Ijue Botswana japo kidogo tu

Free state ni jimbo la wazungu by then na mji wake mkuu ni Bloemfontein ni pazuri sana sana, na hakuna sana ujingaujinga kama wa Jos Au Pretoria wa kuchoma visu na bunduki japo matukio yapo
Poa poa mkubwa
 
Botswana ni moja kati ya nchi nzuri kuishi Africa, INA democrasia yenye vyama vingi. NI KAMA TANZANIA TANGU UHURU NI CHAMA KIMOJA TU KIKO MADARAKANI. PIA KULE HAKUNA WANASIASA WAONGO WAONGO KAMA AKINA LEMA, AKINA MSIGWA, NK. Setswana lugha yao inafanana sana na lugha ya xhoza. Miji yao imepangika vizuri sana mfano Gaborone, Lobatse- near border to RSA, Francis town, Selowi, Maun, CHOMA, Molepolole, Kanye,nk .
Hao jamaa wako vizuri kiuchumi kwa bahati nzuri ni wachache sana chini ya milioni 5 tu nchi kubwa namna ile. Barabara nyingi zina kiwango cha tarmac.
Hakuna kelele nyingi kama TZ, hakuna mambo ya kick za hovyo hovyo.
 
Almasi iligungunduliwa baada ya kupata uhuru na wamehakikisha faida inayopatikana inasaidia wananchi. Wako vizuri sana katika sekta ya elimu, afya na ustawi wa jamii. Wazee wakifikisha miaka 55 wanalipwa state pension kila mwisho wa mwezi ambayo ni sawa na kima cha chini cha mshahara.
 

Ni kweli, Lakini pia kuna Wakalanga ambao wapo kuanzia Tonota, Francistown na wanaingia mpaka Zimbabwe, hawa ni wabantu sio waKhoi au wasan na ndio walienda Shule na ndio wanashikilia idara zote muhimu, wamejaa sana Jeshini, polizi, uhamiaji nk, wao majina yao ni kama yetu tu na lugha yao ni sehemu ya washona wa Zimbabwe

Kweli wako wachache actually wako chini ya 3Mil
 
Hata milioni 4 hawajafika
 

Ni kweli kabiasa, unajua hawa wazungu nchi ambazo hakikuwa na masilahi kwao walizipa uhuru mapema sana. Kwa Botswana ilionekana ni jangwa tu na cha maana kilichoonekana ni coal na shaba kidogo upande wa Maun kwenye mpaka na Zambia (Coppet belt)
Hivyo Botswana ilipata uhuru 1966 ikipakana na Zimbabwe 1980, Namibia 1990' na South Africa 1994, so Botswana iliachwa ikiwa haina kitu, eneo lake lililokuwa liko fertile (Mafikeng) likachukuliwa na South Africa

Kaunda wa Zambia ndio alikuwa anawalipa mishahara civil servant wa Botswana (police, walimu nk), na barabara ya kutoka Francistown mpaka Kazungura border post mpaka livingstone-Lusaka imetengenezwa na Kaunda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…