Iko wapi sukari iliyoagizwa serikali?

Iko wapi sukari iliyoagizwa serikali?

Ndo hasara za kauli za kukurupuka
Hili bomu la sukari halijakaa vizuri. Mbwembwe zooote za Majaliwa na kutuaminisha koote kwamba hakutakuwa na shida ya sukari na hili tatizo litakwisha kabla ya Mfungo zimeishia hewani!
 
Hali ni mbaya sana kila mahali juzi kampuni inayolipa kodi kubwa kuliko kampuni zote TBL walikuwa wanalalamika mauzo yao kushuka 40%
Nimeona mkuu!! na subil iyo tar 8 iyo bajet kuu kiroja gan kitatokea kwenye iyi bajet yao
 
Hili bomu la sukari halijakaa vizuri. Mbwembwe zooote za Majaliwa na kutuaminisha koote kwamba hakutakuwa na shida ya sukari na hili tatizo litakwisha kabla ya Mfungo zimeishia hewani!

Sasa hivi utasikia 'Kwa kutambua madhara ya sukari mwilini serikali imeagiza tende na halua kwa wingi ili watu walie maghimbi kwenye mwezi mtukufu' na hilo litaambatana na bei elekezi ya tende
 
Kwani yako wapi makontena yalokamatwa.? Wapi magodauni yalobainika kuficha sukari, tuliona kwa kideo yamekamatwa na tukaahidiwa kugaiwa bure....😉
 
WANA JF HESHIMA KWENU WOTE

Kwa muda sasa kumekuwa na tatizo la sukari kutopatikana maeneo mengi kutokana uamuzi wa serikali kuzuia vibali vya kuagiza sukari bila kujipanga.

Mwenzi uliopita Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa tani 11,957 ambazo serikali imeagiza zilikuwa zimeshawasili na kwamba hiyo sukari ingeuzwa kwa bei elekezi kilo 1800. Kuhusu tani zingine 240000 za sukari zingewasili ijumaa mei 13 na hadi zitoke bandarini ingekuwa jumapili na usambazaji ungefanya mei 16.

Pia tuliambiwa tani 20000 zingewasili mwisho wa mwenzi uliopita au mwanzoni mwenzi huu. Mpaka sasa hakuna dalili yoyote ya kupatikana sukari kwa maeneo mengi nchini.Uamuzi wa kuzuia sukari kuagizwa nchi ulifanywa kwa kukurupuka bila kujipanga.

Kwenye kujadili hili swala la sukari tunatakiwa kuweka itikadi za vyama pembeni ni swala la muhimu sana watu wanateseka kutokana watu kufanya maamuzi ya kukurupuka bila kujipanga.

Tunataka kujua Sukari iliyoagizwa na Serikali iko wapi?

Bahati nzuri mie nina shamba langu la miwa,,,,deile nakata miwa kama miwili hivi,,,,natwanga napata juis saaafi,,,,,,,,wala sipati taabu tena.
Eti, kwani sukari shilingi ngapi sasa........???????!!!!!😉😉😉😛😛😛😛
 
Hapa mwembe
Arusha sukari kilo 3500 bado hapatikani[/QUOTE]
Dodoma jana nimenunua kg35 000 nikajiuliza sana! Alaf kabla kuuziwa kwanza unaangaliwa uson then ndo anakuuzia yana kama unaziwa madawa ya kulevya
 
Mi nilishangaa Waziri Mkuu anasema Serikali imeingiza sukari jana..wakati michakato ya kusafirisha inaweza kuchukua wiki mbili nikajua zile ni fix..Ila naomba mnisaidie hivi ni taasisi gani ya serikali ndio ilikuwa inauza na kugawa ile sukari na kwa njia zipi?
 
Arusha sukari kilo 3500 bado hapatikani
Dodoma jana nimenunua kg35 000 nikajiuliza sana! Alaf kabla kuuziwa kwanza unaangaliwa uson then ndo anakuuzia yana kama unaziwa madawa ya kulevya[/QUOTE]
Sukari imeshakuwa dili .kilo 3500 mpaka dodoma?
 
Bahati nzuri mie nina shamba langu la miwa,,,,deile nakata miwa kama miwili hivi,,,,natwanga napata juis saaafi,,,,,,,,wala sipati taabu tena.
Eti, kwani sukari shilingi ngapi sasa........???????!!!!!😉😉😉😛😛😛😛
Sukari imeshakuwa dili kilo unaweza kununua hata 5000
 
Kwani yako wapi makontena yalokamatwa.? Wapi magodauni yalobainika kuficha sukari, tuliona kwa kideo yamekamatwa na tukaahidiwa kugaiwa bure....😉
Ile sukari tuliambiwa ipo mbagala baadaye iligundulika sukari aliyekuwa nayo alikuwa na vibali vyake halali .Endeleeni kusubiri mtapewa bure ha ha
 
Na kama sarakasi hizi zikizidi kuendelae tutakumbuka sana kule msoga
 
Da! Afadhil ww mkuu ss na huu mfungo sijui itakuaje yan apa nataka ni bebe asal kwa wingi to
Tuendelee kusubiri ile ya bure tuliambiwa na Baba Jesca
 
Tutamkumbuka sana pamoja na udhaifu wake lakini alikuwa hakurupuki kama huyu
Na kama sarakasi hizi zikizidi kuendelae tutakumbuka sana kule msoga
 
kwa kweli
watuambie tamu yetu iko wapi
juzi nimeuziwa sukari nyeupe kama chumvi
hadi vijiko kumi kwenye kikombe ndio chai inanyweka
 
Back
Top Bottom