IGP Wambura afanya mabadiliko mengine ya Makamanda wa Polisi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,355
8,043
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillius Wambura amefanya mabadiliko ya Makamanda wa Polisi wa mikoa ili kuboresha na kuongeza ufanisi wa utendaji katika mikoa mitatu ya Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Januari 6, 2023 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, IGP Wambura amemhamisha aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim kwenda kitengo cha Mipango, Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

Taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi inaeleza kuwa nafasi ya Kamanda Muslim imechukuliwa na Alex Mukama ambae alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe.

Vilevile, IGP Wambura amemhamisha kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa, Theopista Mallya kwenda kuwa kamanda wa polisi mkoa wa Songwe.

Shadrack Masija ambae alikuwa Ofisa Mnadhimu namba moja mkoa wa Simiyu, naye amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom