Ijumaa iwe siku ya mapumziko: Nini ushauri wako?

The Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
11,100
Reaction score
13,698
Posted Wednesday, October 31 2012 at 22:52
IN SUMMARY
Mbunge wa chama cha upinzani anatoa mchango wake anaambiwa kaa chini hata kama ana mchango mzuri kiasi gani Spika akiwa kwenye chama fulani inaleta mpasukoalisema.
Pia alitaka Katiba Mpya iweke kifungu kitakachoilazimisha Tume ya Uchaguzi (NEC),

Hussein Nyari, Siha
MKAZI wa Kijiji cha Kikwe wilayani Siha, Halima Munisi ametaka katiba ijayo iitambue siku ya Ijumaa kuwa ni siku ya mapumziko kama zilivyo siku za Jumamosi na Jumapili.
Munisi alitoa pendekezo hilo juzi wakati akitoa maoni yake mbele ya kamati ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na Profesa Mwesiga Baregu.
Kwa mujibu wa mwananchi huyo, Ijumaa kutokuwa ni siku ya mapumziko hasa kwa kuwa ndio siku ya kumuabudu Mola kwa Waislam si sahihi na kutaka siku hiyo iwe ya mapumziko.
Mkazi wa Kitongoji cha Nasai, Stanslaus Mallya alitaka katiba ijayo iweke kifungu ili Mawaziri watakaoteuliwa katika Baraza la Mawaziri wasiwe wabunge wa kuchaguliwa wala kuteuliwa.
Mallya alisema kitendo cha Mawaziri kushika kofia mbili ya Uwaziri na Ubunge, kinawafanya wasitekeleze majukumu yao ipasavyo hasa pale inapofikia mahali pa kuibana Serikali.
Kwa upande wake mkazi wa Ndoroso, Solomon Mmari alitaka Spika wa Bunge asiwe Mbunge na wala kuwa mfuasi wa chama chochote cha siasa ili aweze kutenda wajibu wake kwa haki.
Hoja hiyo iliungwa mkono na Radegunda Nyabu, mkazi wa Magadini Bomangombe ambaye alisema endapo Spika anatokana na chama cha siasa, kuna kila sababu ya kutoa upendeleo.
Mbunge wa chama cha upinzani anatoa mchango wake anaambiwa kaa chini hata kama ana mchango mzuri kiasi gani Spika akiwa kwenye chama fulani inaleta mpasukoalisema.
Pia alitaka Katiba Mpya iweke kifungu kitakachoilazimisha Tume ya Uchaguzi (NEC), kutopanga siku ya uchaguzi kwa siku zile ambazo zinatumika kumwabudu Mungu.
Kwa mujibu wa Nyabu, siku hizo ni Ijumaa kwa waumini wa Kiislam na Jumamosi na Jumapili kwa waumini wa Kikristo ili kila mmoja aweze kumwabudu na kumtukuza mola wake.
 
Hakuna aliyemzuia kupumzika yeye na familia yake hata kwa katiba ya sasa. Cha msingi watumishi wa umma wafanye kazi hadi saa 10.30 jioni halafu warudi nyumbani wakapumzike. Mimi huwa nafanya kazi Jumatatu hadi Jumapili, lakini pia huwa napumzika Jumatatu hadi Jumapili.

Mambo ya kufikiria kulala kwenye majamvi misikitini siku nzima ndio yanayotuletea umasikini
 
Tatizo Waislamu wamebaki kulumbana na utaratibu wa Wakristo na kusahau mafundisho ya dini yao!!! Kwani korani imeandika wapi kwamba Waislamu wanapaswa kupumzika ijumaa?? Nchi nyingine waislamu wanapumzika hiyo ijumaa? Huu nao ni ujuha mwingine!!
 
mmhh hao jamaa ni JANGA kuu la kitaifa,huo ni uvivu uliokithiri hawataki kufanya kazi tu hao
mbona JUMAPILI siku TAKATIFU hata wao hufunga maduka yao kariakoo na sehemu nyingine bila kuambiwa na mtu?
lakini hiyo siku yao ya IJUMAA wanaendelea na kazi kama kawaida lakini wanatenga muda tu wa kwenda kuswali?
mashindano na WAKRISTO hamtayaweza,mtaishia kulalama tu kuwa serikali inaendeshwa kwa MFUMO KRISTO huku mkijisahaulisha kuwa VIONGOZI WOTE WALIOSHIKA NYADHFA NYETI TANZANIA NI WAISLAM
naomba kuwasilisha na AMANI YA BWANA YESU KRISTO IWE NANYI NYOTE WENYE MAHANGAIKO,DAMU YA YESU ITAWAPONYA
 
umasikini uliletwa na siasa ya ujamaa nakujitegemea, mafisadi na sera za kuchukia nchi tajiri. Ujamaa uliwafutia wanamuziki hati miliki na wala hauukuwa na sera za kujenga studio za wanamuziki kufyatua santili. matokeo yake wnamuziki wengi waliishia kuwa masikini wakupwa.
 
Hakuna aliyemzuia kupumzika yeye na familia yake hata kwa katiba ya sasa. Cha msingi watumishi wa umma wafanye kazi hadi saa 10.30 jioni halafu warudi nyumbani wakapumzike. Mimi huwa nafanya kazi Jumatatu hadi Jumapili, lakini pia huwa napumzika Jumatatu hadi Jumapili.

