Ijue maana halisi ya neno "Kanisa"

Ijue maana halisi ya neno "Kanisa"

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Ukipita huku na kule utaona vibao vimeandikwa: Kanisa la Anglikana, Kanisa Katoliki, Kanisa la Baptist, Kanisa la EAGT, Kanisa la Pentekoste, Kanisa la SDA n.k. Je, hiyo ndiyo maana halisi ya neno “Kanisa” kama ilivyokusudiwa katika Biblia? Je, Kanisa ni jengo au taasisi? Ili kuujua ukweli, ni lazima turudi kwenye Maandiko Matakatifu.

1. Maana ya Neno “Kanisa” kwa Kigiriki
Neno "Kanisa" limetafsiriwa kutoka neno la Kigiriki "Ekklesia" ambalo linamaanisha “the called-out ones," yaani watu walioitwa kutoka kwenye dunia ili wawe wa Mungu. Sio jengo, wala dhehebu, bali ni watu wanaomwamini Yesu Kristo, walioitwa watoke dhambini.

Katika Mathayo 16:18 Yesu anasema:
"...juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”

Yesu hajasema hapo kwamba atajenga dhehebu, bali Kanisa lake, yaani watu wa Mungu waliookolewa.

2. Kanisa sio Jengo, bali ni Watu
Mara nyingi watu wanachanganya Kanisa na jengo la kuabudia. Lakini Biblia haina tafsiri hiyo. Kanisa linafanywa na watu waliozaliwa mara ya pili kwa imani katika Kristo Yesu.

Ndio sababu Paulo anasema:
“...sisi tu Hekalu la Mungu aliye hai..."
— 2 Wakorintho 6:16

3. Kanisa ni Mwili wa Kristo
Biblia inaeleza kuwa Kanisa ni mwili wa Kristo, na Yesu ndiye kichwa cha mwili huo.
“Wakolosai 1:18
Naye[Yesu] ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa..."
— Wakolosai 1:18

Kwa mantiki hiyo hakuna dhehebu linaloweza kujihesabu kuwa ni “kanisa kamili” peke yake.

Kanisa ni muunganiko wa watu wote duniani wanaoamini, sio shirika au jina la dhehebu. Kwahiyo sio sahihi kusema eti hili ni "Kanisa la KKT," "Kanisa la Presbyterian" au "Kanisa la TAG." Hayo ni madhehebu.

Tafsiri potofu ya neno "Kanisa" ndiyo inayoleta matengano na kuvuruga umoja aliotuombea Yesu tuwe nao.
“...ili wawe na umoja kama vile wewe Baba ulivyo ndani yangu na mimi nilivyo ndani yako...”
— Yohana 17:21

Migawanyiko ya kimadhehebu ndiyo inayosababisha watu wa dhehebu moja kujiona bora kuliko watu wa dhehebu jingine, kiasi kwamba wengine wanaenda mbali zaidi na kusema "Sisi ndio Kanisa la asili. Wengine ni vijikanisa!" Kibiblia, watu wanaomwamini Yesu hata wakiwa wawili au watatu katika nyumba fulani, ni Kanisa, sio kijikanisa. Angalia Paulo anavyosema hapa:
Rum 16:4 SUV
"...nisalimieni na kanisa lililomo katika nyumba yao."
Kanisa hilo linalosalimiwa na Paulo ni watu wachache tu waliokusanyika kama kanisa la nyumbani(katika nyumba ya Prisila na Akila — wanandoa Wayahudi waliomwamini Yesu Kristo na kumsaidia Paulo katika huduma).

Mpaka hapo naamini umeona wazi sasa kuwa kwa mtazamo wa kibiblia, Kanisa ni watu wote wanaomwamini Yesu Kristo(popote walipo duniani, wawe wawili au watatu), bila kujali wapo katika dhehebu au taasisi gani. Kanisa ni watu waliompokea Roho Mtakatifu, na wanaoishi maisha matakatifu na kumtii Mungu. Sio jengo, sio dhehebu, wala shirika la kidini. Hivyo, matumizi ya maneno kama "Kanisa la Mennonite au Kanisa la Ufufuo" ni matumizi ya kibinadamu tu, yasiyoakisi maana halisi ya neno Kanisa kama lilivyokusudiwa na Yesu Kristo.

cc: johnthebaptist The Watchman Pascal Mayalla CONTROLA Ozon
 
Yesu yuaja upesi(Ufu 22:12) kulinyakua Kanisa. Kanisa atakalolinyakua sio dhehebu fulani. Ni watu watakatifu, wasio na chembe chembe yoyote ya dhambi.
Waefeso 5:27 NENO
"...apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na doa wala kunyanzi au waa lolote, bali takatifu na lisilo na hatia."
 
