Ikiwezekana wale wanaoalikwa katika TV kufanya Uchambuzi wa kumhusu Hayati Magufuli wawe wanapimwa Akili zao Kwanza tafadhali

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
" Rais Dkt. Magufuli alikuwa ni Yesu wa duniani na nadhani hata Yesu Mwenyewe angekuwepo angemfurahia na Kuona kuwa kapata Mrithi wake kutoka Tanzania "

" Rais Dkt. Magufuli hukupenda kwenda nchi za Mabeberu Ulaya na Marekani ila China alienda "

" Rais Dkt. Magufuli ndiyo alikuwa Rais pekee Kupenda Kukosolewa kuliko wote waliopita "

" Rais Dkt. Magufuli ndiyo Rais pekee ambaye katika Uongozi wake hujawahi Kusikia Kumetokea Matukio makubwa na ya Kutisha kama Tawala zilizopita "

" Rais Dkt. Magufuli ndiyo kasababisha Kiwango cha Elimu Kuongezeka kwa Kasi nchini Tanzania pamoja na Vyuo Vikuu "

" Rais Dkt. Magufuli ametujengea Uwanja mkubwa wa Michezo huko Dodoma kama ambavyo Mzee Mkapa nae alitujengea huu wa Dar es Salaam
"

" Rais Dkt. Magufuli amefanya Mambo makubwa kuliko hata yaliyofanywa na Watangulizi wake akina Hayati Nyerere, Mzee Mwinyi, Hayati Mkapa na Mzee Kikwete "

Televisions Kubwa za Tanzania kuanzia TBC1, ITV, Channel Ten, Clouds Tv na Star Tv lizingatieni mno hili na kama mtakuwa mnawapima Kwanza Akili hao mnaowaalika Studioni Kwenu itapendeza zaidi kwani kuna wengine tumeshachoka sasa Kuvumilia Uwongo na Unafiki wao.

Na ieleweke kuwa All - Rounder siyo kwamba labda nakataa kuwa Marehemu hakuna alichofanya au hastahili Sifa la hasha hata Mimi nimeona Utendaji wake mzuri na wa Kiuthubutu wa Kuijenga Tanzania na Kutekeleza Miradi yenye Umuhimu, ila sipendi tu Chumvi na Sukari nyingi zinavyozidishwa katika Kumzungumzia Mambo ambayo ama hayapo au aliyashindwa Kiutendaji.
 
Kuna jamaa flani huwa ana alikwa TBC huwa naona tittle yake kuwa ni mchambuz wa maswala ya kisiasa aisee hyo bwana ni too much sio kwa mapambio yale mpaka anaboa ni dogo mmj ali pruniwa kwenye kura za maoni nafikiri ni Iringa mjini mfupi na sura ya upigajipigaji hivi
 
Hili ni bandiko Konki, barikiwa. Kuna yule mchambuzi sijui Mchang'ombe ni mwandishi wa habari anaongea kwa nguvu kama anagombana na hadhira, huyo ndo Zuzu kuliko the so called wachambuzi wote. Juzi kasema bila aibu Marehemu kabalance miradi, eti kilichojengwa Songea ndo kilichoko Tanga, kilichojengwa Chato ndo kilichoko Iramba.
 
Siku zote madikteta hutawala kwa kubagua baadhi ya watu/makundi fulani katika jamii na kuyapendelea makundi mengine!
Kinacho tokea baada ya hapo; wale wanufaika! Watamsifia sana na kumtukuza daima huyo Dikteta wakati na hata baada ya kifo chake! Na wale watengwa/walio baguliwa/walioteswa, kudhulimiwa, kuonewa, nk. watamlaani milele mtu wa aina hiyo.

Jambo hili limetokea Iraqi chini ya Saddam Husein, Libya chini ya Muammar Gaddaf, Uganda chini ya Idd Amini Dada, Ujerumani chini ya Adolf Hitler, Italia chini ya Benito Musolini, na sasa linashuhudiwa pia Tanzania! Ingawa huyu wa kwetu alikuwa ni Dikteta Uchwara (according to Tundu Antipas Lissu)
 
Back
Top Bottom