Mambo ya kufikiria kulala kwenye majamvi misikitini siku nzima ndio yanayotuletea umasikini
umasikini hapa TZ umeletwa na siasa ya Ujamaa na kujitegemea, Mafisadi, mahakam kuu kutokuwa huru, kutaifisha mali za matajiri, na sera mbovu za kuchukia nchi Tajiri! Kwa nini siku hizi kuna hati miliki na sehemu za kurecodia muziki? Yanga na simbo zinaendeshwa kibiashara na kutoa ajira kwa vijana nzuri tuu, serikali haiingirii kuwafukuza makocha vilabuni kama walivyofanya kwa Tambwe Leya na Nabi Camara, watu wanaruhusiwa kuwa na mishahara miwili,kuboresha movies za kikwetu ambazo at list husaidia viaja wengi kujipatia pesa. Sasa kwa nini Ujamaa na kjtgmea ulikuwa hautaki haya yafanyike kwa wananchi? Yaani vitu hizi vimesaidia sana kuwapa kipato raia wetu.

HUyu mama hakufikiria production goals wala international communication net works. Kama ijumaa tukipumzika na halafu wiki hiyo kuna sikukuu either ya X-mass, au Iddi basi ziku za production zitakuwa mbili au moja kwa wiki. Halfu shughuli za kutumiana pesa kwa mtindo wa kisasa, wewe uko nje ya nchi unatuma ijumaa, halafu unaambiwa kuwa mabenki, western union yote yamefungwa kwa sababu leo ni siku ya mapumziko! Hizo pesa ambapo unatarajia zingemsaidia mgonjwa, au dhaman kwa nduguyo basi ungojee mpaka jumatatu!!!

Nchi masikini kama TZ kuwa na holiday nyingi si vizuri kwa sababu huykatiasha tamaa wawekezaji. Maana wanatuona ni wavivu.

Scoop! Unajua sisi watanzania tukazanie kitu kimoja kuhusu kulinda bidhaa zetu tutengenezazo Viwandani. Lazima kipengere cha "Protective policy for our own home grown goods &products"tungekuwa tuna policy hii, kiwanda cha bora kisinge kufa wala kilimanjaro na mang'ura machine tools navyo visingekufa kabisaa.

viwanda vingine kama scania pale Kibaha navyo vimejikuta vinakufa na kupoteza ajira za mamia ya watu, kwa sababu ya kuingiza nchini bidhaaa mabazo viwanda vyetu vinatengeneza. Madhara yake ni watu kupoteza kazi na kuja ishi maisha ya maharage mboga ya anasa na kambale mboga ya mgeni.

Jamani hii policy naomba sana tuichambue vizuri na kuibana serikari serikali itunze ajira za wananchi kwanza. hii kitu lazima iingie ktk katiba.
 
umasikini hapa TZ umeletwa na siasa ya Ujamaa na kujitegemea, Mafisadi, mahakam kuu kutokuwa huru, kutaifisha mali za matajiri, na sera mbovu za kuchukia nchi Tajiri! Kwa nini siku hizi kuna hati miliki na sehemu za kurecodia muziki? Yanga na simbo zinaendeshwa kibiashara na kutoa ajira kwa vijana nzuri tuu, serikali haiingirii kuwafukuza makocha vilabuni kama walivyofanya kwa Tambwe Leya na Nabi Camara, watu wanaruhusiwa kuwa na mishahara miwili,kuboresha movies za kikwetu ambazo at list husaidia viaja wengi kujipatia pesa. Sasa kwa nini Ujamaa na kjtgmea ulikuwa hautaki haya yafanyike kwa wananchi? Yaani vitu hizi vimesaidia sana kuwapa kipato raia wetu.

[/COLOR]

Naamini hata wewe mwenyewe hujui ulichokiandika hapa! Hivi kuna mahali au kanuni ya siasa ya ujamaa na kujitegemea iliyo ruhusu ufisadi??? Huu ni zaidi ya ujinga!
 
Hakuna aliyemzuia kupumzika yeye na familia yake hata kwa katiba ya sasa. Cha msingi watumishi wa umma wafanye kazi hadi saa 10.30 jioni halafu warudi nyumbani wakapumzike. Mimi huwa nafanya kazi Jumatatu hadi Jumapili, lakini pia huwa napumzika Jumatatu hadi Jumapili.

Mambo ya kufikiria kulala kwenye majamvi misikitini siku nzima ndio yanayotuletea umasikini

hahahahahahaha, aende somalia.
 
Heh, ndo ipi tena hiyo¿ Nahitaji.kwenda madrasa.
Ila mie sioni tatizo, tufanye weekend yetu ijumaa na jumamosi. Halafu jumapili tuingie kazini. Ila boss wangu akae akijua mie siasa kali, naingia church saa moja asubuhi hadi saa saba ndo ntaenda ofisini, manake na waislamu wakienda kuswali sie huwa tunaendelea na kazi bila kulalama.
Tubadilishe na kalenda hii ya sasa ni ya kikristo..ni muda wa kutumia ya kiislamu sasa
 
Back
Top Bottom