SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 43,707
- 60,760
Na ushahidi pekee walio nao upande wa Jamhuri ni hayo maelezo yanayobishaniwa, yakikataliwa hamna kesi tena,DPP ataamua tu kuiondoa kesi mahakamani.Leo ni maamuzi ya nusu kesi, na kulingana na umuhimu wa rulling ya leo kama maelezo ya washtakiwa mahakama ikubali kuyatumia kwenye kesi, maelezo hayo yatakuwa na umuhimu mkubwa kuonesha ni upande upi utakuwa mshindi siku ya hukumu ya mwisho.
Kama yatakubaliwa, jamhuri watakuwa kwenye nafasi nzuri; japo binafsi siamini kama hili linawezekana kulingana na mazingira yaliyogubika zoezi zima kuanzia kuwakamata watuhumiwa mpaka kuchukua maelezo toka kwa washtakiwa, palikuwa na matendo mengi yaliyokiuka sheria na haki za binadamu kwa ujumla.
Endapo yatakataliwa na mahakama, upande wa washtakiwa watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kushinda kesi siku ya mwisho, hili litasababishwa na upande wa jamhuri kupoteza moja ya ushahidi wao muhimu kwenye kesi husika.
Kukubaliwa na mahakama au kutokubaliwa kwa vielelezo vya leo kuna nafasi kubwa kwenye kuamua kama hukumu ya mwisho itakuwa ya haki, au isiyo ya haki.