Salim tevez
JF-Expert Member
- Apr 21, 2016
- 394
- 182
Nasema serikali hii changa la macho watanzania tujifunze
Kwahiyo ukikutwa umevaa nguo ya mtumba sijui utapewa adhabu gani. Nawaza tu...Na bado, kuna waziri nani huyu sijui nae katia mkwara kuzuia nguo za nje kuanzia January mwakani. Najenga picha itakuwaje ikiwa upungufu wa nguo utaanza pia.... #SerikaliYaMwendokasi.
Ngoja mimi niende kwenye barabara za mwendo kasi labda nitapata jamaa mwenye gari kaingilia barabara ya mwendo kasi nimkamate nijipatie matairi nikayauze jioni nipoze koo
Ngoja mimi niende kwenye barabara za mwendo kasi labda nitapata jamaa mwenye gari kaingilia barabara ya mwendo kasi nimkamate nijipatie matairi nikayauze jioni nipoze koo
mtaaani ninako ishi baada ya zile kauli za mkuu wa kaya kua sukari itayokamatwa ikiwa mafichoni kugawiwa bure wazee walishangilia mnooo na kujipanga kupata mgao wao wa sukari kwani mkuu kasema itagawiwa bureeee,leo napokutana nao hawa wazee nikiwauliza wamepata kilo ngapi za sukari naambulia matusi ya nguoni.viongozi wanaamini kua raia hawatunzi kumbukumbu za kila wanacho ambiwa ndio maana viongozi hukurupuka tuuu na matamkoo yasiyo tekelezeka.
Nimeishia kucheka chai inaagizwa PakistanMsiwe na haraka sukari iliyoagizwa imeshawasili kwa vile serekali ya awamu hii (mwendokasi) inawajali sana wananchi wake hasa masikini tumeamua tuwapikie chai kabisa so tumeagiza majani ya chai toka Pakistan. Andaeni vikombe kabisa majani yakija mtakunywa chai
Hii awamu ina mambo yasiyoeleweka mnooo,na kwa nini waagize sukari kutoka nchi za mbali?,Rwanda wananunua sukari Mazabuka Zambia na Dwangwa Malawi,Ndiyo tenda anayofanya GSM GALCO,kuchukua sukari Zambia na Malawi na kuipeleka Rwanda,kwa nini serikali yetu isinunue sukari hapa jirani kama wenzetu,ambako ndani ya siku kumi gari zinakua zimekwenda na kurudi!!!!.WANA JF HESHIMA KWENU WOTE
Kwa muda sasa kumekuwa na tatizo la sukari kutopatikana maeneo mengi kutokana uamuzi wa serikali kuzuia vibali vya kuagiza sukari bila kujipanga.
Mwenzi uliopita Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa tani 11,957 ambazo serikali imeagiza zilikuwa zimeshawasili na kwamba hiyo sukari ingeuzwa kwa bei elekezi kilo 1800. Kuhusu tani zingine 240000 za sukari zingewasili ijumaa mei 13 na hadi zitoke bandarini ingekuwa jumapili na usambazaji ungefanya mei 16.
Pia tuliambiwa tani 20000 zingewasili mwisho wa mwenzi uliopita au mwanzoni mwenzi huu. Mpaka sasa hakuna dalili yoyote ya kupatikana sukari kwa maeneo mengi nchini.Uamuzi wa kuzuia sukari kuagizwa nchi ulifanywa kwa kukurupuka bila kujipanga.
Kwenye kujadili hili swala la sukari tunatakiwa kuweka itikadi za vyama pembeni ni swala la muhimu sana watu wanateseka kutokana watu kufanya maamuzi ya kukurupuka bila kujipanga.
Tunataka kujua Sukari iliyoagizwa na Serikali iko wapi?