Iko wapi kauli ya vizuri huwa havidumu?

Nsennah

JF-Expert Member
Jan 9, 2021
1,509
974
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano,

Nipo hapa kuwakumbusha kauli inayotawala miongoni mwa watu, VIZURI HUWA HAVIDUMI. Nimelileta kwenu kutokana na mijadala inayoendelea ya kumuattack hayati JPM.

Wapo wanaoshangilia mpaka leo kuwa yule kuondoka ni kusudio la Mungu kuwaepusha na balaa (iko wapi kauli hiyo?)
Rejea vifo kama vya J.K, KANUMBA, MAALIM, wote walitangulia na tukasema vizuri huwa havidumu, kwa nini kizuri kingine hakikudumu lakini mnabadilika na kukichafua kila kukicha?

JPM R.I.P japo watanzania wengi wanakukumbuka sana, na Mungu asituadhibu kwa kauli mbaya tunazotoa juu yako. Utaratibu huwa ni kumuombea marehemu lakini wanasiasa uchwara uliowaadhibu wanajitahidi kukuchafua japo ulishatangulia mbele za haki.

Iko wapi kauli ya vizuri huwa havidumu? Kama JPM alikuwa mbaya kwa nini hakudumu? Kifa chako wanaona ni majibu ya M/Mungu ktk vilio vyao ila kifo cha Maalim Seif n.k hawaoni kama majibu bali wakati wake ulifika.

Tuwe na akiba ya maneno, siasa isitutoe kwenye reli ya utamaduni wetu. Madhaifu yake tumuombee asamehewe na mazuri yake tuyaenzi. VIZURI HUWA HAVIDUMU japo najua ni chungu kwenye vinywa vya watu waliotikiswa na mwamba.

Tumuache apumzike maana ni kipenzi cha wengi kama huamini weka kipengele hicho kwenye sensa ya 2022 kuwa jibu NDIYO au HAPANA ( JPM mnamiss?) Halafu tukutane kwenye majumuisho.
 
Mkuu usipate presha.

Wanavyomsema ni uthibitisho huyu mzee alikuwa HATARI. imagine watu bado wanapambana na Marehemu, wanakomaza shingo utafikiri yupo hai.Magufuli alikuwa tishio aise!! Wa wanabwabwaja wakubwa kwa wadogo hadi mate yanawatoka kumbe mzee wetu ameshakwisha pumzika my dear dah



May his soul continue resting in eternal peace.
 
Mkuu usipate presha.

Wanavyomsema ni uthibitisho huyu mzee alikuwa HATARI. imagine watu bado wanapambana na Marehemu, wanakomaza shingo utafikiri yupo hai.Magufuli alikuwa tishio aise!! Wa wanabwabwaja wakubwa kwa wadogo hadi mate yanawatoka kumbe mzee wetu ameshakwisha pumzika my dear dah



May his soul continue resting in eternal peace.
Nakumbuka baada ya ule moshi kule Ruangwa! Zitto alitoka na habari kuwa mzee kakata na akampost Samia huko twiter akikagua gwaride akisema sasa ni zamu yako! Baada ya siku 3 akaibuka na nyimbo ya Goodluck -Hauwezi kushindana! Zitto kabwe akaomba radhi! Ila leo kageuka tena!

Inawezekana Diwani Athuman alilala! Ila kuna ukweli kulikuwa na mpango wa wazi nyuma ya pazia ukiendelea.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom