Ikiwa leo ni hukumu ya Mbowe na wenzake, anatukumbusha mwandishi huyu wa 1980

Mkuu pascal, kwa hiyo hapo unatuambia kuwa mama naye ana seat yake kwenye maamuzi ya kesi hii?
Mama si walishamuingiza mkenge kwamba wenzanke Mbowe wameshahukumiwa na wanatumikia vifungo vyao wakati ni uwongo mtupu?

Unadhani mama analifurahia hilo kuonekana kituko mbele ya media kubwa iliyomfanyia exclusive interview kama BBC?

Ukimuuliza mama leo hao waliohukumiwa wapo jela ipi na case namba ipi na nakala ya hukumu iko wapi anayo majibu?

Watu wenye guts za kumdanganya Rais wataogopa kuudanganya umma?
 
Mkuu Interested Observer , kwanza asante kwa kumbukumbu hii ya Dumisani Dube, japo kumbukumbu yangu inaniambia kifungo ni miaka 6 na sio miaka 5. Sheria zinaruhusu mkimbizi kutumikia kifungo chake kwenye jela ya nchi nyingine yoyote, hivyo Dumisani Dube, alichagua UK.

Hicho ulichokisema "WE have to fight CCM - The System providers", ni maneno makali na umeyatamka kwa uchungu toka moyoni na nafsini kwako. Kwanza nikupe pole, kisha nikujulishe, to fight CCM is a mistake na ndilo kosa kubwa pekee linalofanywa na upinzani Tanzania na ndio maana wakiendelea kufanya kosa hili, siku zote, Ikulu wataendelea kuishia kuisikia tuu kwenye bomba, na CCM itaendelea kutawala Tanzania milele na milele!.

Hii kauli ya "WE have to fight CCM" kwa kudhani CCM is "The System providers" is wrong, kwa Tanzania, CCM is not a systém provider, CCM is the systém!. Huu ndio ukweli wenyewe japo ni ukweli mchungu, lakini ndio ukweli.

Kanisome hapa ndipo utaelewa adui wa kweli wa nchi hii sio CCM!.
P
Hakuna mtu anajielewa atakubaliana na wewe.ADUI MKUU WA DEMOCRACY NA HAKI HAPA TZ NI CCM.
Nani anavuruga chaguzi kwa kuiba kura?
Nani aneelekeza vyombo vya dola kama polisi kuvuruga mikutano ya wapinzani?
Nani anacontrol utendaji wa tume ya uchaguzi?
Mambo ni mengi yanayofanywa na wewe paschal unajua,sema tu machoni pako kuna kitambaa cha kijani kinakuzuia kuona hivyo unalazimika kuhamisha mjadala kwa kuwaangushia zigo watanzania wote.
 
Washitakiwa walipigwa,waliteswa,walikaa na njaa kwa Siku 10,walilazwa chumba chenye maji,walitundikwa Kama popo,walichomwa na bisibisi,walipigwa nyayo za miguu,walihamishwa vituo vya polisi central,tazara,mbweni walipewa majina bandia kisha wakalazimishwa kusaini maelezo chini ya mtutu wa bunduki huku mwenzao MOSES LIJENJE akiwa ameuwawa kwa mateso makari.Leo Jaji ameteuliwa kuwa jaji kiongozi inatia Shaka cheo hicho.Haina haja ya kumuomba mungu ila ahadi pekee Ni kuwa haki isipotendeka mahakamani italazimika kutafutwa nje ya mahakama.

Haki ikitendeka kila mtu atajua. Kwani huyu bibi hajajua kuwa haki ilitendeka?

inashangaza sana kuona mtuhumiwa anachagua jaji anayemtaka asikilize kesi yake!!
je inaruhusiwa kisheria kwa mtuhumiwa kuchagua Jaji anayemtaka ili asikilize kesi yake?

Hivi mshitakiwa kamchagua jaji yupi?
 
inashangaza sana kuona mtuhumiwa anachagua jaji anayemtaka asikilize kesi yake!!
je inaruhusiwa kisheria kwa mtuhumiwa kuchagua Jaji anayemtaka ili asikilize kesi yake?
... mtuhumiwa yupi kamchagua jaji?
 
The trial​

Finally,
The judge will take his place
And the accused,
The complainant
And the onlookers:
All will know where to be - and
Justice will be meted out
Even before the trial.
Kwahiyo ndani ya mahakama kuna watu wataingia wakiwa hawajui hukumu na wamo ambao wanaingia huku tayari walikwisha ijua hukumu! One people two countries apart.
 
Kwenye kesi ya Dumisani Dube Vs Republic, kwa kifo cha Skoine kwa ajali ya gari kule Morogoro, kesi ilikuwa hivi:

Siku ya kwanza, Mashitaka matano kwa Dumisani Dube yalitajwa mahakamani
Dumisani Dube alikataa kabisa kuhusika na - Kesi iliahirishwa
Mara ya pili Mashitaka yale yale yalitajwa Dumisani Dube akakubali Makosa Yote, na alihukumiwa miaka 5 jela..
Wananchi tulishangaa lakini tulikubali,
Baada ya miezi kadhaa, Dumisani Dube aliibukia London,
Ameishi huko hadi Africa Kusini inapata Uhuru, akarudi Africa Kusini, akapewa na cheo, kama nilisikia alifariki, labda nipekue tena.

Paskali, hii ndiyo Tanzania, "communist" kantri, uongo mwingi, laghai wengi, na hii ndiyo tabia CCM imetuhusisha, tutaamini kila kitu, kwa sababu kila kitu tunafanya kuaminishwa ingawa hatuamini.

