Elections 2010 Igunga: Nani ataibuka kidedea kati ya hawa?

KURA YA MAONI: VOTE Online IGUNGA ELECTION

  • Total voters
    93
  • Poll closed .
KUMEKUCHA HAPO MAGAMBA WANAKAZI KUBWA. HUYO TUMBO NI JEMBE LA UKWELI WAKAE MKAO WA KULIWA
peeeeeoplesssssssssss poweeeeeeeeeeer
 
Hii ngoma bado mbichi kabisa, subiri kampeni zianze, tathmini itatokana na mahudhurio ya watu kwenye mikutano ya kampeni.
 
Majibu haya yanapingana na ya Slaa alipojibu maswali hapa Jf j2 fulani zilizopita, kwani alikiri na kusema Igunga inahitaji mwana Igunga anayejua matatizo ya pale siyo kwa kuhadithiwa. sasa unapompeleka mtu mwa kisesa igunga hiyo ni dhahiri kuwa ni tamaa ya madaraka na sio uwakilishi, kwani unataka uniambie wilaya nzima hawana muwakilishi mpaka cdm mumpeleke mtu wa mbali? kwahilo mngekiri kuchemka. hapo upinzani itakuwa baina ya Amina said Fundikira na Lucas Mahona na hapo magamba watafanya kila mbinu Naye Mzee fundikira apate mlith serikalini

''kwani unataka uniambie wilaya nzima hawana muwakilishi mpaka cdm mumpeleke mtu wa mbali? kwahilo mngekiri kuchemka.'' Nani kasema Tumbo kapelekwa Igunga na chama?? Tumbo kama mwanachama anahaki ya kuwa kiongozi. Kamati itakaa na kufilter majina na hatimaye watapata mtu mwenye vigezo.

CDM sio kama magamba ambao viongozi wao wanateua mgombea kwa fitna. Ref. Uteuzi wa Anne Makinda, Kingwangala et al
 
quote_icon.png
By Mr.Mak
Majibu haya yanapingana na ya Slaa alipojibu maswali hapa Jf j2 fulani zilizopita, kwani alikiri na kusema Igunga inahitaji mwana Igunga anayejua matatizo ya pale siyo kwa kuhadithiwa. sasa unapompeleka mtu mwa kisesa igunga hiyo ni dhahiri kuwa ni tamaa ya madaraka na sio uwakilishi, kwani unataka uniambie wilaya nzima hawana muwakilishi mpaka cdm mumpeleke mtu wa mbali? kwahilo mngekiri kuchemka. hapo upinzani itakuwa baina ya Amina said Fundikira na Lucas Mahona na hapo magamba watafanya kila mbinu Naye Mzee fundikira apate mlith serikalini
Dah!..Picha inaanza kuwa pana zaidi haya mambo madogo madogo muhimu yanaanza kujitokeza...na sidhani kama Chadema walikuwa na ofisi za chama jimboni hapa miaka ya nyuma. Pia yaonyesha Chadema hawakuwa na mgombea uchaguzi ulopita 2010..Sii mchezo mdogo.
 
Chadema wana diwani tena mjini Igunga kwa hiyo ofisi ipo hiyo toa wasiwasi, kweli hawakuwa na mgombea ubunge Igunga lakini pamoja na hayo kura za urais jimbo hilo zinaonyesha chama kinakubalika hata bila kuwa na mgombea ubunge itakuwaje wakati huu wakati mgombea yupo.
 
Vizuri sana, nani mwenyekiti wa chama pale Igunga na Ofisi ziko wapi! - kuna mtu nataka muwasiliane naye...
 
Vizuri sana, nani mwenyekiti wa chama pale Igunga na Ofisi ziko wapi! - kuna mtu nataka muwasiliane naye...
Siku hizi huna kitu zaidi ya upenzi unatabiri ulisomea wapi ushehe yahya unataka kutuambia diwani alipatikana chini ya mti.
 
