Iko wapi sukari iliyoagizwa serikali?

Emma.

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
19,932
5,560
WANA JF HESHIMA KWENU WOTE

Kwa muda sasa kumekuwa na tatizo la sukari kutopatikana maeneo mengi kutokana uamuzi wa serikali kuzuia vibali vya kuagiza sukari bila kujipanga.

Mwenzi uliopita Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa tani 11,957 ambazo serikali imeagiza zilikuwa zimeshawasili na kwamba hiyo sukari ingeuzwa kwa bei elekezi kilo 1800. Kuhusu tani zingine 240000 za sukari zingewasili ijumaa mei 13 na hadi zitoke bandarini ingekuwa jumapili na usambazaji ungefanya mei 16.

Pia tuliambiwa tani 20000 zingewasili mwisho wa mwenzi uliopita au mwanzoni mwenzi huu. Mpaka sasa hakuna dalili yoyote ya kupatikana sukari kwa maeneo mengi nchini.Uamuzi wa kuzuia sukari kuagizwa nchi ulifanywa kwa kukurupuka bila kujipanga.

Kwenye kujadili hili swala la sukari tunatakiwa kuweka itikadi za vyama pembeni ni swala la muhimu sana watu wanateseka kutokana watu kufanya maamuzi ya kukurupuka bila kujipanga.

Tunataka kujua Sukari iliyoagizwa na Serikali iko wapi?
 
WANA JF HESHIMA KWENU WOTE

Kwa muda sasa kumekuwa na tatizo la sukari kutopatikana maeneo mengi kutokana uamuzi wa serikali kuzuia vibali vya kuagiza sukari bila kujipanga.
Mwenzi uliopita Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa tani 11,957 ambazo serikali imeagiza zilikuwa zimeshawasili na kwamba hiyo sukari ingeuzwa kwa bei elekezi kilo 1800.
Kuhusu tani zingine 240000 za sukari zingewasili ijumaa mei 13 na hadi zitoke bandarini ingekuwa jumapili na usambazaji ungefanya mei 16.
Pia tuliambiwa tani 20000 zingewasili mwisho wa mwenzi uliopita au mwanzoni mwenzi huu.
Mpaka sasa hakuna dalili yoyote ya kupatikana sukari kwa maeneo mengi nchini.Uamuzi wa kuzuia sukari kuagizwa nchi ulifanywa kwa kukurupuka bila kujipanga.
Kwenye kujadili hili swala la sukari tunatakiwa kuweka itikadi za vyama pembeni ni swala la muhimu sana watu wanateseka kutokana watu kufanya maamuzi ya kukurupuka bila kujipanga.
Tunataka kujua sukari iliyoagizwa na serikali iko wapi?
No comment!
 
Sie huku tunatumia sukari inatengezwa na ndizi kikojozi.wala hatuna hofu
 
Walisema hayo kutuliza munkari wa wananchi baada ya kushindwa kuwapa sukari ya bure waliyo waahidi.
 
Na bado, kuna waziri nani huyu sijui nae katia mkwara kuzuia nguo za nje kuanzia January mwakani. Najenga picha itakuwaje ikiwa upungufu wa nguo utaanza pia.... #SerikaliYaMwendokasi.
 
Pia tuliambiwa tani 20000 zingewasili mwisho wa mwenzi uliopita au mwanzoni mwenzi huu.
Mwanzo wa mwezi huu bado haujaisha:D:D:D

Labda watuambie wanatujali sana na hii ilikuwa motisha kwa wananchi kwenda na lishe bora kwa kupunguza matumizi ya sukari, kuna magonjwa kama kisukari, presha kwa namna moja ama nyingine yanachangiwa na matumizi mabaya ya sukari:rolleyes:
 
Hizo tani 11,957 ambazo tuliambiwa zimeshaingia nchi ziko wapi?
 
Na bado, kuna waziri nani huyu sijui nae katia mkwara kuzuia nguo za nje kuanzia January mwakani. Najenga picha itakuwaje ikiwa upungufu wa nguo utaanza pia.... #SerikaliYaMwendokasi.
Serikali ya kukurupuka wanazuia vitu kuingizwa nchi bila kuwa njia mbadala wa kuziba hilo pengo
 
Back
Top Bottom