Ikiwa leo ni hukumu ya Mbowe na wenzake, anatukumbusha mwandishi huyu wa 1980

Leo ni maamuzi ya nusu kesi, na kulingana na umuhimu wa rulling ya leo kama maelezo ya washtakiwa mahakama ikubali kuyatumia kwenye kesi, maelezo hayo yatakuwa na umuhimu mkubwa kuonesha ni upande upi utakuwa mshindi siku ya hukumu ya mwisho.

Kama yatakubaliwa, jamhuri watakuwa kwenye nafasi nzuri; japo binafsi siamini kama hili linawezekana kulingana na mazingira yaliyogubika zoezi zima kuanzia kuwakamata watuhumiwa mpaka kuchukua maelezo toka kwa washtakiwa, palikuwa na matendo mengi yaliyokiuka sheria na haki za binadamu kwa ujumla.

Endapo yatakataliwa na mahakama, upande wa washtakiwa watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kushinda kesi siku ya mwisho, hili litasababishwa na upande wa jamhuri kupoteza moja ya ushahidi wao muhimu kwenye kesi husika.

Kukubaliwa na mahakama au kutokubaliwa kwa vielelezo vya leo kuna nafasi kubwa kwenye kuamua kama hukumu ya mwisho itakuwa ya haki, au isiyo ya haki.
 
Yaani jimbo la hai na wilaya ya hai lina watu wajanja wajanja sana sabaya jela mbowe naye mtego unaweza ukanasa wakati wowote
 
Mkuu the Big Eagle , kwanza asante kwa kutukumbusha "Mwandishi Huyu wa 1980s", kitendo cha kutomtaja ni mwandishi gani, wa wapi na maneno hayo aliyaandika wapi, sio tuu unakuwa hujawatendea haki wasomaji, bali unakuwa hukitendei haki, chombo chetu cha utoaji haki kwa ku insinuate kuwa uamuzi umeisha fanyika hivyo hii kesi ni kesi tuu ya kubambikiza kuhalalisha, kitu ambacho sio kweli na sio kitu kizuri.

Maandishi yoyote yaliyoandikwa na kuwa printed, hii ni kazí ya mtu, inaitwa, literacy work, hivyo kazí zote za uandishi, maandishi, zinalindwa na sheria ya copy right law, mtu huwezi kujichukulia tuu na kutumia bila idhini ya mhusika, ukitumia au uki quote sehemu kazi ya maandishi yoyote bila idhini ya publisher ni wizi tuu wa plagialism na unachukuliwa kama mwizi mwingine yoyote.

Namna ya kutumia kazí ya maandishi yoyote kwa nia njema bila kuonekana mwizi ni kwa kutoa kitu kinachoitwa attribution, unatoa credits ya kule uliko yachukua hayo maandishi.

Hivyo na wewe leo umefanya wizi wa plagiarisim, wewe ni plagialist, ume plagialize andishi kutoka ukurasa wa 163, kwenye kitabu cha Summons - Poems from Tanzania , kilichochapishwa na Tanzania Publishing House (TPH) ya Dar Es Salam, mwaka 1980.

Acha wizi!
P
 
Leo ni siku muhimu sana kwa haki. Kama itampendeza mheshimiwa jaji kutupilia mbali pingamizi kutoka upande wa utetezi basi ina maana:

1. Atakuwa amejiridhisha kuwa mshitakiwa wa pili alitoa maelezo yake kwa Kingai ndani ya masaa 4 tokea kukamatwa kama sheria inavyoelekeza.

2. Jaji atakuwa amejiridhisha pasi na shaka kuwa mshitakiwa wa pili aliyatoa maelezo yake kwa Kingai kwa mujibu wa sheria na bila kuwepo na shinikizo lolote.

Wonders shall never end.

Macho yetu kwake Mheshimiwa Jaji Kiongozi.
 
Mkuu the Big Eagle , kwanza asante kwa kutukumbusha "Mwandishi Huyu wa 1980s", kitendo cha kutomtaja ni mwandishi gani, wa wapi na maneno hayo aliyaandika wapi, sio tuu unakuwa hujawatendea haki wasomaji, bali unakuwa hukitendei haki, chombo chetu cha utoaji haki kwa ku insinuate kuwa uamuzi umeisha fanyika hivyo hii kesi ni kesi tuu ya kuuhalalisha, kitu ambacho sio kizuri.
P
Kwenye kesi ya Dumisani Dube Vs Republic, kwa kifo cha Skoine kwa ajali ya gari kule Morogoro, kesi ilikuwa hivi:

Siku ya kwanza, Mashitaka matano kwa Dumisani Dube yalitajwa mahakamani
Dumisani Dube alikataa kabisa kuhusika na - Kesi iliahirishwa
Mara ya pili Mashitaka yale yale yalitajwa Dumisani Dube akakubali Makosa Yote, na alihukumiwa miaka 5 jela..
Wananchi tulishangaa lakini tulikubali,
Baada ya miezi kadhaa, Dumisani Dube aliibukia London,
Ameishi huko hadi Africa Kusini inapata Uhuru, akarudi Africa Kusini, akapewa na cheo, kama nilisikia alifariki, labda nipekue tena.