Ukipita huku na kule utaona vibao vimeandikwa: Kanisa la Anglikana, Kanisa Katoliki, Kanisa la Baptist, Kanisa la EAGT, Kanisa la Pentekoste, Kanisa la SDA n.k. Je, hiyo ndiyo maana halisi ya neno “Kanisa” kama ilivyokusudiwa katika Biblia? Je, Kanisa ni jengo au taasisi? Ili kuujua ukweli, ni lazima turudi kwenye Maandiko Matakatifu.

1. Maana ya Neno “Kanisa” kwa Kigiriki
Neno "Kanisa" limetafsiriwa kutoka neno la Kigiriki "Ekklesia" ambalo linamaanisha “the called-out ones," yaani watu walioitwa kutoka kwenye dunia ili wawe wa Mungu. Sio jengo, wala dhehebu, bali ni watu wanaomwamini Yesu Kristo, walioitwa watoke dhambini.

Katika Mathayo 16:18 Yesu anasema:
"...juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”

Yesu hajasema hapo kwamba atajenga dhehebu, bali Kanisa lake, yaani watu wa Mungu waliookolewa.

2. Kanisa sio Jengo, bali ni Watu
Mara nyingi watu wanachanganya Kanisa na jengo la kuabudia. Lakini Biblia haina tafsiri hiyo. Kanisa linafanywa na watu waliozaliwa mara ya pili kwa imani katika Kristo Yesu.

Ndio sababu Paulo anasema:
“...sisi tu Hekalu la Mungu aliye hai..."
— 2 Wakorintho 6:16

3. Kanisa ni Mwili wa Kristo
Biblia inaeleza kuwa Kanisa ni mwili wa Kristo, na Yesu ndiye kichwa cha mwili huo.
“Wakolosai 1:18
Naye[Yesu] ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa..."
— Wakolosai 1:18

Kwa mantiki hiyo hakuna dhehebu linaloweza kujihesabu kuwa ni “kanisa kamili” peke yake.

Kanisa ni muunganiko wa watu wote duniani wanaoamini, sio shirika au jina la dhehebu. Kwahiyo sio sahihi kusema eti hili ni "Kanisa la KKT" "Kanisa la Presbyterian" au "Kanisa la TAG." Hayo ni madhehebu.

Tafsiri potofu ya neno "Kanisa" ndiyo inayoleta matengano na kuvuruga umoja aliotuombea Yesu tuwe nao.
“...ili wawe na umoja kama vile wewe Baba ulivyo ndani yangu na mimi nilivyo ndani yako...”
— Yohana 17:21

Migawanyiko ya kimadhehebu ndiyo inayosababisha watu wa dhehebu moja kujiona bora kuliko watu wa dhehebu jingine, kiasi kwamba wengine wanaenda mbali zaidi na kusema "Sisi ndio Kanisa la asili. Wengine ni vijikanisa!" Kibiblia, watu wanaomwamini Yesu hata wakiwa wawili au watatu katika nyumba fulani, ni Kanisa, sio kijikanisa. Angalia Paulo anavyosema hapa:

Rum 16:4 SUV
"...nisalimieni na kanisa lililomo katika nyumba yao."
Kanisa hilo linalosalimiwa na Paulo ni watu wachache tu waliokusanyika kama kanisa la nyumbani(katika nyumba ya Prisila na Akila — wanandoa Wayahudi waliomwamini Yesu Kristo na kumsaidia Paulo katika huduma).

