Ijue nchi ya Misri

Wazo Kuu

Senior Member
Oct 21, 2018
114
293
Jiografia
Misri imepakana na Bahari ya Mediteranea, Israel, Eneo la mamlaka ya Palestina, ghuba ya Suez, ghuba ya Aqaba, Bahari ya Shamu, Sudan na Libya. Umbo la nchi hufanana na trapeza.

Tabianchi ni yabisi sana na maeneo makubwa ni jangwa, pamoja na oasisi na maeneo ya savana ya miiba. Karibu wananchi wote huishi ndani ya kanda nyembamba ya bonde la mto Naili. Bonde hili linavuka nchi kuanzia mpakani na Sudani katika kusini kuelekea kaskazini hadi mdomo wa mto kwenye Bahari ya Mediteranea. Ardhi pande zote mbili za mto inamwagiliwa na kulimwa. Kwatika umbali mdogo kutoka mto jangwa inaanza.

Takriban kilomita 250 kabla ya mdomo Naili inagawanyika katika mikono mbalimbali na kuunda delta ya mto.

Kanda hili bichi si zaidi ya asilimia 5 za eneo lote la nchi, ila 98% za wananchi wote huishi humo.[1] Kwa hiyo Naili huitwa "Baba wa Misri", kwa maana bila mto huo pasingekuwepo taifa hili.

Mji mkuu wa Kairo uko mwanzoni mwa eneo la delta.

Nchi yote huwa na kanda asilia zifuatazo:

Oasisi ya mto Naili: mto umechimba bonde kama mfereji katika mwamba asilia ya nchi. Ndani ya bonde hili jembamba lenye upana hadi kilomita 25 kuna kanda la ardhi yenye rutuba kuanzia Ziwa Nasser hadi Kairo.

Delta ya Naili: upande wa kaskazini wa Kairo Naili inajigawa katika mikono miwili mikuu na kati ya mikono hiyo miwili kuna eneo la delta yenye km² 23,000 kwa umbo la pembetatu. Inajaa ardhi ya rutuba kutokana na matope ya Naili iliyopelekwa huko na mafuriko katika muda wa miaka elfu kadhaa. Eneo hili linalimwa kote na kumwagiliwa likiwa na mikono midogo ya kando ya Naili.

Jangwa la Magharibi: ni eneo kubwa upande wa magharibi wa Naili lisilo na milima mikubwa. Kaskazini mwake kuna tambarare ya Lybia iliyo takriban mita 240 juu ya uwiano wa bahari. Kusini mwake linainama eneo la mbonyeo wa Qatara hadi mita 133 chini ya UB, halafu jangwa linapanda tena juu kuelekea kusini magharibi.

Ndani ya eneo hili kubwa kuna beseni kadhaa pamoja na oasisi za Siwa, Bahariyya, Farafra, Dakhla na Charga. Kilomita 100 upande wa kusini-magharibi wa Kairo kuna oasisi kubwa ya Fayyum pamoja na ziwa la Warun lenye eneo la km² 230.

Jangwa la Mashariki: ni eneo upande wa mashariki wa mto Naili. Huko kuna milima inayopanda juu ya mita 2,000 pamoja na wadi yaani bonde kali. Jangwa linatelemka hadi mfereji wa Bahari ya Shamu ambao ni sehemu ya Bonde la Ufa linaloanza Palestina na kuendelea hadi Ziwa Nyasa.

Rasi ya Sinai: ni eneo la jangwa na milima inayofikia hadi mita 2637 (Jabal Katharina).

miri 1.jpeg

misri 3.jpeg
 
Hii nchi inategemea prymids tuu lkini uchumi wake uko juu balaa..nchi za africa lkini ukienda hutamini kama hpo ni africa
 
View attachment 2005511

View attachment 2005509
Kumbe eeh
 
Back
Top Bottom