Ijue nophone, kifaa cha bei rahisi kuliko nokia ya tochi

Ijue nophone, kifaa cha bei rahisi kuliko nokia ya tochi

Hii thread nimeiona leo tarehe 12-april. Yaani nimecheka sijui wazungu washatuona sisi maboya kabisa
watu 915 wamechangia zaidi ya dola 18,000 kickstarter kuwa watu vitu vya kijinga kama hivi wao ndio wanapenda.

 
yap hakiwaki wala hakifanyi chochote, na hio version ya selfie ni kioo tu kimebandikwa hivyo picha yako huwezi kuisave unajiangalia tu.

wanajisifia kwenye security sababu hamna mawasiliano yoyote yanayofanyika humo.

mfano ukienda kwa fundi seremala akakuchongea kipande cha mbao akakubandikia na kioo juu, je kuna mtu anaweza kukuspy kupitia kipande cha mbao?
Duh, natamani nijue hiko kifaa ukikifungua ndani utakutana na nini? Au ni empty?
 
watu 915 wamechangia zaidi ya dola 18,000 kickstarter kuwa watu vitu vya kijinga kama hivi wao ndio wanapenda.


Bora hata wangeweka kioo chenye saa au basic phone application. Hata kioo cha black n white kama motorola F3. au hata Keypad bila display.

Lakini sipati picha kutembea na kiPlastic ambacho kina michoro ya button, speaker, camera , mic, ports. Halafu unanunua UPGRADE ya Kioo na kukinatisha kwa juu.

[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji28] [emoji28]

motorola_f3_00.jpg
 
Hii nzuri kimeo kikikuomba no ya simu unakiambia natumia nophone
[emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28]

Binti: Baby naomba Namba yako ya Simu....
Jamaa: Ooh! honey I'm just using no-phone.....

Binti: naomba hiyo hiyo number...
Jamaa: Its just no-phone ,no number, no battery, no charger,no power....
 
Hii imetengenezwa kuondoa addiction ya simu,

kama una addiction ya kila dakika kuangalia simu unshuriwa kununua kifaa hiki, ili kila unapoigeuza simu kuiangalia unakutana nacho baada ya muda addiction ya kuiangalia simu itaisha so next time ukiwa na simu yako hutakuwa unaifunuafunua kila sekunde
 
Iphone nao wametoa pete za ndoa ambazo unaweza kumu-track mke/mume hawa jamaa wanawaza kupiga ela kwa kila njia hiyo no phone ndio wamenivunja mbavu tu aiseee......mabelari hatari
Hii kitu msiitangaze sana jama itakuwa majanga wengine watu wetu wamo humu naweza kesho nikaambiwa nikanunue pea za hizi pete ila kama za kuchaji poa siku itakayoisha charge ndio mwisho wake
 
Wazungu huwa ni vichaa sana sema tu kwavile wao hawaokoti makopo
 
Hiki kifaa ukinunua huku kwetu, ndugu zako watakuendea kwa madokta wale wa dodoma kimya kimya kufungua file kwa kujua tayari dishi lishacheza.
 
Back
Top Bottom