Mpaka hapo naamini umeona wazi sasa kuwa kwa mtazamo wa kibiblia, Kanisa ni watu wote wanaomwamini Yesu Kristo(popote walipo duniani) bila kujali wapo katika dhehebu au taasisi gani. Kanisa ni watu waliompokea Roho Mtakatifu, na wanaoishi maisha matakatifu na kumtii Mungu. Sio jengo, sio dhehebu, wala shirika la kidini. Hivyo, matumizi ya maneno kama "Kanisa la Mennonite au Kanisa la Ufufuo" ni matumizi ya kibinadamu tu, yasiyoakisi maana halisi ya neno Kanisa kama lilivyokusudiwa na Yesu Kristo.

cc: johnthebaptist The Watchman Pascal Mayalla CONTROLA Ozon
Mkuu Set free asante kwa elimu hii。
“Wakusanyikapo wawili au watatu kwa ajili ya jina langu,nami nipo kati yao”

Hii elimu ya kanisa ni muhimu sana,kuna wengi wanaliabudu jengo la kuabudia wakijua ndio kanisa!。Angalizo: Kuna Wengi Wanamwabudu Shetani Wakidhani ni Mungu!. Jee Wewe Unajijua?, Jitambue!.

P
 
Neno "Kanisa" limetafsiriwa kutoka neno la Kigiriki "Ekklesia"
Maelezo yanayoelezea dhana ya kikanisa (ecclesiology) ya kanisa Katoliki linaelezwa kama muungano wa wanadamu, wanaoamini imani moja ya Kikristo, wanaoshiriki katika sakramenti zile zile, walioko chini ya uongozi wa wachungaji halali (maaskofu, mapadre, na maaskofu wakuu, wanaongoza kwa mujibu wa mamlaka halali ya Kanisa na chini ya askofu wa Roma (Papa). Je, kwa maana hii "makanisa mengine sio kanisa." ??
 
Hawakutakiwa kulifunga bali kudeal na mhusika, tatizo mhusika ana nguvu ya ziada + akili na hela
 
Maelezo yanayoelezea dhana ya kikanisa (ecclesiology) ya kanisa Katoliki linaelezwa kama muungano wa wanadamu, wanaoamini imani moja ya Kikristo, wanaoshiriki katika sakramenti zile zile, walioko chini ya uongozi wa wachungaji halali (maaskofu, mapadre, na maaskofu wakuu, wanaongoza kwa mujibu wa mamlaka halali ya Kanisa na chini ya askofu wa Roma (Papa). Je, kwa maana hii "makanisa mengine sio kanisa." ??
Asante sana Ozon kwa maelezo yako juu ya ecclesiology ya Kanisa Katoliki. Niseme tu hivi kwamba hayo ni maelezo ya dhehebu la Katoliki. Lakini kwa mujibu wa Maandiko Matakatifu, maana halisi ya "Kanisa" ni watu wote wanaomwamini Yesu Kristo kwa kweli na waliookolewa kwa njia ya imani.

Kumbuka kuwa neno “Kanisa” limetafsiriwa kutoka katika lugha ya Kigiriki “Ekklesia” ambalo linamaanisha:
“Watu walioitwa kutoka katika ulimwengu wa dhambi na kuja kwa Mungu” — yaani waamini wanaomkubali Yesu Kristo, waliotakaswa kwa damu yake, na wanaoishi kwa kutii Neno lake.

Hii inaonekana wazi katika maandiko yafuatayo:
Matendo 2:47:
“...Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa..”
Hapo, “Kanisa” ni wale waliokuwa wakiokolewa – si mfumo au taasisi.

Waefeso 5:25–27: “…Kristo alilipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake… apate kujiletea Kanisa takatifu lisilo na ila wala kunyanzi.”

Yesu atarudi kulitwaa Kanisa takatifu, sio dhehebu fulani, bali watu waliotakaswa katika kweli.
 
Ukipita huku na kule utaona vibao vimeandikwa: Kanisa la Anglikana, Kanisa Katoliki, Kanisa la Baptist, Kanisa la EAGT, Kanisa la Pentekoste, Kanisa la SDA n.k. Je, hiyo ndiyo maana halisi ya neno “Kanisa” kama ilivyokusudiwa katika Biblia? Je, Kanisa ni jengo au taasisi? Ili kuujua ukweli, ni lazima turudi kwenye Maandiko Matakatifu.