Hongereni Joseph Kashindye na Peter Kafumu kwa kuwakilisha vyama vyenu wana Igunga wamewaamini najua mmoja wenu atakuwa mbunge.
 
Mpaka sasa chama cha mapinduzi kinaongoza kwa kuwa na wafuazi wengi wa
kukipigia kura. vyama vingine vinafuata kuwa na wafuasi wa vyama vingine

Je nje ya igunga Mtazamo wa wapiga kura ukoje?
Kama ungekuwa mwana Igunga kura yako ungempa nani?1. Leopold Mahona (CUF)
2.Joseph Kashindye (CHADEMA)
3. Peter Kafumu (CCM)
4. Said Makeni (DP)
5.Lazaro Ndageya (UMD)
6. John Maguma (SAU)
 
no research, no right to speak......
 
Huku wengi ni CDM.. Igunga Internet inapatikana kwa tabu sna na ni ni wachache wako aware.
 
Huku wengi ni CDM.. Igunga Internet inapatikana kwa tabu sna na ni ni wachache wako aware.

Japokuwa tunnadhani ni maoni ya wale walio na uwezo wa kuaccess internet popote pale walipo.

Haina maana kwamba Igunga wako pamoja na ulimwengu nje ya igunga awataka wawe kama wengi waliopiga kura hizo.
 
Mpaka sasa chama cha mapinduzi kinaongoza kwa kuwa na wafuazi wengi wa
kukipigia kura. vyama vingine vinafuata kuwa na wafuasi wa vyama vingine

Je nje ya igunga Mtazamo wa wapiga kura ukoje?
Kama ungekuwa mwana Igunga kura yako ungempa nani?1. Leopold Mahona (CUF)
2.Joseph Kashindye (CHADEMA)
3. Peter Kafumu (CCM)
4. Said Makeni (DP)
5.Lazaro Ndageya (UMD)
6. John Maguma (SAU)

[h=3]This poll will close on 21st October 2011 at 10:34[/h]
  • Peter Kafumu (CCM) - 2 10.53%

  • Said Makeni (DP) -0 0%

  • Leopold Mahona (CUF) -0 0%

  • Lazaro Ndageya (UMD) -0 0%

  • John Maguma (SAU) -0 0%

  • Joseph Kashindye (CHADEMA) - 17 89.47%

WANAZUONI wa Kiislamu nchini wameipa siku tatu Chadema Taifa kulaani kitendo cha wafuasi na viongozi wake kulidhalilisha vazi tukufu la hijab na kumwomba radhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario, kwa kumvua sitara yake.

Wamesema iwapo chama hicho kitapuuza kufanya hivyo na kupita muda huo wanazuoni hao na Waislamu wataiona Chadema kama chama chenye sera na madhumuni ya kuhujumu Uislamu na Waislamu wa Tanzania na kuhimiza Waislamu kukiepuka kama ukoma.

Kauli hiyo iko kwenye tamko la Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (HAY-AT) lililosomwa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti Kuu ya Umoja huo, Shehe Sherali Hussein Sherali na kusema siku tatu hizo zilianza jana.

Wanazuoni hao zaidi ya 10 wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Shehe Suleimani Kilemile, walitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari na kusema baada ya hapo umoja huo utakaa na kutafakari hatua stahiki za kukabiliana na dharau hizo na kuelekeza Waislamu cha kufanya.

Sherali alisema ifahamike, kwamba shambulio lolote dhidi ya hijab ni dhidi ya Uislamu na Waislamu wote, haliwezi kuvumilika na watakabiliana na yeyote anayetaka kuidhalilisha amri ya hijab iliyo katika Quran sura ya 33:59.

"Tunataka ifahamike, kwamba yeyote atakayelidharau vazi la hijab kwa kauli au vitendo, atakuwa amewachokoza Waislamu na sisi kamwe hatukubali hilo liendelee na kukaa kimya, tutachukua hatua stahiki na ikibidi tutalazimika kuondoa munkari kwa mikono yetu wenyewe, kama dini yetu inavyotuelekeza," alisema.

