga hela nyingi sana kwa kuwaruhusu wenye malori kariakoo
Wafunge na kuharibu barabara zilizojengwa kwa gharama nyingi,
Machinga munawaonea tu
 
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu leo aanaongea na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam pamoja na viongozi wa wamachinga Ikulu ya Dar es Saam.

Kumekuwa na badiliko la sera ya wamachinga karibuni kutoka utawala uliopita kwa 'kupangwa upya' ama kwa wengine kuondolewa na vibanda vyao kuvunjwa. Pia majanga ya moto hayako nyuma

Nini kitajiri! Kuwa nami.

========

Amos Makalla, RC Dar

Mafanikio tulioyapata tutayalinda. Na katika kuyalinda tumekuja na kampeni ya usafi. Usafi ni sehemu ya kulinda mafanikio ya kutokufanya biashara holela. Dar es Salaam itaendelea kupendeza na yenye mazingira mazuri ya watu kufanya biashara katika mpango mzuri kama ambavyo tumepangana sasa.

Steven Lusinde, M/mwenyekiti wa Wamachinga taifa

Kwenye hotuba yako Mh. Rais uliagiza Wamachinga tupangwe vizuri. Jambo lile lilitupeleka mchakamchaka kidogo. Sasa tumepangana vizuri na mambo yamekwenda kama tulivyotarajia.

Rais Samia Suluhu Hassan

Nimeamua kukutana nanyi wa Dar es Salaam lakini haimaanishi sitakutana na wengine. Dar es Salaam inaleta mkusanyiko wa watu wote na meseji ikitoka Dar itawafikia na wengine.

Dar es Salaam mmeonesha mfano wakati wa kupangana. Kuna watu walikuwa wanasubiri vurugu zitokee nchi iharibike lakini mmekuwa waungwana, mmekuwa wazalendo. Mmeshirikiana na viongozi wa serikali na hayo hayakutokea.

Niwape pole kwa mioto inayotokea ndani ya mkoa wetu wa Dar. Tulishuhudia moto pale Kariakoo na hivi majuzi pale Karume. Na mioto hii ina sababu mbalimbali.

Ni matumaini yangu mbele tuendako tutakaa kitako. Timu za serikali na zinafanya uchunguzi wa sababu za mioto. Lakini uongozi wa achinga na masoko utakaa kitako kuona sababu ni zipi na tuweze kuzichukulia hatua.

Niwape pole kwa yale yote yanayotokea. Serikali ipo pamoja nanyi katika hili.

Nataka niwaambie kuwa hili kundi lenu serikali inawatambua vyema. Katika mipango yetu yote ya Serikali, mpango wetu wa miaka 5 uliomalizika, mpango wa pili na huu tunaokwenda nao na wan ne tutakaotunga, mtazamo wetu mkubwa ni kwa vijana. Watanzania asilimia 65 kama siyo 70 ni vijana. Na vijana hawa lazima wawe na ajira, wawe na kazi.

Kwa Serikali peke yetu si kweli kwamba tutaweza kutoa ajira kwa vijana wote. Mlilolifanya kujiajiri wenyewe katika biashara, mkaunda umoja wen una mkajipanga vyema, hii itatusaidia sana Serikali kulihudumia kundi hili na kuhakikisha ajira zao zinaendelea kuwepo.

Sasa ni rasmi Serikali inalitambua kundi hili kwamba ni moja ya makundi katika yale makundi maalum yali katika wizara wizara maalum tuliyounda. Ni moja kati ya makundi maalum yatakayofanya kazi na serikali.

Tuliamua kupangana kwakuwa hata nyie hali mliiona. Ilikuwa Kariakoo huna pa kupita. Wale vijana waovu walitumia fursa ile ya kuchanganyika kule ili kufanya uovu. Mitaani wakasema, wamachinga wezi, wamachinga majambazi, wamachinga wanatukupua kumbe siyo wamachinga ni vijana waovu waliotumia fursa ile.

Mwenyekiti wa wamachinga Tanzania yuko Mkoa wa Arusha, Leo mbele ya Rais kaibuka mtu mwingine anasema ni Mwenyekiti wa wamachinga Tanzania. Hii imekaaje?
 
Mwenyekiti wa wamachinga Tanzania yuko Mkoa wa Arusha, Leo mbele ya Rais kaibuka mtu mwingine anasema ni Mwenyekiti wa wamachinga Tanzania. Hii imekaaje?
wababaishaji tu hao wana create tatizo na kujifanya wamekuja na jibu....
huyu mama anaona sasa ameshikwa na wahuni nyie , namhurumia sana huyo mama
 
Sasa machinga wanaweka kwenye wizara ya wazee jinsia wanawake na watu maalam ikiwa wale ni wafanyabiashara wanatamani kukua.

Muda huo huo una waita wafanya biashara na mabenki watoe pesa kuwatia mikopo.

Muda huo mmeruhusu waanze ujenzi wa vibanda pale karume ikiwa Rc makala kaambiwa atafute kandarasi na soko litajengwa.

Nchii hii ya ccm ina kazi nzito sana kufika kila mtu anapo tarajia.

Ujenzi wa soko na kutafuta kandarasi kuna familia ndio zinauaga umasikini
 
Aidha, amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutafuta mkandarasi atakayejenga soko eneo la Jangwani, na baada ya hapo, ujenzi wa Soko la Karume utafuata.

Mmmh!!! Jangwani tena??

Kwa nini wasitumie lile eneo la UDA ilipo karakana ya mwendokasi sasa, na hao BRT wakaenda Ubungo pape wanajengewa
 
Back
Top Bottom