IGP: Sheria haielezi nini maana ya mikutano ya ndani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,876
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro amesema kuna changamoto ya kutokuwepo sheria inayoeleza maana ya mikutano ya ndani.

Ameyasema hayo leo Alhamisi Septemba 23, 2021 alipokutana na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mikutano ya vyama vya siasa na changamoto zinazojitokeza baina ya jeshi hilo na baadhi ya vyama.

“Jambo la kwanza tulikuwa tunaangalia changamoto zinazojitokeza kwa baadhi ya vyama vya siasa ambavyo vimekuwa vikilalamika kuzuiwa kufanya mikutano yao ya ndani” amesema Sirro.

Naye Jaji Mutungi amesema kupitia kikao hicho yapo mambo waliyoyachukua ambayo watayaunganisha na mengine watakayoyapata kwenye kikao na vyama vya siasa.

"Hata hawa wanasiasa tutawaeleza mambo yaliyosemwa na wadau wengine ikiwemo Jeshi la Polisi. Msingi wa vikao hivi ni kutaka kupunguza misuguano isiyokuwa ya lazima na leo nimegundua wakati mwingine polisi wanakuwa na nia njema lakini raia tumekuwa hatujui,” amesema Jaji Mutungi.
 
IGP Sirro namkubali ni mzalendo wa kweli kwa Taifa lake asiye tetereka wala kuyumbishwa.
ni mfano mzuri kwa viongozi wengine.
Mungu azidi kumlinda na kumpa nguvu zaidi ya kulitumikia Taifa lake.
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro amesema kuna changamoto ya kutokuwepo sheria inayoeleza maana ya mikutano ya ndani.

Ameyasema hayo leo Alhamisi Septemba 23, 2021 alipokutana na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mikutano ya vyama vya siasa na changamoto zinazojitokeza baina ya jeshi hilo na baadhi ya vyama.

“Jambo la kwanza tulikuwa tunaangalia changamoto zinazojitokeza kwa baadhi ya vyama vya siasa ambavyo vimekuwa vikilalamika kuzuiwa kufanya mikutano yao ya ndani” amesema Sirro.

Naye Jaji Mutungi amesema kupitia kikao hicho yapo mambo waliyoyachukua ambayo watayaunganisha na mengine watakayoyapata kwenye kikao na vyama vya siasa.

"Hata hawa wanasiasa tutawaeleza mambo yaliyosemwa na wadau wengine ikiwemo Jeshi la Polisi. Msingi wa vikao hivi ni kutaka kupunguza misuguano isiyokuwa ya lazima na leo nimegundua wakati mwingine polisi wanakuwa na nia njema lakini raia tumekuwa hatujui,” amesema Jaji Mutungi.
Rubbish!
 
Hapo wanatafuta gap kubana mikutano ya kisiasa maana kama sheria haielezi kwani wao ni kazi yao kutafasiri sheria, Polisi kazi yao kusimamia sheria mbona wanajipa majukumu yasiyowahusu, je wanapata wapi uhalali wa kuzuia mikutano ambayo hawaijui? Na mbona mikutano ya chama tawala huwa haipigwi zengwe jamani watanzania sio wajinga mbaya zaidi kuna majobless wako mtaani haya ni suala la muda tu
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro amesema kuna changamoto ya kutokuwepo sheria inayoeleza maana ya mikutano ya ndani.

Ameyasema hayo leo Alhamisi Septemba 23, 2021 alipokutana na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mikutano ya vyama vya siasa na changamoto zinazojitokeza baina ya jeshi hilo na baadhi ya vyama.

“Jambo la kwanza tulikuwa tunaangalia changamoto zinazojitokeza kwa baadhi ya vyama vya siasa ambavyo vimekuwa vikilalamika kuzuiwa kufanya mikutano yao ya ndani” amesema Sirro.

Naye Jaji Mutungi amesema kupitia kikao hicho yapo mambo waliyoyachukua ambayo watayaunganisha na mengine watakayoyapata kwenye kikao na vyama vya siasa.

"Hata hawa wanasiasa tutawaeleza mambo yaliyosemwa na wadau wengine ikiwemo Jeshi la Polisi. Msingi wa vikao hivi ni kutaka kupunguza misuguano isiyokuwa ya lazima na leo nimegundua wakati mwingine polisi wanakuwa na nia njema lakini raia tumekuwa hatujui,” amesema Jaji Mutungi.
Hata mikutano ya ndani ya CCM pia sheria hailezi ama ni ya vyama vya upinzani tuu ?
 
Back
Top Bottom