Ijue sheria (utaratibu wa kuhamisha umiliki wa ardhi)

chapangombe

JF-Expert Member
Sep 28, 2014
362
289
Kabla ujaingia Katika manunuzi ya nyumba au kiwanja omba kopi ya hati ukafanye official search kujilizisha kuwa kweli ni Mali harali ya muhusika

.kutembelea eneo husika kuangalia Kama halina changamoto ya kimazingira Kama vile kujaa maji au hapafikiki

kufatilia valuation report kujua uhalisia wa thamani ya eneo husika

Kujilizisha Kama nyumba haijaombewa mkopo

kujilizisha kuwa nyumba sio yenye mgogoro

Kujilizisha kuwa mke,au mume ametoa consent ya kuuzwa

kujilizisha kuwa nyumba haina mgogoro wa mirathi

kujilizisha kuwa eneo halipo Katika mipango ya serikali Kama vile shule,hosp,nk

kujilizisha kuwa anayeuza ndiyo mmiliki

Baada ya kujilizisha basi hatua inayofuata ni kuandaa mkataba wa kisheria ambao umeandaliwa na wakiki

Kuwepo na hakikisho la kulipwa kwa Kodi za eneo husika

Kuwepo na hakikisho la kulipwa kwa Kodi ya proparty tax

Kuwepo na hakikisho la kulipwa kwa Kodi ya capital gain tax

Lazima stamp duty ilipiwe

Kusajiri uhamishaji wa umiliki

Ofisi inayo husika ni ofisi ya msajiri wa nyaraka

Vitu vingine muhimu vina vyotakiwa ni pamoja na taarifa ya kiapo Cha kukubali kuuzwa na mwenza Kama umeoa

Kuwepo na taarifa ya ahadi lini utajenga kiwanja husika.

Fomu zinazotakiwa

F.29
F.30.
F.35
F.38
UShauri kumekuwepo na migogoro mingi ya ardhi kwa sababu ya watu kukwepa wataalamu Katika mchakato wa manunuzi hivyo kuingia kwenye migogoro ya kesi kwa gharama kubwa.

Hivyo ni UShauri wangu tafuta wataalamu Katika mchakato wa mauziano

NB. Mjumbe,mwenyekiti wa serikali,mtendaji sheria haiwatambui wasimamie zoezi la uuzwaji wa nyumba au kiwanja be aware

Thank

.
 
Mkuu,habari naomba mwongozo wako,kuna shamba lilikuwa la wazazi wangu ambalo nao walilirithi kutoka kwa wazazi wao(upande wa baba) sasa kutokana na kuwa shamba lile lilikuwa mbali na eneo tulilokuwa tukiishi hatukulitumia eneo hilo kwa muda.

Kisha baba yangu akaamua kumwazima mdogo wake wa kike alitumie kwa kilimo tu,muda ukaenda na kwa bahati mbaya sana yule shangazi yetu aliyeazimwa lile eneo akafariki dunia,shamba likabaki mikononi mwa mume wake, baada ya muda wazazi wetu wote nao walifariki,miezi kadhaa baada ya mzazi wetu wa mwisho kufariki tuliamua kufuatilia mashamba ya wazazi wetu,na hilo tajwa likiwemo.

Sasa cha kushtua ni kuwa yule mume wa marehemu shangazi yetu amegeuka na kudai kuwa shamba lile ni mali yake halali kwani mke wake alipewa kabisa na kaka yake kitu ambacho si kweli,zingatia kuwa makabidhiano yote yalikuwa yakifanyika kwa mdomo bila maandishi yoyote, msaada wako unahitajika hapo, tufanyeje ( kwa hatua za awali) ili tuweze kulirejesha eneo mikononi mwetu?

Nb hatukuwa na haja ya kulitumia eneo hilo siku za karibuni,tunachotaka ni kuwa yeye atuonyeshe kuwa anatambua kuwa shamba si mali yake na aonyeshe utayari wa kulirejesha kwa wamiliki pale atakapohitajika kufanya hivyo! Thanks in advance.
 
Mkuu,habari naomba mwongozo wako,kuna shamba lilikuwa la wazazi wangu ambalo nao walilirithi kutoka kwa wazazi wao(upande wa baba) sasa kutokana na kuwa shamba lile lilikuwa mbali na eneo tulilokuwa tukiishi hatukulitumia eneo hilo kwa muda...
Zipo taratibu unaweza kuanza nazo.

Moja unaweza ukaandikiwa notice ya kuliachia eneo Hilo kabla ya muda fulani la sivyo hatua za kisheria zitafuatwa barua inaandikwa na wakili

Hatua ya pili inategemea na thamani ya eneo lakini kama lipo chini ya milioni 3 nenda kafungue shauli Baraza la kata watamuita na nyinyi mtapeleka ushahidi na yeye ataleta ushahidi then haki itatolewa
 
Back
Top Bottom