Aliongeza kuwa wanalaani na kupinga kitendo kilichofanywa na wanaodaiwa kuwa wafuasi na viongozi wa Chadema kumvua nguo Mkuu huyo wa Wilaya na kumwacha bila sitara.

Alisema Kimario ni Mwislamu anayefuata mafundisho ya Uislamu yanayomtaka kila
mwanamke ajisitiri kwa vazi la hijab, hivyo kumvua ni kumdhalilisha kwa wanajamii kama mwanamke wa Kiislamu, mama mwenye watoto na kiongozi wa Serikali.

Tumetafakari tukio hili kwa undani na tunalichukulia kama shambulio la wazi na la makusudi dhidi ya mafundisho yetu na dini ya Kiislamu, yanayomtaka kila mwanamke aliyevunja ungo, kujisitiri kwa kuvaa vazi la hijab," alisema Sherali.

Aliwaomba Watanzania wote, wanaharakati wa asasi za kijamii na wa haki za binadamu, viongozi wa vyama vya siasa na wa dini zote, kulaani na kupinga unyanyasaji huo wa kijinsia na kidini unaokwenda kinyume na Katiba ya nchi na utamaduni wa Watanzania wa kuheshimiana.

"Tumesikitishwa na ukimya wa asasi za kijamii zinazodai kutetea haki za binadamu na za wanawake, kutolaani kitendo hiki cha mwenzao kudhalilishwa kijinsia, kuendelea kukaa kimya kunatulazimisha kuwaona wanafiki na ndumilakuwili juu ya madai yao ya kutetea wanawake," alisisitiza.

Alisema wanaitaka Serikali ilitafakari kwa kina tukio hili la kudhalilishwa mwanamke Mwislamu, akilitumikia Taifa kama mmoja wa viongozi wake, kukaa kimya kutatoa tafsiri hasi juu ya jinsi inavyolichukulia tukio hilo na kuitaka kuwachukulia hatua kali wahusika.

Wanawake Waislamu Katika hatua nyingine, kikao cha wanawake Waislamu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee Jumapili, wanawake walilaani tukio hilo.

Kikao hicho chini ya Mwenyekiti wake Fatma Juma, kiliwataka wanawake na wapenda amani wote kulaani kitendo hicho cha udhalilishaji wanawake.

Walisema kitendo hicho kimeonesha dharau, si tu kwa Uislamu, bali hata kwa madhehebu mengine na kinaweza kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini hivi sasa.

Tamko la kikao hicho, lilisema litaanza kusambazwa katika misikiti yote Ijumaa, ili Waislamu waelewe namna walivyoguswa na kusononeshwa na tukio hilo.

Shura ya Maimamu
Habari zaidi zilizopatikana zilisema Shura ya Maimamu nayo itakutana hivi karibuni kujadili tukio hilo la mwanamke wa Kiislamu kuvuliwa hijab.

Mbali ya kukutana huko, Shura hiyo itaandaa maandamano ya kupinga kitendo hicho ambacho wamekitafsiri kuwa ni matusi dhidi ya Uislamu.

Katibu wa Shura ya Maimam, Shehe Ponda Issa Ponda, jana alithibitisha kuwapo kwa ajenda hiyo.

Akizungumza na gazeti hili jana alisema kitendo kilichofanywa na wafuasi wa Chadema kimekosa utu, ustaarabu, uungwana na maadili mema na kinapaswa kukemewa na wapenda amani wote nchini, bila kujali itikadi zao, kwani kikiachwa kitazidi kukomaa na kuonekana ni
jambo la kawaida katika jamii.

Akizungumzia kadhia hiyo, Katibu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini (Baraza Kuu), Shehe Ramadhan Sanze, naye alisema taasisi yake inaungana na wanaolaani tukio hilo .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom