lukindo
JF-Expert Member
- Mar 20, 2010
- 8,466
- 9,028
hili kaburi lipo opposite na NBC Samora na sio NMB kama alivyopost. Ukweli kidogo uliopo ni kuwa liliibuka wakati wa utawala wa Mzee Mwinyi lakini (sina uhakika) kulikuwa hakuna kitu na baadhi ya marafiki (nadhani waislamu) wakaibuka na kusema aliwahi kuzikwa Ustaadh mmoja siku za nyuma. Watu waliamka asubuhi wakakuta limejengewa na baada ya ubishi kidogo yakaingizwa mambo ya udini, nadhani Mzee Kitwana Kondo ndiye alikuwa Mayor. Katika mivutano zaidi ndiyo wakaliwekea kabisa tiles.
Lakini fikiria tangia dunia iumbwe, kweli ni rahisi kujua ni sehemu gani watu wote waliowahi kuishi walizikwa wapi ili kupajengea makaburi!? Kwa vile aliyezikwa pale hajulikani bali kuna hizo assumptions, ni bora tu kungebakishwa bustani maana nazo zinatukuza waliokufa lakini lile kaburi 'linastua'

Mimi nalijua vizuri sana lipo maeneo ninako ishi. Marehemu ni MTANZANIA wa kwanza kuwa IMAMU ktk miaka hiyo ya 1800. Usisahau maunganisho yale ni ya mitaa ya Msikiti na India na yanaendelea hadi Samora. Jina lake silikumbuki. Asante. kaburi hili limekuwa kama limetupwa lakini ni historia nzuri sana. Japo linatunzwa hakuna kibao chochote cha kuonyesha historia ya IMAMU wetu huyu.