1. Maana ya Neno “Kanisa” kwa Kigiriki
Neno "Kanisa" limetafsiriwa kutoka neno la Kigiriki "Ekklesia" ambalo linamaanisha “the called-out ones," yaani watu walioitwa kutoka kwenye dunia ili wawe wa Mungu. Sio jengo, wala dhehebu, bali ni watu wanaomwamini Yesu Kristo, walioitwa watoke dhambini.

Katika Mathayo 16:18 Yesu anasema:
"...juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”

Yesu hajasema hapo kwamba atajenga dhehebu, bali Kanisa lake, yaani watu wa Mungu waliookolewa.

2. Kanisa sio Jengo, bali ni Watu
Mara nyingi watu wanachanganya Kanisa na jengo la kuabudia. Lakini Biblia haina tafsiri hiyo. Kanisa linafanywa na watu waliozaliwa mara ya pili kwa imani katika Kristo Yesu.

Ndio sababu Paulo anasema:
“...sisi tu Hekalu la Mungu aliye hai..."
— 2 Wakorintho 6:16

3. Kanisa ni Mwili wa Kristo
Biblia inaeleza kuwa Kanisa ni mwili wa Kristo, na Yesu ndiye kichwa cha mwili huo.
“Wakolosai 1:18
Naye[Yesu] ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa..."
— Wakolosai 1:18

Kwa mantiki hiyo hakuna dhehebu linaloweza kujihesabu kuwa ni “kanisa kamili” peke yake.

Kanisa ni muunganiko wa watu wote duniani wanaoamini, sio shirika au jina la dhehebu. Kwahiyo sio sahihi kusema eti hili ni "Kanisa la KKT," "Kanisa la Presbyterian" au "Kanisa la TAG." Hayo ni madhehebu.

Tafsiri potofu ya neno "Kanisa" ndiyo inayoleta matengano na kuvuruga umoja aliotuombea Yesu tuwe nao.
“...ili wawe na umoja kama vile wewe Baba ulivyo ndani yangu na mimi nilivyo ndani yako...”
— Yohana 17:21

Migawanyiko ya kimadhehebu ndiyo inayosababisha watu wa dhehebu moja kujiona bora kuliko watu wa dhehebu jingine, kiasi kwamba wengine wanaenda mbali zaidi na kusema "Sisi ndio Kanisa la asili. Wengine ni vijikanisa!" Kibiblia, watu wanaomwamini Yesu hata wakiwa wawili au watatu katika nyumba fulani, ni Kanisa, sio kijikanisa. Angalia Paulo anavyosema hapa:
Rum 16:4 SUV
"...nisalimieni na kanisa lililomo katika nyumba yao."
Kanisa hilo linalosalimiwa na Paulo ni watu wachache tu waliokusanyika kama kanisa la nyumbani(katika nyumba ya Prisila na Akila — wanandoa Wayahudi waliomwamini Yesu Kristo na kumsaidia Paulo katika huduma).

Mpaka hapo naamini umeona wazi sasa kuwa kwa mtazamo wa kibiblia, Kanisa ni watu wote wanaomwamini Yesu Kristo(popote walipo duniani, wawe wawili au watatu), bila kujali wapo katika dhehebu au taasisi gani. Kanisa ni watu waliompokea Roho Mtakatifu, na wanaoishi maisha matakatifu na kumtii Mungu. Sio jengo, sio dhehebu, wala shirika la kidini. Hivyo, matumizi ya maneno kama "Kanisa la Mennonite au Kanisa la Ufufuo" ni matumizi ya kibinadamu tu, yasiyoakisi maana halisi ya neno Kanisa kama lilivyokusudiwa na Yesu Kristo.

cc: johnthebaptist The Watchman Pascal Mayalla CONTROLA Ozon
Kanisa ni watu waliompokea Roho Mtakatifu, na wanaoishi maisha matakatifu na kumtii Mungu. Sio jengo, sio dhehebu, wala shirika la kidini.
 
Great! Umenukuu vizuri sana.
 
Back
Top Bottom