Paskali, hii ndiyo Tanzania, "communist" kantri, uongo mwingi, laghai wengi, na hii ndiyo tabia CCM imetuhusisha, tutaamini kila kitu, kwa sababu kila kitu tunafanya kuaminishwa ingawa hatuamini.

Labda CCM ifutwe hapo baadaye, lakini uwepo wake hakuna mabadiriko yatakayotokea kwenye "mindset" ya waTangnganyika.

We fought JK, then Magu, now Samia; but we forget that these also are victims of the system, the system which they can manipulate to their advantages, WE have to fight CCM - The System providers
 
Washitakiwa walipigwa,waliteswa,walikaa na njaa kwa Siku 10,walilazwa chumba chenye maji,walitundikwa Kama popo,walichomwa na bisibisi, walipigwa nyayo za miguu,walihamishwa vituo vya polisi central, tazara, mbweni walipewa majina bandia kisha wakalazimishwa kusaini maelezo chini ya mtutu wa bunduki huku mwenzao MOSES LIJENJE akiwa ameuwawa kwa mateso makari. Leo Jaji ameteuliwa kuwa jaji kiongozi inatia Shaka cheo hicho. Haina haja ya kumuomba mungu ila ahadi pekee Ni kuwa haki isipotendeka mahakamani italazimika kutafutwa nje ya mahakama.
 


We fought JK, then Magu, now Samia; but we forget that these also are victims of the system, the system which they can manipulate to their advantages, WE have to fight CCM - The System providers
Mkuu Interested Observer , kwanza asante kwa kumbukumbu hii ya Dumisani Dube, japo kumbukumbu yangu inaniambia kifungo ni miaka 6 na sio miaka 5. Sheria zinaruhusu mkimbizi kutumikia kifungo chake kwenye jela ya nchi nyingine yoyote, hivyo Dumisani Dube, alichagua UK.

Hicho ulichokisema "WE have to fight CCM - The System providers", ni maneno makali na umeyatamka kwa uchungu toka moyoni na nafsini kwako. Kwanza nikupe pole, kisha nikujulishe, to fight CCM is a mistake na ndilo kosa kubwa pekee linalofanywa na upinzani Tanzania na ndio maana wakiendelea kufanya kosa hili, siku zote, Ikulu wataendelea kuishia kuisikia tuu kwenye bomba, na CCM itaendelea kutawala Tanzania milele na milele!.

Hii kauli ya "WE have to fight CCM" kwa kudhani CCM is "The System providers" is wrong, kwa Tanzania, CCM is not a systém provider, CCM is the systém!. Huu ndio ukweli wenyewe japo ni ukweli mchungu, lakini ndio ukweli.

Kanisome hapa ndipo utaelewa adui wa kweli wa nchi hii sio CCM!.
P
 
Inashangaza sana kuona mtuhumiwa anachagua jaji anayemtaka asikilize kesi yake.

Je, inaruhusiwa kisheria kwa mtuhumiwa kuchagua Jaji anayemtaka ili asikilize kesi yake?
 


Endapo yatakataliwa na mahakama, upande wa washtakiwa watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kushinda kesi siku ya mwisho, hili litasababishwa na upande wa jamhuri kupoteza moja ya ushahidi wao muhimu kwenye kesi husika.
Mkuu denooJ , hiki ndicho kinachokwenda kutokea Mama hapendi hizi mambo, ushahidi utakataliwa kesi itafutwa, ila karma ya wahusika wote haitafutika bali itakula kichwa!.
P
 
inashangaza sana kuona mtuhumiwa anachagua jaji anayemtaka asikilize kesi yake!!
je inaruhusiwa kisheria kwa mtuhumiwa kuchagua Jaji anayemtaka ili asikilize kesi yake?
Hairuhusiwi popote, kinachoruhusiwa ni mtuhumiwa kumkataa jaji yoyote akijihisi hana imani naye na hata tendewa haki. Jaji atabadilishwa ila sio mtuhumiwa kuchagua aje nani.
P
 
Back
Top Bottom