Labda CCM ifutwe hapo baadaye, lakini uwepo wake hakuna mabadiriko yatakayotokea kwenye "mindset" ya waTangnganyika.

We fought JK, then Magu, now Samia; but we forget that these also are victims of the system, the system which they can manipulate to their advantages, WE have to fight CCM - The System providers
Do you really know who is the system provider? Until you know.....
 
Hakuna mtu anajielewa atakubaliana na wewe.ADUI MKUU WA DEMOCRACY NA HAKI HAPA TZ NI CCM.
Nani anavuruga chaguzi kwa kuiba kura?
Nani aneelekeza vyombo vya dola kama polisi kuvuruga mikutano ya wapinzani?
Nani anacontrol utendaji wa tume ya uchaguzi?
Mambo ni mengi yanayofanywa na wewe paschal unajua,sema tu machoni pako kuna kitambaa cha kijani kinakuzuia kuona hivyo unalazimika kuhamisha mjadala kwa kuwaangushia zigo watanzania wote.
Umesoma comment yote ya Ndugu Mayalla? Au umesoma nusu nusu na kukimbilia kujibu?
 
Mkuu the Big Eagle , kwanza asante kwa kutukumbusha "Mwandishi Huyu wa 1980s", kitendo cha kutomtaja ni mwandishi gani, wa wapi na maneno hayo aliyaandika wapi, sio tuu unakuwa hujawatendea haki wasomaji, bali unakuwa hukitendei haki, chombo chetu cha utoaji haki kwa ku insinuate kuwa uamuzi umeisha fanyika hivyo hii kesi ni kesi tuu ya kubambikiza kuhalalisha, kitu ambacho sio kweli na sio kitu kizuri.

Maandishi yoyote yaliyoandikwa na kuwa printed, hii ni kazí ya mtu, inaitwa, literacy work, hivyo kazí zote za uandishi, maandishi, zinalindwa na sheria ya copy right law, mtu huwezi kujichukulia tuu na kutumia bila idhini ya mhusika, ukitumia au uki quote sehemu kazi ya maandishi yoyote bila idhini ya publisher ni wizi tuu wa plagialism na unachukuliwa kama mwizi mwingine yoyote.

Namna ya kutumia kazí ya maandishi yoyote kwa nia njema bila kuonekana mwizi ni kwa kutoa kitu kinachoitwa accreditation, unatoa credits ya kule uliko yachukua hayo maandishi.

Hivyo na wewe leo umefanya wizi wa plagiarisim, wewe ni plagialist, ume plagialize andishi kutoka ukurasa wa 163, kwenye kitabu cha Summons - Poems from Tanzania , kilichochapishwa na Tanzania Publishing House (TPH) ya Dar Es Salam, mpaka 1980.

Acha wizi!
P
Paskali, unaonaje hii tuiite kesi ndogo iliyozaliwa na kesi ndogo chini ya kesi kubwa na tuipangie jaji.
 
Kwahiyo ndani ya mahakama kuna watu wataingia wakiwa hawajui hukumu na wamo ambao wanaingia huku tayari walikwisha ijua hukumu! One people two countries apart.
Hukumu ya Lema kuvuliwa ubunge ilivuja siku moja kabla, wote tuliijuwa hukumu kabla siku ya hukumu.

Nadhani mahakama imejifunza kitu katika kutunza siri, maana hata Sabaya licha ya watu wenye akili timamu kujuwa lazima afungwe lakini hakuna kilichovuja mpaka dakika ya mwisho.
 
Mama si walishamuingiza mkenge kwamba wenzanke Mbowe wameshahukumiwa na wanatumikia vifungo vyao wakati ni uwongo mtupu?

Unadhani mama analifurahia hilo kuonekana kituo mbele ya media kubwa iliyomfanyia exclusive interview kama BBC?

Ukimuuliza mama leo hao waliohukumiwa wapo jela ipi na case namba ipi na nakala ya hukumu iko wapi anayo majibu?

Watu wenye guts za kumdanganya Rais wataogopa kuudanganya umma?
Ulipotea sana mkuu...Nakusalimu
 
Hukumu ya Lema kuvuliwa ubunge ilivuja siku moja kabla, wote tuliijuwa hukumu kabla siku ya hukumu.

Nadhani mahakama imejifunza kitu katika kutunza siri, maana hata Sabaya licha ya watu wenye akili timamu kujuwa lazima afungwe lakini hakuna kilichovuja mpaka dakika ya mwisho.
Fahamu kuwa siku zote katika maisha siri huwa ni ya mtu mmoja, mkiwa wawili si siri tena.
Jaji akimuhusisha mtu wa pili kwenye uamuzi wake kuna uwezekano mtu wa pili akamueleza mkewe na mkewe akamueleza mama au baba awe mkwe au mzazi. Jaji pia huenda chini ya msukumo asioupenda anaweza akamueleza mkewe na mkewe akamueleza mama au baba mkwe au mzazi.
 
Msiri wa Jaji ni secretary wake, hakuna mtendaji yeyote ambaye hana mtu wa kumsaidia au kumrahisishia majukumu.

Kama upo mijini humu kwenye vibanda vya stationary unaweza kujuwa naongea nini, wale wana siri nyingi sana.

Hadi mawakili janjajanja wanachapisha mambo yao kwa hawa wa stationary za town.
 
Back
Top Bottom