Jamiitrailer
Senior Member
- Oct 20, 2019
- 161
- 382
Habari wakuu
Watu wengi wameandika kuhusu ajenda ya Chadema ya kutaka uwepo wa mabadiliko katika taratibu na sheria zinazosimamia chaguzi zetu kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Wengine wanaunga mkono ajenda ya Chadema,na wengine wanaunga mkono lakini wakisema hakuna muda wa kutosha kati ya sasa na October, na wengine kama Paschal Mayala wanakejeli wakisema ajenda waliyokuja nayo Chadema ni UTOPIA...dhana isiyoweza kutekelezaka...na akaenda mbali zaidi kwa kusema kwamba Chadema imekuwa na fursa nyingi za kushinda chaguzi huko nyuma wakati CCM ikiwa dhaifu lakini hawakushinda kwa vile tu HAWAKUJIPANGA.
Anachomaanisha Mayala ni kwamba CCM ilishinda japo ilikuwa haina mvuto kwa wapiga kura kwa vile tu ilijipanga.
Nnachotaka kumueleza Mayala na wenzie wenye mtazamo huo kwamba SISI WAPIGA KURA tuliliona hilo jambo muda mrefu...na TULIELWEA kwamba kujipanga huko kwa ccm kunatokana sababu moja tu....,WATENDAJI WOTE WANAOSIMAMIA MFUMO WA UCHAGUZI ni wateule wa rais/mwenyekiti wa CCM..na wanawajibika kwake.
Mifano ni mingi sana na inaeleweka....tuchukue mfano..,...uchaguzi wa mkuu 2010 kura za urais jimbo la Karatu aliongoza Dr. Slaa kwa mbali..ndicho kilichopo katika rekodi hata za tume yenyewe, lakini matokeo yaliyotangazwa na tume kwa umma yalionesha Kikwete kumshinda Slaa eneo hilo.
Mfano mwingine, uchaguzi mkuu 2015 matokeo ya urais eneo la Tunduma,Edward Lowassa alimshinda Magufuli kwa mujibu wa matokeo yaliyobabdikwa katika vituo vyote. Lakini matokeo ya tume ya uchaguzi taifa yaliyokuwa yakitangazwa katika TV yalionesha kinyume chake.
Sisi wananchi tuliiona hali hiyo na tukasema ili mgombea tunayemtaka ashinde hapana budi kufanyike mabadiliko makubwa ya mfumo mzima wa uchaguzi, hususan katiba kwa ujumla.
Kilichofanyika uchaguzi wa 2020,bila kutaja kilichofanyika mwaka jana katika serikali chaguzi za serikali za mitaa,..bila shaka mtu yeyote mwenye akili timamu ataungana na wananchi kutaka hayo mabadiliko.
Mabadiliko yanayohitajika ni kwa mapana yake ili kufaidisha wananchi na taifa kwa ujumla na siyo kwa maslahi ya vyama.
Kwa mfano, kwa vile hakuna kipengele kinachoruhusu mgombea binafsi,utakuta wagombea ambao wanapendwa na wananchi lakini hawatakiwi na vyama vyao kwa ubabe wa kichama...wananchi wanakosa mwakilishi makini.
Sisi wananchi tumekuwa tukivishangaa vyama vya siasa vya upinzani vinavyoshiriki chaguzi kila msimu katika mazingira ambayo hata mwendawazimu anajua,yanatoa upendeleo kwa chama tawala.
kwa Chadema kuja na hilo wazo la No reform,No election, kimsingi linagusa kile ambacho sisi wananchi tulikihitaji kwa muda mrefu....na ndo maana umeona muitikio wa wanachi umekuwa mkubwa.
Wenye mamlaka ya kutunza amani ya nchi hii wanatakiwa kujua jambo moja ....unaporuhusu wananchi kudhulumiwa haki zao siku hadi siku,...ile hasira ya kulipuka ikifika ,madhara yake yanakuwa makubwa....,kama Ivory coast ilipomchoka Bagbo, au Burkina Fasso ilipomchoka Campare kwa figisu zao
Sasa tusifike huko kwa vile hakuna watu wapole duniani...binadamu wote ni wanyama wendawazimu...ni suala la muda tu atalipuka kama volcano.
Kuna watu wamesema hoja ya mabadiliko kwa sasa imechelewa.
Sisi wananchi tunauliza imechelewa kwa nani....wakati sisi wenyewe wapiga kura hatuna haraka kihivyo..tuko tayari tuahirishe hata kwa mwaka miaka 2 lakini mabadiliko yafanyike.
Huyo mwenye HARAKA tunataka tujue ana harakia nini.